Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,582
Ukiona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji kichwa chako ndicho kitakachofuatia.
Panapofuka moshi, chini kuna moto, na ukiona kwa mwenzako kunaungua, kwako kunateketea!
Nimeangalia breaking news ya Sky News, Serikali ya Uingereza imeamua kubana matumizi, mawaziri hakuna fungu la mafuta (fuel allowance) na badala yake ni lazima kutumia public transport. Hakuna tena kusafiri daraja la kwanza, first class, kwa watumishi wote wa umma!.
Hizi ndizo hizo dalili za kufuka kwa moshi, ama huko kunaungua, basi kwetu kunateketea.
Uingereza ndiyo nchi inayochangia fungu kubwa kuliko nchi nyingine yoyote kwenye lile kapu kubwa la hazina kwa jina la General Budget Support, kama mtoaji anaanza kubana matumizi, sidhani kama ataendelea kuchangia bajeti yetu ambapo mawaziri bado wanajivinjari kwa ma 4-wheel huku mwenye pesa akipanda dala dala. Au wanene wetu wakisafiri 1st Class huku mwenye pesa akisafiri Economy, au Bussiness.
Taarifa hii ni angalizo tuu kufuatia dalili ya mvua.
Pia sio vibaya kujiuliza kama wenye hela, wameamua hakuna kupata 1st Class, sisi masikini wa kutupwa tunapandia nini hizi 1st Class?!.
Kama Tanzania imepata uhuru wake zaidi ya miaka 46 iliyopita, kitendo cha kuendelea kutegemea bajeti tegemezi, sio kipimo tosha cha failed economy ya chama kilichoshika nchi, tufike mahali tukiweke pembeni na kufungua ukurasa mpya?.
Pamoja na utajiri mkubwa wa ardhi yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, kuanzia maziwa, mito, vijito, chemchemi, mifereji mpaka mabwawa, lakini kilimo chetu kwanini bado kinategemea mvua mpaka leo?!.
Tumezungukwa na madini ya kila aina, kuanzia Almasi, dhahabu, Tanzanite, chuma, shaba, fedha, vito kedekede, nk, nk huu umasikini unatokana na nini?!.
Watanzania tufike mahali tuseme basi!, imetosha!.
Mungu Ibariki Tanzania,