Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Oky Inaendelea...........


Basi siku yenyewe ilivyofika jamaaa alinishitua kutoka usingizini akaniambia bro ndio siku yenyewe ya maziwa na asali lakini kucheki kwa njee ilikuwa ni kama asubuhi tayari imeshafika nikabaki kujiuliza hivi mganga alituambia twende usiku saa 7 au asubuhi

Ilibidi niamke nianze kujiandaa kila mmoja alikuwa amejipanga jinsi anavyoweza kwa sekeseke nilikuwa nimekutana nalo ilibidi nivae viatu vya michezo wengine wanaita six ,halafu kamba nimezifungia miguuni nimeuganisha na suruali ili tatizo lolote likitokea nikianza kutimua mbio nisipate majeraha au kiatu kisitoke.

Ukiangalia sura zetu sio ma handsome tulikuwa tumetengeneza sura chafu za kukabiliana na kitu chochote mradi tutimize lengo la kupata pesa basi baada ya hapo tukatoka njee lakini siku hiyo upepo ulikuwa unapuliza sana utadhani kuna bahari maeneo ya hapo

Tukajisogeza hadi karibu na barabara halafu kila mmoja akachukua uelekeo wake basi mimi nikaanza kutembea lakini cha ajabu sikukutana na mtu yoyote hata pale tulipokuwa tunakaaa hatukuona mtu yoyote nilimaliza barabara nzima hadi nikamezwa na kichaka sikukutana na mtu wala boda

Nikawa najiuliza mbona leo watu hawaamki basi mimi sikujali nikaendelea kupiga tambo kwenye yale matuta ya majani nikielekea upande wa mwembe ulipo moyoni nilikuwa sina hofu sana nilikuwa najua lazima nitakuta mbegu zimeote yaani nilikuwa na asilimia mia.

Lile eneo ambalo ule muembe ulikuwepo haikuwa mbali sana ila nilijikuta nitembea sana bila kufika hadi nikaanza kuchoka kwa mbali nikaanza kuuona na ukumbuke hapo bado nilikuwa sijakutana hata na kifaranga cha kuku basi nikaongeza mwendo nikazidi kuukaribia ule muombe asee ile na ukaribia vizuri nilisikia kitu kama radi inapiga kwa nguvu halafu likatokea giza totoro hapo sikuwa nimebeba hata tochi

Nikasema sirudi nyuma lolote litakalo nitokea lazima niendee tu nikashuhudie siwezi poteza muda kiasi hiki alafu niishie kurudi tena nyuma basi nikazidi kuusogelea ule muembe kwa haraka zaidi huku nikiwa nimepanic kichwani kama dakika kadhaa nikawa nimefika chini ya ule muembe tatizo nilikuwa sijabeba tochi ikabidi nianze kutafuta lile jiwe nililokuwa nimeegesha maana pembeni yake ndio nilikuwa nimepnda zile mbegu

Basi nikaanza kulitafuta bila mafanikio tafutata sana silioni papasa sana majani yaliyokuwa pale chini hadi nikachoka ikabidi nikae nikaanza kujiuliza au mganga atakuwa amatuchezea changa la macho basi wakati naendelea kujiuliza nikahisi kama kunakitu kimenigusa bega niligeuka fasta kwa spidi ya 5G lakini sikuona mtu yoyote kwanyuma kabisa nikaliona lile jiwe kwa mbali kidogo

Ikabidi niliiendee fasta maana mimi nilikuwa upande mwingine wakati nimelizungukia ghafla tena naona liko upande mwingine basi nikasema wee jamaa usinitanie nalala na wewe mbele hivyo hivyo nikaanza kulizungukia kwa kasi bila mafaniko nilijikuta nimezunguka hadi nimechoka ikabidi nikae chini naishia kulitazama tu.

Akili ya haraka haraka akanijia nikasema hapa nikimbie hadi kule getto nichukuwe zile dawa za mganga ninywe, nioge halafu nichukue stiki ya bangi nivute pamoja na tochi labda inaweza nisaidia halafu nirudi tena kuhakikisha kama nachokiona ni kweli.

Basi nikatesti mara ya mwisho kwanza kulifikia kabla sijaondoka lakini hali ikawa bado iko vilevile, nasema ukweli toka moyoni kama sikuile siku changanyikiwa sewezi tena kuugua ukichaa maishani mwangu maana nilipanic kweli kweli .Kunajamaa hapo juu alicomment eti naeleza haya yote itakiwa bado na moshi wa bangi unanisumbua kichwani niseme tu leo hata mungu akaondoa vilevi vyote kuanzia cocaine hadi pombe za kienyeji bado tu watu waliochanganyikiwa wataendelea kuwepo

Oky tuendelee nilitoka pale nikiwa na nguvu za kutosha na kuanza mchaka mchaka hadi nikatika getto lakini kabla sijaingia nikamkuta yule mama mwenye nyumba amesimama mlangoni ameshikilia na mkono mmoja kwa jinsi nilivyokuwa nimechanganywa kichwani nikamsalimia nikaingia ndani ile nafungua mlango nikakimbia moja kwa moja kuwasha sola tulikuwa tunatumia zile zenye kichuma flani hivi zakuanika kwa njee wale wa vijijini watakuwa wanazifaamu vizuri.

Nikawasha ili nichukue zile dawa nikaoge nyingine ninywe basi ile nimewasha tu nikaona damu zimejaa chini ya sakafu wala sikujali nikachukua maji kwenye dumu la njano nikaweka kwenye kindoo changanya dawa fasta nikaenda kuoga kurudi nikaanza kuvaa nyingene dawa nikanywa halafu nikachukua bangi nikaanza kuvuta mule mule getto

Wakati naendelea kuvuta tena nikipiga pagu haraka haraka nikachukua kisimu changu tecno jeneza nikaangalai wakati nikakuta ni saa 9 usiku kama na madakika nikazidi kuchanganyikiwa nikavaa viatu haraka haraka nikachukua ile tochi ya sola nikaondoka tena kurudi kwenye ule muembe

Sasa ile natoka tu kuanza safari nikakutana na agustino ananiuliza vipi unaenda wapi nikamwabia bado sijaona zile mbegu na rudi kwa mara nyingine nilikuwa nimesahau tochi ndio akaniambia ulisahauje usiku wote ule nikamwabia usiku gani na tulitoka asubuhi daaa aliangua kicheko cha kufa mtu nikamuuliza wewe umeona mbegu zako zimeota daa akaniambia ndio asee hapo ndio nilizidi kuchanganyikiwa nilitoka na spidi ya kimbuga kuelekea kwenye ule muembe huku nikisika sauti ya kicheko cha agustino ikitokeza nyuma yangu

Sio kwamba alikuwa ananicheka kwa nia mbaya laahasha kulingana na situation iliyokuwepo kwa kweli kama ingekuwa ni kwenye nyumba za watu wengine wadadisi tungekuwa tumeshatimuliwa pale kwa sababu ya ushirikina

Wakati natimua riadha kuelekea kwenye ule muembe kidogo nilikuwa natumaini kuwa namimi nitakuta zimechomoza kulingana na maneno ya agustino niliendelea kukimbia huku hofu ikiendelea kunijaa moyoni....



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu asubuhi ndiyo hii fanya fanya basi
Hahaha..!
Wadau mtamtoa roho ndugu mwandishi walaqhi'.!
Nimewahi saa kumi na mbili hapa sioni kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Asubuhi sana c ndo hii

Sent using Jamii Forums mobile app
Shusha vitu mkuu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu asubuhi hii lete mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuuu tumeshafika tumepanga na foleni hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo hapo wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom