Baada ya ng'ombe 692 waliokamatwa kufa, Serikali yaamua kuwarudisha waliobaki kwa wamiliki

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
MPINA MIFUGO KIFO.jpg

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru ng'ombe waliobaki hai kati ya 692 waliokufa katika Pori la Akiba la Rukwa/Lwafi, waliokuwa wameshikiliwa warudishiwe kwa wamiliki wa mifugo hiyo.

Akiwa katika ziara yake Mh. Mpina amelazimika kutoa maamuzi hayo baada ya kukuta mizoga 692 ya ng’ombe ikiwa imetapakaa katika Pori hilo ambapo imedaiwa kwamba ng'ombe hao walikufa kwa kukosa mahitaji muhimu.

Waziri Mpina ameshangazwa kuona mizoga mingi kiasi hicho huku mifugo hai ikiishi zizi moja na iliyokufa, huku kukiwa na harufu mbaya

Imeelezwa kwamba mazingira hayo yamechangia kasi ya maambukizi ya magonjwa nyemelezi kuwa kubwa zaidi na kupelekea ongezeko la vifo kwa mifugo hiyo.

Hata hivyo baada ya kushudia Mizoga hiyo, Mh. Mpina amepokea taarifa ya Mkoa, Wahifadhi, Chama cha Wafugaji na wamiliki wa mifugo hiyo na kupitia nyaraka mbalimbali, ilibainika kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, ilitoa amri ya ng’ombe hao kukabidhiwa kwa wenyewe tangu Julai 27, mwaka jana.

Mifugo hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika hifadhi hiyo tangu mwezi machi mwaka jana

Chanzo: EATV
 
nadhani kuwe na utaratibu mzuri wa kudhibiti ng'ombe mipakani kabla hawajaingia nchini,pia kitu alichoongea rais juzi kuhusu kutaifisha ranch waliopewa wawekezaji ambao na wao wanawakodishia wakulima nakubaliana nacho,wafugaji wetu hamna haja ya kuvusha ng'ombe nchi jirani wakati tuna ranch hazitumiki ipasavyo
 
Vijana wengi wanaoajiriwa kwenye law enforcement agencies hua akili yao ya kufanya maamuzi sahihi ni ndogo, little learning, slow reasoning and decision making process.

Wengi hua ni losers, losers wengi hua hawatumii akili bali nguvu na mamlaka.

Ndio maana nchi zilizoendelea zimeanza kuweka masharti kuanza kuajiri hawa watu angalau mwenye college au university degree.

Nimeumia sana kuona ile hali jana kwenye taarifa ya habari. Wanyama wale wameteswa kiwango ambacho hakikubaliki.
 
Aiseee! Huu ni ukatili kwa wanyama, kwa nini lakini?????

Nataka kuona watu wakiwajibishwa kwa ukatili huu.
nahisi kuna watoa maamuzi waliohusika katika hili ni "brainless"
Mkuu kama damu yao inaendana na Mkulu wapo salama.
uwajibishwaji kwa sasa ni very Selective.
kuna watu wanasubiriwa wakiteleza kidogo tu wanatumbuliwa na kuna watu hata afanye utumbo gani ataachwa tu.[/
 
Wapo Watu wanakufa/wamekufa kwa sababu ya Njaa..Kwa kifupi tu Serikali isikwepe lawama hizi ,mmewatia Watu hasara na hata lengo lenu mlilo likusudia hamku litekeleza na mbaya kabisa mmewaua Wanyama hao bila ya sababu zozote za Msingi..
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru ng'ombe waliobaki hai kati ya 692 waliokufa katika Pori la Akiba la Rukwa/Lwafi, waliokuwa wameshikiliwa warudishiwe kwa wamiliki wa mifugo hiyo.

Akiwa katika ziara yake Mh. Mpina amelazimika kutoa maamuzi hayo baada ya kukuta mizoga 692 ya ng’ombe ikiwa imetapakaa katika Pori hilo ambapo imedaiwa kwamba ng'ombe hao walikufa kwa kukosa mahitaji muhimu.

Waziri Mpina ameshangazwa kuona mizoga mingi kiasi hicho huku mifugo hai ikiishi zizi moja na iliyokufa, huku kukiwa na harufu mbaya

Imeelezwa kwamba mazingira hayo yamechangia kasi ya maambukizi ya magonjwa nyemelezi kuwa kubwa zaidi na kupelekea ongezeko la vifo kwa mifugo hiyo.

Hata hivyo baada ya kushudia Mizoga hiyo, Mh. Mpina amepokea taarifa ya Mkoa, Wahifadhi, Chama cha Wafugaji na wamiliki wa mifugo hiyo na kupitia nyaraka mbalimbali, ilibainika kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, ilitoa amri ya ng’ombe hao kukabidhiwa kwa wenyewe tangu Julai 27, mwaka jana.

Mifugo hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika hifadhi hiyo tangu mwezi machi mwaka jana

Chanzo: EATV

Aisee kuna watu wana roho Mbaya,

SASA hao ng'ombe si bora wanagewarudishia wenyewe kama mahakama ilivyoamua,

Aisee CCM ni adui mkubwa wa maendeleo
 
Kuna siku Mungu atatupiga kwa janga la ukosefu wa mifugo na chakula ,,,yaani uho ni uzembe na roho mbaya iliyopitiliza ,,mmewapora watu mifugo yao,,,halafu mmeenda kuwafungia kwenye zizi lisilo na chakula wala maji *****,,,,,ng'ombe 692 ni zaidi ya tsh. Ngapi sijui imepotea hapo,,,,,zaidi ya tsh. MILIONI MIA MBILI HAPO imepotea
 
Fidia ihusike, na si walienda kinyume na maamuzi ya mahakama kuhusu hao mifugo kuachiwa, wakafungue shauri la kulipwa fidia, nadhani kesi ya fidia wameshinda mpaka hapo, wadai pesa nyingi ili hao wapuuzi wa maamuzi mabovu siku ingine watatumia akili.
 
Back
Top Bottom