Baada ya ng'ombe 692 waliokamatwa kufa, Serikali yaamua kuwarudisha waliobaki kwa wamiliki

Kwa ninavyofahamu utendaji mzuri wa huyu Waziri, inabidi apangue safu ya watumishi wake. Naamini kuna wengi ni mapandikizi na ambao wamewekwa kwa kujuana tu. Hawa watamwangusha sanaa. Haiwezekani ng'ombe wafe wengi kiasi hicho huku maafisa mifugo,madakitari wa Kanda hizo za Kusini wapo tuu wanaangalia hadi Waziri afike? Hapo,lazima wawepo wa kuwajibika.
 
Kwa nonavyofahamu utendaji mzuri wa huyu Waziri, inabidi apangue safu ya watumishi wake. Naamoni kuna wengi ni mapandikizi na ambao wamewekwa kwa kujuana tu. Hawa watamwangusha sanaa. Haiwezekani ng'ombe wafe wengi kiasi hicho huku maafisa mifugo,madakitari wa Kanda hizo za Kusini wapo tuu wanaangalia hadi Waziri afike? Hapo,lazima wawepo wa kuwajibika.
Na wale ndugu zetu wa Kimara mahakama ilivyotoa zuio na TANROADS wakagoma unahaur nini kwa Mbarawa
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru ng'ombe waliobaki hai kati ya 692 waliokufa katika Pori la Akiba la Rukwa/Lwafi, waliokuwa wameshikiliwa warudishiwe kwa wamiliki wa mifugo hiyo.

Akiwa katika ziara yake Mh. Mpina amelazimika kutoa maamuzi hayo baada ya kukuta mizoga 692 ya ng’ombe ikiwa imetapakaa katika Pori hilo ambapo imedaiwa kwamba ng'ombe hao walikufa kwa kukosa mahitaji muhimu.

Waziri Mpina ameshangazwa kuona mizoga mingi kiasi hicho huku mifugo hai ikiishi zizi moja na iliyokufa, huku kukiwa na harufu mbaya

Imeelezwa kwamba mazingira hayo yamechangia kasi ya maambukizi ya magonjwa nyemelezi kuwa kubwa zaidi na kupelekea ongezeko la vifo kwa mifugo hiyo.

Hata hivyo baada ya kushudia Mizoga hiyo, Mh. Mpina amepokea taarifa ya Mkoa, Wahifadhi, Chama cha Wafugaji na wamiliki wa mifugo hiyo na kupitia nyaraka mbalimbali, ilibainika kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, ilitoa amri ya ng’ombe hao kukabidhiwa kwa wenyewe tangu Julai 27, mwaka jana.

Mifugo hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika hifadhi hiyo tangu mwezi machi mwaka jana

Chanzo: EATV

Afadhari wamesaidiwa kupunguza mifugo
 
Na wale ndugu zetu wa Kimara mahakama ilivyotoa zuio na TANROADS wakagoma unahaur nini kwa Mbarawa
Awaweke sawa,japo ni two different scenarios. Hapa,ng'ombe wangeweza kupata huduma muafaka na wakaishi hata muda zaidi ya huo
 
Back
Top Bottom