Baada ya Nchimbi na Nahodha, Mwema, Mwamunyange na Othman Wanasubiri Nini?

Kwa Afisa Usalama Mkuu wa TISS ni ngumu, kwa wengineo...inawezekana kabisa.
 
Hivi kuna mtu hapa anaweza kutueleza ile sifa kuu za TISS, TPDF ziliko ishia? nini kimetokea hadi heshma ile kubwa iliyojengwa na kujengeka kuporomoka kiasi hiki?...Kwa uelewa wangu mambo ya TISS yalianza kwenda harijojo baada ya USA et al kufanya tathmini na kugundua kuwa kikwazo kikubwa kuliko kitakacho wakwaza kukwapua rasilimali zetu na hatimae tuwe wategemezi wa US ni TISS, Muundo wa TISS ulikuwa na nguvu kubwa sana! walikuwa wanafanya counter threat analysis za ukweli! Maadui wengine walikuwa wanapotezewa juu kwa juu... TISS iliimarishwa sana wakati ule wa mapambano na makaburu na pia wakati cold war btn USA n USSR... MKAPA one of EHM wa USA alipewa majukumu ya kuidhoofisha TISS vilivyo! mwaka 1996 ilitungwa sharia ya kuiondolea meno TISS, Kwa mara ya Kwanza TISS ilipewa kazi ya kupeleka umbea (Kushauri!). wote tunajua kuwa ushauri unaweza kupokelewa ama kuwekwa kwapuni kama inavyofanyka sasa hivi!!! katk kuondolea TISS meno kuna watu walikuwa wanaonekana radical na hawanunuliki, hawa walitengenezewa mizengwe (Rejea kisa cha mkewe kutibiwa nje ya nchi) na wengine walinyamazishwa kabisa (Imran Kombe)... Itoshe kusema TISS, Police, Magereza na TPDF wamechakachuliwa sana, hizi idara zinatakiwa zifanyiwe mageuzi makubwa ya kisasa yatayoendana na kukabiliana vilivyo na wakati tulionao... ona sasa tunateswa hadi na wauza sembe...Shame kwetu sote kwa kuendelea kuikumbatia chama cha majambazi kinachoendelea kuingamiza Taifa letu...
 
Back
Top Bottom