Baada ya Nchimbi na Mahodha, Mwema, Mwamunyange na Othman Wanasubiri Nini?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Wanabodi,

Mara baada ya kifo cha Mwangosi nilipandisha uzi huu humu jf
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? kwenye hitimisho langu nilisema h
" Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.

Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!".
Mwisho wa kunukuu!
Hiki kilichotokea sasa kwa mawaziri kuwajibika ni utekelezaji tuu wa "karma" na kilichotokea juzi kwenye oparation tokomeza sio kipya nchini mwetu, wale wenye kumbukumbu, mwaka 1976, kulitokea operation kama hiyo Mkoani Mwanza na Shinyanga hali ilikuwa kama ifuatavyo.

Kulitokea mauaji ya vikomgwe huko Mwanza na Shinyanga kwa tuhuma za ushirikina. Watuhumiwa wawili, walifariki mkoani Mwanza. Mwaka huo 76 mimi nilikuwa nasoma darasa la kwanza pale Nyakahoja!.

Watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Kahula Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, walipoteza maisha kwenye mahojiano. Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu, Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa nae aliwajibika!, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Wakati huo, Peter Kisumo ndiye alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye pia aliwajibika!. Watekelezaji ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RSO wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya! walishitakiwa katika ile kesi maarufu ya Mauaji Mwanza.

Wakuu hao watatu wa polisi walikuwa wakiishi nyumba tatu zilizofuatana zikiwa pale Isamilo ya chini ikianza ya Ihuya, ikafuatia ya Andew M na ya mwisho ni ya Mkwawa!. Nyumba ya nne ilikuwa ni Daktari Mkuu wa Mkoa, Dr. Dahoma ambaye yeye alihusishwa kutoa post morterm report fake, ili aligeuzwa PW, hivyo kutoshitakiwa. Just imagine hali ilikuwaje mtaani wakati vigogo wanne wanene wa serikali wanaokaa mtaa wote wanashitakiwa kwa kosa la mauaji!.

Kesi iliendeshwa, aliyekutwa na hatia alihukumiwa, Mshtakiwa mmoja Andrew M, hakukutwa na hatia. aliachiwa huru, ila wakuu wote waliwajibishwa!.

Hiki kilichotokea kwenye operation tokomeza, hakina tofauti na operation ile, Kama waziri wa Mambo ya Ndani amejiuzulu, IGP Saidi Mwema anasubiri nini?!. Kama Waziri wa Ulinzi Amejiuzilu, CDF Mwamunyange anasubiri nini?!. Waziri wa TISS na Mkurugenzi Mkuu wa Tiss nao wanasubiri nini?. Tunasubiri kuona wahusika wakipandishwa mahakamani kama ile ya 1976!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,895
2,000
Kweli kabisa Mwamunyange ,Othmani,wajipime wenyewe kama wanastahili kuwepo pale!na muda wao ulishaisha!
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,858
2,000
Mkuu,hata mimi leo niliweka bandiko kama hilo nikihoji ni kwanini hao wote uliiwataja nao wasiwajibike.

Hata hivyo chini ya utawala huu wa JK hii ni kama ndoto!

Kosa la wabunge lilikuwa kuwakomalia mawaziri tu bila hao wengine na bahati mbaya JK hawezi chukua hatua bila shinikizo.

Kwa maneno mengine,maadamu wabunge hawakupiga sana kelele kuhusu hao vigogo basi nae atapotezea tu!

Nchi hii ni kama hatuna Raisi mtendaji!
 
ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,961
1,225
Idara ya Usalama wa Taifa haikamati, haishtaki ! - Mkuchika:

BUNGE limeelezwa majukumu ya Idara ya Usalama wa Taifa kwa kuambiwa kwamba haihusiki kukamata wala kushitaki mtu yeyote.

Ufafanuzi huo ulitolewa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kufahamu msaada unaotolewa na Idara ya Usalama wa Taifa kuhakikisha rasilimali za taifa hazimilikiwi kifisadi na wachache ili taifa liwe salama kwa vizazi vijavyo.

Katika swali la nyongeza, mbunge huyo alitaka kufahamu ni hatua gani zimechukuliwa kwa baadhi ya watendaji waliopuuzia taarifa za idara hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuhusu utoroshwaji wa nyara za taifa na matokeo yake, zikapelekwa nje ya nchi.

Mbunge huyo alisema watumishi wa idara hiyo wako katika Uwanja wa KIA na kwa taarifa alizo azo ni kwamba walitoa ushauri kwa Serikali dhidi ndege ya Qatar iliyotua katika uwanja huo Novemba 22, 2010 na kuondoka Novemba 25 mwaka huo ikiwa na wanyama.

"Kwa kuwa Serikali ilipuuzia taarifa za Usalama wa Taifa, ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya watendaji wa Serikali. Kama hatua hazijachukuliwa Serikali inashauri wananchi wachukue hatua gani dhidi ya Serikali," alihoji Nyerere.

"Idara ya Usalama wa Taifa haimkamati mtu haimshitaki mtu, kazi yake ni kukusanya habari na kushauri, na inapokuwa imeshauri na kama mtu hakufuata ushauri, mamlaka iliyoko juu yake ndiyo inapaswa kumchukulia hatua…usalama kazi yake ni kutoa ushauri," alisema Mkuchika.

Kwa upande wake, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) alitaka kufahamu hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa idara hiyo wanaotuhumiwa na wanasiasa na vyombo vya habari na kusababisha chombo hicho kisiaminiwe na wananchi.

Aidha, Selasini alitaka kufahamu kama tuhuma zinazotolewa dhidi ya idara hiyo si za kweli, ni wanasiasa au vyombo vya habari vipi vinavyoituhumu, vimeshakamatwa.

Mkuchika alisema wapo wanasiasa ambao wamekuwa wakiituhumu idara kwa kutafuta umaarufu na wengine kwa kutafuta visingizio kutokana na madai au mashitaka yanayowakabili.

Alisema baada ya kauli hizo kutolewa dhidi ya chombo hicho, Serikali imekuwa ikitoa maelezo kukanusha tuhuma husika.

Awali katika majibu kwa swali la msingi, Mkuchika alisema majukumu ya idara hiyo yameainishwa katika kifungu cha 5 cha Sheria Na. 15 ya mwaka 1996 ya kuundwa kwake.

Majukumu hayo ni kukusanya taarifa za kiusalama, kuzifanyia uchunguzi na kuishauri Serikali kwa malengo ya kuchukua hatua zinazostahili.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na zinazohusu vitendo vya hujuma dhidi ya uchumi na rasilimali za taifa kama vile kumilikiwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi. Hatua hiyo imetajwa kwamba huchukuliwa kuhakikisha rasilimali zilizopo zinanufaisha taifa sasa na baadaye.

"Hivyo basi, Idara ya Usalama wa Taifa imekuwa ikitekeleza majukumu hayo kwa weledi na umakini mkubwa ili kuhakikisha taifa linaendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu," alisema Mkuchika.
 
Makaro

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
615
195
Pasco,
Pamoja na hao viongozi uliowataja nilitegemea Baada ya ile report PM angejiuzulu Mara moja. Tz ni nchi ya ajabu mno.
Kuhusu IGP, CDF na mkuu wa TISS wao wanatakiwa kujipima kwani ndiyo washauri wakuu wa Ulinzi na Usalama kwa Amri Jeshi Mkuu wa Nchi.

Kwenye report ya tume, CDF alitajwa moja kwa moja kuwa kila Siku alikuwa anapata habari. Kwenye ile operation kila idara iliwakilishwa ipasavyo.
 
Daddo

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,409
2,000
Kelele lazima tupige sana juu ya hili ila kiuhalisia kama tungetaka yasitokee haya tungeanza na kuzuia tatizo kwa kushauri operation ile ifanyike kiraia. Kitendo cha kuingiza jeshi na kuifanya operation kijeshi ni wazi kwamba lazima torture ilikuwa haiepukiki. Wanajeshi wamejikita katika swala zima la mafunzo ya kivita. Si rahisi kumwambia mtu atoe siraha akaitoa kama hajabanwa kikwelikweli.

Mbali zaidi wananchi wengi hawana imani na vyombo vya usalama tulivyonavyo hivyo wengi walikuwa wakiona hao wayu wa misako wanakuja wanachukua jukumu la kukimbia kujificha hata kama hawana kosa na kitendo cha kukimbia ni kiashiria cha uhalifu kwa hawa wenzetu yaani wanajeshi hivyo si ajabu mtu ukalambwa risasi bila kosa lolote.

Nasema tena wakuu wetu walikurupuka kwenye mchanganuo wa nani ahusishwe kwenye operation na nani asihusishwe.
Sidhani pia kama hii operation ilichukua muda kufikiriwa faida na hasara zake pia njia bora za kupunguza hasara.

Kimsingi ilitakiwa zitungwe sheria za kufuatwa wakati wa msako na zisimamiwe vilivyo sasa sidhani kama hicho kitu kilifanyika na kama sheria zilikuwepo basi usimamizi ulikuwa hafifu sana.
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,270
2,000
wabunge ndio wanafiki kwani wanakazania mawaziri kujiuzulu ili nao wapate uwaziri kama kweli walikuwa na uchungu wasingeishia kwa mawaziri watendaji wengine wote wakiwamo hao uliowataja walitakiwa wawajibike
 
funza

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
7,475
2,000
Tokea kipindi kile Walipoanza Akina Mwinyi kujipima na kuachia ngazi wenyewe Hali imekuwa ikiendelea hivyo hivyo kwa wanasiasa kwani siku zote wa kuwajibika hapa Tz ni mwanasiasa tu wengine hudai wanapokea Amri toka kwa Mawaziri japo vyeo vyao vina nguvu kuliko wana siasa hivyo ni vigumu upepo wa akina Nchimbi kuwafikia
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,275
2,000
Mwema ni shemeji wa JK hawezi kujiuzulu,nyingi ya nafasi hizo ni investment ya rais,kupata replacement atakayeweza kuendelezea pale alipoacha mwingine ni shida.Si unaona hata EL ilibidi mbinde hadi kuondoka?Na baada ya hapo mambo yao mengi yameyumba.

BTW nasikia Mrema alikuwa afisa usalama wa taifa wilayani maeneo hayo,wengine wakisema alishiriki kwenye mahojiano yale.

Je TISS wana mkono kwenye mahojiano haya?
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Mwema ni shemeji wa JK hawezi kujiuzulu,nyingi ya nafasi hizo ni investment ya rais,kupata replacement atakayeweza kuendelezea pale alipoacha mwingine ni shida.Si unaona hata EL ilibidi mbinde hadi kuondoka?Na baada ya hapo mambo yao mengi yameyumba.

BTW nasikia Mrema alikuwa afisa usalama wa taifa wilayani maeneo hayo,wengine wakisema alishiriki kwenye mahojiano yale.

Je TISS wana mkono kwenye mahojiano haya?
Kama Mrema alikuwa ofisa usalama na alishiriki, then alikuwa ni bwana mdogo akitekeleza amri halali za mabosi wake. Walioshitakiwa ni watoa amri, RPC, RSO, OCD na DSO. Hao wengine ni watekelezaji tuu wa amri halali na sio makosa yao!. Ukiondoa operetion za kijeshi, yaani combat oparation za kivita, ambayo jeshi linahusiuka lenyewe, operation nyingine yoyote inayohusu usalama wa ndani, TISS inahusika!.

Mfano aliyemlipua Mwangosi, kama alipewa amri halali, yeye hana kosa, anayepaswa kusimama kizimbani ni RPC wake alietoa amri!. Ila wanachofanya ili kujenga public sympathy, wataendesha kesi na yule askari atahukumiwa kifungo kirefu, then anaingizwa gerezani mwezi, miezi miwili na kuachiwa kimya kimya kama wale vijana wa Kombe!.
Pasco
 
engmtolera

Verified Member
Oct 21, 2010
5,150
1,250
Wanabodi,

Mara baada ya kifo cha Mwangosi nilipandisha uzi huu humu jf
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? kwenye hitimisho langu nilisema h
" Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.

Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!".
Mwisho wa kunukuu!
Hiki kilichotokea sasa kwa mawaziri kuwajibika ni utekelezaji tuu wa "karma" na kilichotokea juzi kwenye oparation tokomeza sio kipya nchini mwetu, wale wenye kumbukumbu, mwaka 1976, kulitokea operation kama hiyo Mkoani Mwanza na Shinyanga hali ilikuwa kama ifuatavyo.

Kulitokea mauaji ya vikomgwe huko Mwanza na Shinyanga kwa tuhuma za ushirikina. Watuhumiwa wawili, walifariki mkoani Mwanza. Mwaka huo 76 mimi nilikuwa nasoma darasa la kwanza pale Nyakahoja!.

Watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Kahula Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, walipoteza maisha kwenye mahojiano. Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu, Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa nae aliwajibika!, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Wakati huo, Peter Kisumo ndiye alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye pia aliwajibika!. Watekelezaji ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RSO wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya! walishitakiwa katika ile kesi maarufu ya Mauaji Mwanza.

Wakuu hao watatu wa polisi walikuwa wakiishi nyumba tatu zilizofuatana zikiwa pale Isamilo ya chini ikianza ya Ihuya, ikafuatia ya Andew M na ya mwisho ni ya Mkwawa!. Nyumba ya nne ilikuwa ni Daktari Mkuu wa Mkoa, Dr. Dahoma ambaye yeye alihusishwa kutoa post morterm report fake, ili aligeuzwa PW, hivyo kutoshitakiwa. Just imagine hali ilikuwaje mtaani wakati vigogo wanne wanene wa serikali wanaokaa mtaa wote wanashitakiwa kwa kosa la mauaji!.

Kesi iliendeshwa, aliyekutwa na hatia alihukumiwa, Mshtakiwa mmoja Andrew M, hakukutwa na hatia. aliachiwa huru, ila wakuu wote waliwajibishwa!.

Hiki kilichotokea kwenye operation tokomeza, hakina tofauti na operation ile, Kama waziri wa Mambo ya Ndani amejiuzulu, IGP Saidi Mwema anasubiri nini?!. Kama Waziri wa Ulinzi Amejiuzilu, CDF Mwamunyange anasubiri nini?!. Waziri wa TISS na Mkurugenzi Mkuu wa Tiss nao wanasubiri nini?. Tunasubiri kuona wahusika wakipandishwa mahakamani kama ile ya 1976!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.

na kwakuwa nao wamekili kuwa kulikuwa na tatizo,ni vyema wakapima na kufanya maamuzi kwa maslahi mapana ya Taifa letu
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,791
2,000
Wanabodi,

Mara baada ya kifo cha Mwangosi nilipandisha uzi huu humu jf
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? kwenye hitimisho langu nilisema h
" Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.

Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!".
Mwisho wa kunukuu!

Hiki kilichotokea kwenye operation tokomeza, hakina tofauti na operation ile, Kama waziri wa Mambo ya Ndani amejiuzulu, IGP Saidi Mwema anasubiri nini?!. Kama Waziri wa Ulinzi Amejiuzilu, CDF Mwamunyange anasubiri nini?!. Waziri wa TISS na Mkurugenzi Mkuu wa Tiss nao wanasubiri nini?. Tunasubiri kuona wahusika wakipandishwa mahakamani kama ile ya 1976!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.
....kwavile rais wangu alikuwa bado hajazaliwa "maamuzi' haya hayafahamu na hawezi kuyachukua....

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Hawa ni watu muhimu na wana nguvu sana, wakijiudhuruau au kuwajibishwa nchi itayumba-Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Rais na Waziri Mkuu wanafanya kazi kwa style ya 'mimi simo' inayochagizwa na kauli mbiu ya 'Huu ni upepo na utapita'. Kutokana na style hii, usitegemee hawa watu wataachia madaraka hasa ikichukuliwa kuwa, ubinafsi kwa sasa nchini ni fashion.

Wananchi wenyewe hawana msukumo kutaka jambo hili litokee. Unategemea wao ndiyo wataguswa kimsukumo. Never!
 
KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,182
2,000
Mwambieni Nape anaweza si anawaita mawaziri mizigo je hao wakuu waidala za usalama nchini wao ni mizigo au la?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom