johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,872
Kiukweli kabla Rais Magufuli hajafanya ziara mikoa ya Lindi na Mtwara nilimuona mbunge wa Ndanda mh Cecil Mwambe kama kamanda anayeweza kumrithi mkongwe wa siasa za upinzani mh Mbowe.
Lakini baada ya Mwambe kuhojiwa na Rais Magufuli na kukiri kuwa alikuja Chadema kwa bahati mbaya baada ya kura zake kule CCM kwenye maoni kupewa mtu mwingine na yeye kupigwa chini, nimegundua Cecil kimwili yuko Chadema lakini kiroho yuko CCM hivyo hatatosha.
Hivyo basi wanaoniunga mkono naomba kwa pamoja tumchukulie fomu kamanda mwingine shupavu mwenye ujasiri uliotukuka ndugu yetu Tundu Antipas Lisu.
Sijajua fomu inauzwa bei gani lakini ninajitoa kwa gharama yoyote ili tupate kiongozi sahihi wa kumrithi kamanda Freeman.
Naomba kuwasilisha
Maendeleo hayana vyama!