Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Alipopokoea kijiti cha kuiongoza nchi, Tanzania ilikuwa imefilisika. Serikali imeganda , umasikini ulikithiri ,njaa iliuofurutu ada, watoto kwenda shule nusu uchi, ili mradi Tanzania ilikuwa imetoteshwa. Comrade Mugabe ndio alieinusuru nchi isiaangamie kabisa kwa kutoa ruzuku alau nchi ipate kuchechemea.
Historia leo imekuja kupotoshwa kwa kumpaka rangi angafu yule alieididimiza nchi na kurembwa rangi ya giza wale walioinurisha nchi!
Rais Mwinyi alianza kufungua milango ya demokrasia. Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, kukosoa na kukosolewa, yote yaliruhusiwa. Gazeti moja lilivutiwa na hatua za kijasiri alioanza kuzichukua na hakusita kulipa kipaumbele kwenye ukurasa wa mbele tena kwa harufu nene, kumtangaza Rais Mwinyi kuwa ni "Mr Clean"
Hili halikuwafurahisha washika hatamu na siku hiyo hiyo, gazeti hilo lilipigwa marufuku na nakala zote kukusanywa mitaani.Kikundi kilichopewa baraka cha kumtukana Rais Mwinyi kilichojuulikana kama "Punch" ya Chuo kikuu cha Dares salaam, kilianza kumtusi kila ya aina ya tusi kuanzia la nyumbani mpaka kumalizikia nguoni. Rais Mwinyi aliendelea kuwa mvumilivu na mstahamilivu na pale aliofunua kinywa chake aliwajibu kwa hekima na kuwa ambia " yote hayo nyie wenyewe!" akinukuu hadithi maarufu ya " mashindano ya matusi baina ya Mhindi na Mswahili"
Yote hayo katika utawala wake hawakumkamata mtu au watu kuwatisha, kuwafunga au kuwambambakizia kesi.
Zawadi yake alietunukiwa na muumba wa viumbe vyote ni kumzidishiwa na kumbarikia umri mrefu ,afya njema ilyoneemeka, marafiki wema waliomzunguka na kubwa kuliko yote HESHIMA ILIOTUKUKA
Mzee Ruksa amekuwa kipenzi wa vizazi vyote, si mtoto,si kijana,si mzee,si mume si mke. Kama alau tungejaribu kuuishi rai ya utawala wake Tanzania ingekwa mbali, kama vile Zanzibar ya Baraghash.