Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,398
- 2,990
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na marekebisho yake yote, baada ya mhula huu mfupi wa urais wake wa kurithi kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 37(5), Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kuchaguliwa tena kwa mhula mwingine mmoja. Ibara ya 40(4) ambayo ndiyo inahusika inasema hivi:
Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Obviously, kulikuwa na sloppiness katika uandishi wa Ibara ya 40(4). Limit ni ya kuchaguliwa sio kugombea. Kama hujachguliwa unaweza kugombea hata mara tano kama alivyofanya Hayati Maalim Seif kule Zanzibar. Ukiisoma ibara hii sanjari na ibara ya 40(1), utabaini kwamba walichokusudia kuweka katika ibara ya 40(4) ni ukomo wa kuchaguliwa na sio ukomo wa kugombea kama waandishi wa Katiba walivyoandika!
Kwa kuwa mhula huu mfupi unazidi miaka mitatu, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kugombea na kuchaguliwa tena kushika kiti hicho mara moja tu, baada ya mhula huu.
Tofauti na ilivyozoeleka, kwa uchaguzi wa 2025, Lissu na wafuasi wake (na Kambi ya Upinzani kwa ujumla) wajiandae kukimbizwa mchakamchaka na mwanamama (iwapo ataamua kugombea).