Baada ya mkutano wa COP 26, wa mabadiliko ya tabia ya nchi, Tanzania ianzishe sera mpya za kupambana na mabadiliko tabia ya nchi

Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
701
1,000
Baada ya mkutano wa Paris wa 2015, nchini Ufaransa, nchi zilizoendelea zilikubaliana kutoa msaada wa fedha na teknolojia ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye nchi zinazoendelea. Kwenye mkutano wa mwaka huu unaofanyika Scotland tumesikia nchi za Africa zikiomba msaada wa kifedha ili kupambana na mabadiliko hayo.

Mabadiliko ya tabia ya nchi yana athiri moja kwa moja maendeleo ya nchi katika nyanja zote kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mabadiliko haya uleta athari kama vile kuongezeka kwa kina cha bahari, mafuriko , ukame n.k ambayo usababishwa na shughuli za binadamu, uzalishaji wa gesi ya ukaa kutoka viwandani, vyombo vya usafiri vinavyotumia mafuta, matumizi ya makaa ya mawe n.k ambayo usababisha joto kupanda na kuchangia hizo athari.

Kiujumla nchi zilizoendelea ndiyo mchangiaji mkubwa wa mabadiliko haya kutokana na shughuli nyingi za viwanda na teknolojia ambazo uchangia katika mabadiliko haya. China inachangia zaidi ya 30%, Marekani, Japan, Asia na Urusi pia zikichangia kwa kiasi kikubwa ndiyo maana zinawajibika kutoa misaada ya kukabiliana na athari za mabadiliko haya katika nchi zinazoendelea ambazo uchangia kwa wastani mdogo uzalishaji wa gesi ya ukaa.

Tanzania Kama taifa linaloendelea, lazima libuni sera mbadala na thabiti za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, serikali isiishie tu kwenye kuomba msaada wa fedha.

Wizara ya muungano na mazingira chini ya serikali inayo wajibu wa kuja na sera mbadala za kukabiliana na athari hizi kwani athari hizi zinaathiri moja kwa moja uchumi wa nchi kutokana na kukwamisha shughuli za uzalishaji Kwa wanachi. Ni wakati muafaka sasa wa serikali kuweka nguvu zaidi katika kukabiliana na mabadiliko haya.

Nimemsikia waziri mwenye dhamana akisema Tanzania inakabiliana na mabadiliko haya kwa kupanda miti, kutunza misutu na kujenga bwawa la umeme na SGR , pamaoja na jitahidi hizo bado serikali ni lazima ije na mipango na sera madhubuti ya kupambana na mabadiliko haya isiishie tu kwenye kuomba misaada, kwani kwa sasa tunashuhudia mvua zisizo tarajiwa, ongezeko la joto Kali kwenye miji (mfano Dar es salaam), mafuriko, ukame na kuongezeka kwa kina cha maji kwenye maziwa kama Tanganyika, Victoria na bahari ya hindi ambayo yanatishia ustawi wa uchumi na maendeleo kwa ujumla nchini.

Katika kubuni sera hizo, serikali pia iwashirikishe mashirika, wadau na wataalamu wa mabadiliko ya tabia ya nchi katika kupambana na mabadiliko haya, pia iiwezeshe mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), kufanya tafiti zaidi na zenye tija kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko haya.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,217
2,000
QeM-d.jpg
 
Hapa wangeweza kutabiri hiki kinachoendelea sasa hivi kuhusu maji, huenda watu wangechukua tahadhari.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom