ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Baada ya majuzi Azam kupata haki ya kuonyesha VPL kwa mkataba wa miaka kumi walitamka na kiasi kitakacholipwa klabu zote shiriki
Kilichokuja nistua na kuniuma nilipokuja sikia kipindi cha michezo jioni hiyo cha wasafi fm wakitangaza habari ya mechi iliyochezwa huko unguja wikiendi ambapo mwisho wa mechi hiyo kila timu ilipata mgao wa Tsh 1,500/-. Kwa kwel hii kitu imeniumiza sana
Binafsi naelewa kuwa Zanzibar imejaaliwa vipaji hususan soka,najiuliza tatizo ni nini?
Kwanini Zanzibar tunashindwa kuitumia katika jamhuri ili tuwe na kikosi kizuri Taifa stars? Kwanini Isisaidiwe kama kuna changamoto zinazoifanya ibaki nyuma? Mbona zamani ilikua na tinu nzuri na zikaleta changamoto hadi huku bara?ninakumbuka enzi za KMKM,Small Simba nk...nini kilipelekea zikapotea?
Azam amemwaga pesa kwa klabu hizi za bara vipi Znz?basi hakuna jitihada zozote kati ya Azam/TFF/ZFF kuweka mambo sawa?
Tusiwaache ndugu zetu wazanzibar katika kukuza thamani na ubora wa soka letu.itasikitisha sana ikiwa tutaendelea kuishi hivi kama Jamhuri ya muungano.
Tusiiache Zanzibar.