Majighu2015
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,936
- 3,958
Dar es Salaam. Miaka tisa tangu Kitengo cha Tiba ya Mifupa, Upasuji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) kilichopo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kukumbwa na kashfa ya kuchanganya mafaili ya wagonjwa, jana kimeanza kutumia mfumo wa kidigitali kwa kuingiza taarifa za wagonjwa katika mfumo wa kompyuta.
Mwaka 2007, kitengo hicho kilimfanyia upasuaji wa kichwa mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu.
Pia, kilimfanyia upasuaji wa mguu mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa kutokana na kutumia mfumo wa analojia.
Hali katika kitengo hicho jana ilikuwa tete baada ya wagonjwa kupanga mstari mrefu wakati wa kuanza kwa huduma hiyo inayojulikana kwa jina la ‘MediPro’ liliyoanza kuratibiwa na hospitali hiyo ili kutoa huduma sahihi kwa wagonjwa.
Meneja Tehama wa MOI, Haggai Mwakasendo alisema mfumo wa MediPro utamwezesha daktari kuwasiliana na mgonjwa kwa njia rahisi na kuokoa muda.
Alisema mfumo huo uliofadhiliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni wa majaribio kwa hospitali nne nchini, kikiwamo kitengo hicho.
My take: Kama MOI miaka yote hiyo hawatumii mfumo wa computer,huko nachingwea huu mfumo utafika lini?