Baada ya miaka hamsini, tutampata tena Mwalimu Julius Nyerere, Edward Moringe Sokoine na Daktari John Pombe Magufuli

BAADA YA MIAKA HAMSINI;TUTAMPATA TENA MWALIMU JULIUS NYERERE,EDWARD MORINGE SOKOINE NA DAKTARI JOHN POMBE MAGUFULI.

Leo 18:00hrs 03/10/2021

Ni nadra sana kupata viongozi wanaoibadili dunia kutokana na falsafa zao na misimamo yao,katika kada mbalimbali ikiwemo siasa, biashara,taaluma,dini na hata wanaharakati. Rais wa kwanza wa Marekani George Washington anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa wa kuiletea uhuru Marekani pia anatajwa kuwa katika list ya viongozi 10 wenye IQ ya 140.Abraham Lincolin anafuatia kuwa mmoja kati ya Marais waliowahi kupendwa sana Marekani na amekuwa mdau mkubwa sana wa Demokrasia,pia anatajwa kuwa na IQ ya 150.Barani Afrika tunao baadhi ya viongozi kwenye list ya viongozi wenye IQ kubwa kati ya 180 hadi 150,Dr Namdi Azikiwe,Dr Kwame Nkrumah,Tanzania tunao Mwalimu Julius Nyerere,Edward Moringe Sokoine,Hayati Benjamin Mkapa na Daktari John Pombe Magufuli,wengine nitawazungumzia siku nyingine,

Wapo pia wanaharakati ambao waliingia kwenye list ya watu wenye IQ kubwa kati ya 180 hadi 150 baada ya harakati zao kubeba uwezo mkubwa,mfano miaka ya nyuma 1960s huko Marekani ubaguzi ulidhamiriwa kufikia kikoko,Ukomo ulikazaniwa hasa katika nyanja za msingi katika maisha ya mtu mweusi nchini Marekani na hapa waliibuka na kuibuliwa waafrka weusi wenye mawazo ya hali za juu miongoni ni Alhaj Malik Al Shabaash maarufu kama 'Malcolm X' na Martin Luther King,Awa walikuwa mahiri kwa kujibu maswali ya waandishi wa habari wazungu, kutoa hotuba za hamasa ya kujitambua kwa mtu mweusi 'Negro' na kutambuliwa kwa haki zao,Martin Luther King aliendesha harakati zake kwa diplomasia ya amani,lakini Malcom X alidhamiria kuishitaki Serikali ya Marekani umoja wa mataifa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa watu weusi.

List ya IQ kubwa pia iliendelea kuwajumuisha wapigania Uhuru wa Mtu mweusi duniani pote,The Pan Africanist,Martin Delany,Alexander Crummel,Edward Blyden,William Sylvester,Dr William Du Bois,Dr Namdi Azikiwe,Marcus Garvey,Kwame Nkrumah,Haile Selassie,Robert Mugabe,Jomo Kenyatta,George Padmore, Julius Nyerere,Kenneth Kaunda,Dedan Kimath,Ngugi Wathiongo, Nelson Mandela,Oliver Tambo,Thomas Sankara,Patrice Lumumba and Dr John Pombe Magufuli.Mzungu alitaka kuleta propaganda kwa kudai mwafrika hawezi kuwa na IQ kubwa,Walifanikiwa kwa Bob Marley hadi kumtenganisha na baadhi ya weusi walioshika misimamo mikali kwa hila tofauti tofauti ili tu ionekane huyu mwenye damu ya mweupe ndio bora na hakuna mwingine anayeweza kuwa bora bila kuwa na uzungu ndani yake. Mf. Peter Tosh alivyotenganishwa na Bob Marley na kupotezwa kwenye anga za ukombozi hadi kukaribia kusahaulika kabisa mbali na tungo zake kutumika 'The Wailers'

-Faida ya IQ kubwa kwa Tanzania,iliyoletwa na Rais Daktari John Pombe Magufuli.

1.Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha SGR kuunganisha Tanzania na nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC umekamilika.Kama ujenzi huo ungekamilika maana yake ni kwamba hakuna Lori litakaloruhusiwa kubeba mizigo inyozidi tani10 kuelekea nchi hizo.

2.By Cash, Serikali ingenunua mabehewa ya mizigo 300, ya Abiria 100 na vichwa vya Treli ya Umeme 20. Manunuzi hayo yamefanyika kwa Cash baada ya Serikali kukusanya fedha za kutosha kupitia vyanzo vya ndani na sio tozo.

3. Bandari ya Dar es Salaam ingekuwa nyeupe kabisa baada ya Ujenzi wa Bandari kavu ya Mlandizi kukamilika.Tungesikia habari kwa sasa wastani wa meli kusubiri bandarini ni masaa 24.

4. Ujenzi wa Bandari ya Mtwara ungepunguza msongamano wa misigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam.Kwa sasa, mizigo ya nchi za Malawi, Zambia na hata Msumbiji inashushwa na kupakiwa Bandari ya Mtwara

5. Wakala wa Umeme vijijini, REA ungefikia tamati baada ya kuunganisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na hivyo kuwa nchi ya kwanza kusambaza umeme vijijini Barani Afrika.

6. Miradi yote ya Maji kwenye vijiji vyote Tanzania Bara na Visiwani imekamilika. Hivyo, wastani wa umbali wa kutafuta maji umefikia mita 10.

7.Dodoma ingekuwa kama Cairo, California,ama New York baada ya kukamilika kwa ujenzi wake kama mji Mkuu wa Tanzania.

8. Serikali kupitia Shirika la Ndege nchini, ATCL imefanikiwa kununua ndege nyingine za kisasa 20 na hivyo kuwa shirika la kwanza la Ndege Afrika kuwa na ndege nyingi zinazoenda karibu nchi zote duniani.

9. Kwa mara ya kwanza vyama vya upinzani vimeshindwa kupata wabunge wengi Bungeni baada ya chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kuambulia mbunge 1 tu. vyama vingine havijapata kiti hata kimoja.

10. Kwa mara ya kwanza Serikali kupitia TPDC wamefanikiwa kufikisha mabomba ya gesi kwenye mikoa yote ya Tanzania. Pia mabomba hayo yamefika nchi jirani za Rwanda, Kenya, Uganda, Msumbiji, Malawi, DRC na Zambia. Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa Gesi Asilia Duniani.

11. Kasi ya ujenzi wa viwanda imeongezeka ambapo kwa sasa ni asilimia 5 tu ya bidhaa zinazohitajika nchini zinaagizwa China,Tanzania sasa ni nchi ya kwanza Barani Afrika kwa kuwa na viwanda vingi na imealikwa kujiunga na nchi za G 7.

12. Sera ya Elimu Bila Malipo imepanuka na sasa wanafunzi wanasoma bila malipo hadi ngazi ya Chuo kikuu,PhD.

13. Huduma ya Afya imeboreshwa nchini na sasa kila kijiji na Mtaa una Kituo cha Afya chenye miundo mbinu yote,hata kufanya operation ya moyo,kuna madaktari bingwa na madawa ya kutosha.

14. Kasi ya ukuaji uchumi imeongezeka kutoka asilimia 7 mwaka 2016 hadi asilimia 30 mwaka 2024.

15.Bwawa la Umeme la Rufiji lavunja rekodi ya kuzalisha Umeme duniani.

-Ushauri Wangu kwa Chadema.

CHADEMA mkimwomba msamaha Magufuli na kuamua kufuata sera na maono yake, 2025 mnachukua nchi kilaini sana".

Nimeyasema haya kwasababu alitaka mjenge naye uchumi lakini mlianza usumbufu. Mkaanza kumsumbua, aliteua hadi watu kutoka chama chenu lakini bado mliendelea kuwa wasumbufu.

Hamkupenda kushirikiana naye ni kwasababu hamkumkubali. Sasa wakati wa kumkubali ndio huu, kuomba msamaha na kufuata sera na nyayo zake. Na sababu za kutomkubali na usumbufu wote mlioanza kumletea chanzo chake ilikua ni sanduku la kula. Hamkuamini ushindi wake 2015.

Basi hamna budi kujitakasa na kumkubali sasa, 2025 ndipo mtaweza kushinda.Nimesema haya kwasababu watanzania kuna kitu wanakiamini. Hicho ndicho mwatakiwa kukifuata.

Mkifanya hivyo hamtahitaji hata kupiga kampeni wala kuitisha mikutano na wananchi au waandishi wa habari. Mtajikuta mnakubalika tu,mkifanya mioyo yenu kuwa migumu basi kile Chama kikichotabiriwa Chama Cha Hapa Kazi Tu kitachukua nafasi yenu na kuvunja rekodi.

-Nukuu ya Rais Daktari John Pombe Magufuli.

Magufuli alimtaja kiongozi wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye pia ndiye aliyeleta uhuru wa Tanzania na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kijamaa, Rais John Pombe Magufuli alimtaja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama kioo chake cha Uongozi. Yaonekana namna alivyokabiliana na janga la corona ni katika misimamo ya kutaka kuachwa huru na kile ambacho anakiamini sambamba na wapigania Uhuru walivyopigania Uhuru wa Mtu mweusi.

"...Baba wa Taifa hakuwa mtu wa kuambiwa la kufanya ... hawa wanaoweka haya masharti (ya kujifungia ili baadae tuje kuwa ombaomba), wamezoea kutoa maagizo haya ambayo hata Nyerere aliyakataa," alisema Magufuli kwa kupiga mfano wa namna Mwalimu Nyerere alivyokuwa akikataa ushauri wa mataifa ya magharibi ambao wajamaa hawakuyaamini.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effect of micro-financing on Poverty Reduction.
Tatizo hekima ya hicho kikundi ni 0%. Yaani wangekuwa wana msapoti kwa hali ilivyo sasa 2025 wangeweza kushinda. Kwa sababu sasa hivi Mama Samia yupo peke yake, viongozi wateule hata hawamuelewi. Wanafanya mambo ya ovyo ya kumgombanisha na wananchi na wanamdanganya kwa kumuweka busy na matamasha/warsha/etc ili asifikirie juu ya wananchi.
 
Nikitazama jinsi TZ wanavyo mkataa magufuli APA ndipo Na amini nabii akubaliki kwao
Kila nikitazama comment za inch zingine kwenye youtube wanavyo mkubali JPM dah Na Baki Na shangaa

Ila Sisi Congo tungelipata mtu kama Yule jasiri mtu asiyependa michezo ya kipumbavu au ujinga jinga dah Na Fikiri mpaka Sasa ivi tungeli kuwa mbali kinoma
Kama nchi gani hiyo mkuu? Tupe madini...hahahahahahahaaaaaa!

Pia pitia comments za huku bongo kuhusu ghadafi au kim jon un wa Korea kaskazini. Hao watu sioni wakisemwa vibaya huku.....wabongo ni mwendo wa kuwakweza bila kujua chochote. Oh, anawatolea watu mahali; oh, umeme bure kabisa; oh, ukioa tu unapewa nyumba n.k
 
Hivi kweli mtu mwenyewe IQ kubwa anaweza kwenda kusoma Chuo kikuu kupitia mature age examination Kama huyo jiwe?
 
Hivi na jpm unamfananisha na nyerere. Kweli kuna watu hamna akiri kabisa. Aliua mazao takribani yote ya mbaazi, korosho nk kisa ubabe wake, kaua watu kibao kisa udictator wake, kaua uchumi mpaka inafikia hatua nchi inakuwa na wachuuzi tu (machinga) kila kona ya nchi, wawekezaji kukimbia nk. Mungu katusaidi vinginevyo nchi nzima tungekuwa machizi wa kutembea barabarani tunaongea kama mazuzu. Ajira ndo usiseme kabisa na nyongeza za mishara kwa wafanyakazi alizima zote ikawa ni vilio na kusaga meno ukikosoa tu unaokotwa kwenye kiroba kesho yake
Kama kuna vitu Magu aliniumiza ni kufuta annual increment ambayo ipo kisheria kabisa, mkataba wangu niliosaini na serikali unaonesha kila July kuna fedha inabidi iongezwe kwenye mshahara wangu kukabiliana na mfumuko wa bei, jamaa akatumia ubabe kulizima hili. Hivi wanaharakati wetu na vyama vya upinzani hamlioni hili? Kazi yenu kubwa (mnalipwa kwa hilo) ni kupambana na uonevu kama huu, but nyie mpo kimya, busy kupambana na Kigogo Twitter, Guys you have so much kuweza kuwin hearts za waTZ, Orodhosheni haya mambo yote, then muanze kuyapigia kelele!! Lissu alipiga kelele kuhusu ajira kwenye kampeni 2020, Magu akatangaza ajira za walimu 13000 bila kupenda! Orodhosheni mambo ambayo ni kero kwa wananchi and myashikie bango hayo, mbona before 2015 mliweza? Tatizo ni nini sasa?
 
Tanzania tunao Mwalimu Julius Nyerere,Edward Moringe Sokoine,Hayati Benjamin Mkapa na Daktari John Pombe Magufuli,wengine nitawazungumzia siku nyingine
Huwatendei haki hata kidogo viongozi hao kuwachanganya na mtu kama Magufuli.
In fact unawadhalilisha na kuwanyima heshima zao.

Kumweka Magufuli katika kundi hilo ni lazima ukamchubue na tindikali kali kama "concentrated sulphuric acid" ili kuondoa tabia ambazo hazikuwa za kibinaadam kabisa, tabia zinazoweza kupatikana katika shetani pekee. Kiongozi ambaye hakuwa na ubinaadam kabisa.

Hayo ambayo umeyaona mazuri kwake, ambayo hata sisi tuliyaona, na yangeweza kumweka katika kundi hilo, yalielemewa kabisa na kuondolewa kwa mabaya ambayo wewe unayafumbia macho.

Andiko lako limekosa nguvu kutokana na kuwa kipofu juu ya ubaya wa huyo mtu uliyemchanganya kwenye orodha asiyostahili kuwemo hata kidogo.

Ninakuhakikishia hata katika miaka 50 mingine hutampata tena kiongozi wa hovyo aina ya huyo unayemshabikia wewe. Huyo alikuwa ni shetani katika umbo la binaadam, na Mungu anaipenda sana nchi hii, hawezi kuleta tena kiongozi wa aina yake.

Ungeeleweka vizuri kama ungemshukuru Mungu kwa kuondoa balaa juu ya taifa hili kabla hajatufikisha hatua mbaya zaidi.
 
Watu wa aina hiyo hawahitajiki tena katika karne ya 21 na kuendelea mbele, hizi ni zama nyingine na zinahitaji watu wa aina nyingine kuendana na wakati.
Unajuaje kwamba wasingeweza kuendana na wakati wa hiyo karne ya 21? Ukimwondoa huyo shetani kwenye orodha!
Na ni mambo gani hayo ya kipekee zaidi yaliyopo karne ya 21? Watu wa karne hiyo wana utofauti gani wa kipekee na mahitaji yasiyo ya kawaida yanayohitajika kwa binaadam wa kawaida?
 
BAADA YA MIAKA HAMSINI;TUTAMPATA TENA MWALIMU JULIUS NYERERE,EDWARD MORINGE SOKOINE NA DAKTARI JOHN POMBE MAGUFULI.

Leo 18:00hrs 03/10/2021

Ni nadra sana kupata viongozi wanaoibadili dunia kutokana na falsafa zao na misimamo yao,katika kada mbalimbali ikiwemo siasa, biashara,taaluma,dini na hata wanaharakati. Rais wa kwanza wa Marekani George Washington anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa wa kuiletea uhuru Marekani pia anatajwa kuwa katika list ya viongozi 10 wenye IQ ya 140.Abraham Lincolin anafuatia kuwa mmoja kati ya Marais waliowahi kupendwa sana Marekani na amekuwa mdau mkubwa sana wa Demokrasia,pia anatajwa kuwa na IQ ya 150.Barani Afrika tunao baadhi ya viongozi kwenye list ya viongozi wenye IQ kubwa kati ya 180 hadi 150,Dr Namdi Azikiwe,Dr Kwame Nkrumah,Tanzania tunao Mwalimu Julius Nyerere,Edward Moringe Sokoine,Hayati Benjamin Mkapa na Daktari John Pombe Magufuli,wengine nitawazungumzia siku nyingine,

Wapo pia wanaharakati ambao waliingia kwenye list ya watu wenye IQ kubwa kati ya 180 hadi 150 baada ya harakati zao kubeba uwezo mkubwa,mfano miaka ya nyuma 1960s huko Marekani ubaguzi ulidhamiriwa kufikia kikoko,Ukomo ulikazaniwa hasa katika nyanja za msingi katika maisha ya mtu mweusi nchini Marekani na hapa waliibuka na kuibuliwa waafrka weusi wenye mawazo ya hali za juu miongoni ni Alhaj Malik Al Shabaash maarufu kama 'Malcolm X' na Martin Luther King,Awa walikuwa mahiri kwa kujibu maswali ya waandishi wa habari wazungu, kutoa hotuba za hamasa ya kujitambua kwa mtu mweusi 'Negro' na kutambuliwa kwa haki zao,Martin Luther King aliendesha harakati zake kwa diplomasia ya amani,lakini Malcom X alidhamiria kuishitaki Serikali ya Marekani umoja wa mataifa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa watu weusi.

List ya IQ kubwa pia iliendelea kuwajumuisha wapigania Uhuru wa Mtu mweusi duniani pote,The Pan Africanist,Martin Delany,Alexander Crummel,Edward Blyden,William Sylvester,Dr William Du Bois,Dr Namdi Azikiwe,Marcus Garvey,Kwame Nkrumah,Haile Selassie,Robert Mugabe,Jomo Kenyatta,George Padmore, Julius Nyerere,Kenneth Kaunda,Dedan Kimath,Ngugi Wathiongo, Nelson Mandela,Oliver Tambo,Thomas Sankara,Patrice Lumumba and Dr John Pombe Magufuli.Mzungu alitaka kuleta propaganda kwa kudai mwafrika hawezi kuwa na IQ kubwa,Walifanikiwa kwa Bob Marley hadi kumtenganisha na baadhi ya weusi walioshika misimamo mikali kwa hila tofauti tofauti ili tu ionekane huyu mwenye damu ya mweupe ndio bora na hakuna mwingine anayeweza kuwa bora bila kuwa na uzungu ndani yake. Mf. Peter Tosh alivyotenganishwa na Bob Marley na kupotezwa kwenye anga za ukombozi hadi kukaribia kusahaulika kabisa mbali na tungo zake kutumika 'The Wailers'

-Faida ya IQ kubwa kwa Tanzania,iliyoletwa na Rais Daktari John Pombe Magufuli.

1.Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha SGR kuunganisha Tanzania na nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC umekamilika.Kama ujenzi huo ungekamilika maana yake ni kwamba hakuna Lori litakaloruhusiwa kubeba mizigo inyozidi tani10 kuelekea nchi hizo.

2.By Cash, Serikali ingenunua mabehewa ya mizigo 300, ya Abiria 100 na vichwa vya Treli ya Umeme 20. Manunuzi hayo yamefanyika kwa Cash baada ya Serikali kukusanya fedha za kutosha kupitia vyanzo vya ndani na sio tozo.

3. Bandari ya Dar es Salaam ingekuwa nyeupe kabisa baada ya Ujenzi wa Bandari kavu ya Mlandizi kukamilika.Tungesikia habari kwa sasa wastani wa meli kusubiri bandarini ni masaa 24.

4. Ujenzi wa Bandari ya Mtwara ungepunguza msongamano wa misigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam.Kwa sasa, mizigo ya nchi za Malawi, Zambia na hata Msumbiji inashushwa na kupakiwa Bandari ya Mtwara

5. Wakala wa Umeme vijijini, REA ungefikia tamati baada ya kuunganisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na hivyo kuwa nchi ya kwanza kusambaza umeme vijijini Barani Afrika.

6. Miradi yote ya Maji kwenye vijiji vyote Tanzania Bara na Visiwani imekamilika. Hivyo, wastani wa umbali wa kutafuta maji umefikia mita 10.

7.Dodoma ingekuwa kama Cairo, California,ama New York baada ya kukamilika kwa ujenzi wake kama mji Mkuu wa Tanzania.

8. Serikali kupitia Shirika la Ndege nchini, ATCL imefanikiwa kununua ndege nyingine za kisasa 20 na hivyo kuwa shirika la kwanza la Ndege Afrika kuwa na ndege nyingi zinazoenda karibu nchi zote duniani.

9. Kwa mara ya kwanza vyama vya upinzani vimeshindwa kupata wabunge wengi Bungeni baada ya chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kuambulia mbunge 1 tu. vyama vingine havijapata kiti hata kimoja.

10. Kwa mara ya kwanza Serikali kupitia TPDC wamefanikiwa kufikisha mabomba ya gesi kwenye mikoa yote ya Tanzania. Pia mabomba hayo yamefika nchi jirani za Rwanda, Kenya, Uganda, Msumbiji, Malawi, DRC na Zambia. Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa Gesi Asilia Duniani.

11. Kasi ya ujenzi wa viwanda imeongezeka ambapo kwa sasa ni asilimia 5 tu ya bidhaa zinazohitajika nchini zinaagizwa China,Tanzania sasa ni nchi ya kwanza Barani Afrika kwa kuwa na viwanda vingi na imealikwa kujiunga na nchi za G 7.

12. Sera ya Elimu Bila Malipo imepanuka na sasa wanafunzi wanasoma bila malipo hadi ngazi ya Chuo kikuu,PhD.

13. Huduma ya Afya imeboreshwa nchini na sasa kila kijiji na Mtaa una Kituo cha Afya chenye miundo mbinu yote,hata kufanya operation ya moyo,kuna madaktari bingwa na madawa ya kutosha.

14. Kasi ya ukuaji uchumi imeongezeka kutoka asilimia 7 mwaka 2016 hadi asilimia 30 mwaka 2024.

15.Bwawa la Umeme la Rufiji lavunja rekodi ya kuzalisha Umeme duniani.

-Ushauri Wangu kwa Chadema.

CHADEMA mkimwomba msamaha Magufuli na kuamua kufuata sera na maono yake, 2025 mnachukua nchi kilaini sana".

Nimeyasema haya kwasababu alitaka mjenge naye uchumi lakini mlianza usumbufu. Mkaanza kumsumbua, aliteua hadi watu kutoka chama chenu lakini bado mliendelea kuwa wasumbufu.

Hamkupenda kushirikiana naye ni kwasababu hamkumkubali. Sasa wakati wa kumkubali ndio huu, kuomba msamaha na kufuata sera na nyayo zake. Na sababu za kutomkubali na usumbufu wote mlioanza kumletea chanzo chake ilikua ni sanduku la kula. Hamkuamini ushindi wake 2015.

Basi hamna budi kujitakasa na kumkubali sasa, 2025 ndipo mtaweza kushinda.Nimesema haya kwasababu watanzania kuna kitu wanakiamini. Hicho ndicho mwatakiwa kukifuata.

Mkifanya hivyo hamtahitaji hata kupiga kampeni wala kuitisha mikutano na wananchi au waandishi wa habari. Mtajikuta mnakubalika tu,mkifanya mioyo yenu kuwa migumu basi kile Chama kikichotabiriwa Chama Cha Hapa Kazi Tu kitachukua nafasi yenu na kuvunja rekodi.

-Nukuu ya Rais Daktari John Pombe Magufuli.

Magufuli alimtaja kiongozi wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye pia ndiye aliyeleta uhuru wa Tanzania na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kijamaa, Rais John Pombe Magufuli alimtaja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama kioo chake cha Uongozi. Yaonekana namna alivyokabiliana na janga la corona ni katika misimamo ya kutaka kuachwa huru na kile ambacho anakiamini sambamba na wapigania Uhuru walivyopigania Uhuru wa Mtu mweusi.

"...Baba wa Taifa hakuwa mtu wa kuambiwa la kufanya ... hawa wanaoweka haya masharti (ya kujifungia ili baadae tuje kuwa ombaomba), wamezoea kutoa maagizo haya ambayo hata Nyerere aliyakataa," alisema Magufuli kwa kupiga mfano wa namna Mwalimu Nyerere alivyokuwa akikataa ushauri wa mataifa ya magharibi ambao wajamaa hawakuyaamini.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effect of micro-financing on Poverty Reduction.
Magufuli alikuwa anaipeleka nchi hii kuzimu.
 
Watu wa aina hiyo hawahitajiki tena katika karne ya 21 na kuendelea mbele, hizi ni zama nyingine na zinahitaji watu wa aina nyingine kuendana na wakati.
Kweli kabisa, ... dunia iliyoendelea haihitaji kuongozwa na watu wenye akili za kijima za kufikiri wana akili, higher IQs, kushinda wote na hivyo kuwa na haki ya kuwaamilia watu wote waishi vipi bila kuwashirikisha!
 
Nikitazama jinsi TZ wanavyo mkataa magufuli APA ndipo Na amini nabii akubaliki kwao
Kila nikitazama comment za inch zingine kwenye youtube wanavyo mkubali JPM dah Na Baki Na shangaa

Ila Sisi Congo tungelipata mtu kama Yule jasiri mtu asiyependa michezo ya kipumbavu au ujinga jinga dah Na Fikiri mpaka Sasa ivi tungeli kuwa mbali kinoma
Mlimshindwa nini Koku Ngwendu wa Zabanga a.k.a Mobutu ?!.

Unapenda u dictator kwa wenzio kwako mna wakataa !!
 
Kama kuna vitu Magu aliniumiza ni kufuta annual increment ambayo ipo kisheria kabisa, mkataba wangu niliosaini na serikali unaonesha kila July kuna fedha inabidi iongezwe kwenye mshahara wangu kukabiliana na mfumuko wa bei, jamaa akatumia ubabe kulizima hili. Hivi wanaharakati wetu na vyama vya upinzani hamlioni hili? Kazi yenu kubwa (mnalipwa kwa hilo) ni kupambana na uonevu kama huu, but nyie mpo kimya, busy kupambana na Kigogo Twitter, Guys you have so much kuweza kuwin hearts za waTZ, Orodhosheni haya mambo yote, then muanze kuyapigia kelele!! Lissu alipiga kelele kuhusu ajira kwenye kampeni 2020, Magu akatangaza ajira za walimu 13000 bila kupenda! Orodhosheni mambo ambayo ni kero kwa wananchi and myashikie bango hayo, mbona before 2015 mliweza? Tatizo ni nini sasa?
We Kada, haki zako unataka zipiganiwe na wapinzani huku ukiwapinga ?! . Kwani vyama vyenu vya wafanyakazi , kazi yao ni nini ?!.
 
Mimi siyo kada mzee, mimi siamini katika taasisi, naamini katika watu! Tanzania tuna taasisi nzuri ila tuna watu wabovu wanaoongoza hizo taasisi! Namuunga mkono Samia sababu hana doa lolote, ana nia nzuri na nchi hii, taja doa lolote la Samia..
 
Kuruhusu ubambikaji na kuushabikia . Pili kuikakana katiba ya wananchi aliyoichea yeye. Au niongeze ?!
 
Back
Top Bottom