Baada ya MIAKA 50, Sherehe za UHURU HAZINA TIJA TENA

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Nashauri sherehe za uhuru sasa zifanyike mara moja kwa miaka mitano, maana hazina tena maana, hatuwezi tena singizia ukoloni kushindwa kwetu kupata maendeleo. Sherehe hizo ni gharama kubwa zaidi ya dispensaries 100 huko vijijini, full equipped dispensaries.


Imepitwa na wakati kufanyiwa maadhimisho ya kitaifa kwa gharama kubwa vile, ibaki kwenye historia yetu tu.

Nawasilisha
 
Miaka 50 Zanzibar leo, je bado kunahaja ya kufanya sherehe zinazotukuza ukoloni???
 
Tukupuuze mkuu!
Hujatoa sababu kwanini watu tusifanye sherehe hizi muhimu kwa taifa!
Labda hujaonja magumu ya ukoloni kama sisi wengine lkn angalau wazazi za baby zetu wametuambia kilichotokea na tunaona umuhimu wake. Kwangu mm hoja yako ni dhaifu sana!
 
sherehe inatumia bilioni 98 wakati hakuna vifaa tiba vya milioni 200 tu??? hakuna maabara wala dawa?? basi tuziahirishe kwa miaka 10, tutumie hiyo hela kufanya maendeleo
 
Back
Top Bottom