Baada ya miaka 200, Marekani yapata Waziri wa Fedha Mwanamke

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Baraza la Seneti la Bunge la Marekani limepiga kura na kumuidhinisha kwa wingi mkubwa mwanauchumi anayeheshimika Janet Yellen kuwa waziri mpya wa fedha wa taifa hilo.

Wajumbe wa Seneti wamemuidhinisha Yellen kwa kura 84 za ndiyo dhidi ya 15 za hapana na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza wizara ya fedha tangu ilipoanzishwa zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Yellen anatajwa kuwa miongoni mwa wachumi wenye tajriba kubwa baada ya hapo kabla kufanya kazi kama gavana wa benki kuu ya Marekani na mjumbe wa Baraza la washauri wa uchumi wa Ikulu ya White House.

Katika hatua nyingine kamati ya masuala ya mambo ya kigeni ya Baraza la Seneti imemuidhinisha mwanadiplomasia mkongwe Antony Blinken kuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani. Hatua hiyo inamsafishia njia Blinken yakuidhinishwa na Baraza la Seneti litakapopiga kura wiki inayokuja.
 
Waafrica tutafakari maamuzi ya Hawa mabeberu. Haiwezekani sisi wanatuimbia wimbo wa 50/50 angali wao bado. Hebu oneni zaidi ya miaka 200 ndio wanapata waziri wa fedha mwanamke.

Acha hilo Hilary Clinton ndio angalao walitegemea awe mwanamke wa kwanza kuwa raisi wa marekani. Chunguza bunge/ Baraza lao la seneti kama utakuta 40% ya wanawake.

Kulazimisha usawa kuwe na mantiki coz wanajua wakitulazimisha kuwa na usawa bungeni na nyanja mbali mbali za uongozi n kuchagua hata watu wasiofaa coz tunataka 50/50.
 
Safi Sana nimefanya rejea ya machapisho yake kwenye economics pamoja na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa benki kuu prof.Ben Benanke ,hao ni wachumi wazuri

Unfortunately huku Bongo ushauri wa kitaalamu huwa haufuatwi wala kuheshimiwa wenye madaraka ambao wengine ni wasomi bado wanategemea ramli za kaka kuona
 
Waafrica tutafakari maamuzi ya Hawa mabeberu. Haiwezekani sisi wanatuimbia wimbo wa 50/50 angali wao bado. Hebu oneni zaidi ya miaka 200 ndio wanapata waziri wa fedha mwanamke.

Acha hilo Hilary Clinton ndio angalao walitegemea awe mwanamke wa kwanza kuwa raisi wa marekani. Chunguza bunge/ Baraza lao la seneti kama utakuta 40% ya wanawake.

Kulazimisha usawa kuwe na mantiki coz wanajua wakitulazimisha kuwa na usawa bungeni na nyanja mbali mbali za uongozi n kuchagua hata watu wasiofaa coz tunataka 50/50.
Sidhani kama wanalazimisha bali wanajaribu kuweka mazingira sawa kwa wote ili Lila mtu pasi kujali jinsia awe na haki sawa tena sio kwa previlage but on merit na hata hao wao kwa mfano akina C.Rice walipata hizo nafasi on merit na si vinginevyo
 
Sijui ni mimi tu huwa nafikiria kuwa Kamala Harris is going to be the president, it's not going to be Joe Biden.

Joe will either step down or be unfit to serve within 2 years of his term in which case Kamala will be the president.

Nahisi Joe Biden anatumika kama figure head to get Kamala Harris into the White House by the back door.
 
Baraza la Seneti la Bunge la Marekani limepiga kura na kumuidhinisha kwa wingi mkubwa mwanauchumi anayeheshimika Janet Yellen kuwa waziri mpya wa fedha wa taifa hilo.

Wajumbe wa Seneti wamemuidhinisha Yellen kwa kura 84 za ndiyo dhidi ya 15 za hapana na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza wizara ya fedha tangu ilipoanzishwa zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Yellen anatajwa kuwa miongoni mwa wachumi wenye tajriba kubwa baada ya hapo kabla kufanya kazi kama gavana wa benki kuu ya Marekani na mjumbe wa Baraza la washauri wa uchumi wa Ikulu ya White House.

Katika hatua nyingine kamati ya masuala ya mambo ya kigeni ya Baraza la Seneti imemuidhinisha mwanadiplomasia mkongwe Antony Blinken kuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani. Hatua hiyo inamsafishia njia Blinken yakuidhinishwa na Baraza la Seneti litakapopiga kura wiki inayokuja.
weka picha yake
 
weka picha yake
1611817500635.png
 
Back
Top Bottom