Baada ya mauaji ya ajabu kutokea Kangaye Mwanza, sasa wananchi kufunga siku tatu mfululizo

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,482
20,426
Baada ya watu watatu kufariki wakati wa mazishi na hivyo kusababisha misiba kufika minne, wakazi wa Kangaye Mwanza wameamua kufunga kwa siku tatu mfululizo kuomboleza misiba hiyo pamoja na kuombea amani katika eneo lao.

Itakumbukwa siku sio nyingi wakati mazishi yakiendeleaa, mtu mmoja alitoa bastola kwa nia ya kupiga hewaani ili kuwaandaa mababu kumpokea marehemu huko aendako lakini kwa bahati mbaya alimpiga muombelezaji mwingine na kumsababishia kifo, ambapo wananchi wenye hasira walimshambulia naye hadi kumsababishia kifo. Wakati purukushani zikiendelea mtoto mmoja alipata majeraha ambayo yalimsababishia kifo.

Mwenyekiti wa mtaa huo ametoa wito kuwaomba wananchi kuepuka kula hadharani wakati wa kipindi hiki cha mfungo.
 
Mwenye bastola ni miongoni mwa wale wanaomiliki silaha kwa kutafuta sifa kuwa anamiliki cha moto.

Ni aina hiyohiyo ya yule jamaa aliyemuua rafiki yake na yeye kujiua pale sinza.

Mamlaka ya utoaji vibali vya kumiliki silaha iongeze umakini.
 
Gross mistake ya yule jamaa alietoa bastola imegharimu maisha ya watu 3, 3 innocent lives lost yeye mwenyewe akiwemo.
 
Kuhusu swala lakufunga si kweli mkuu nachojua aliyepigwa risasi alikufa papo hapo ila aliyepiga risasi alifia hospital ya mkoa,mwanza baada ya wanafunzi wa kangaye sec na wananchi wenye hasira kali kumshambulia. Kalibu elephat pub hapa round about kangaye mkuu
 
Back
Top Bottom