Baada ya Masanja kutumia picha za miradi ya Lesotho kuisifia Serikali ya awamu ya tano, Msemaji wa Serikali naye kaja na upotoshaji huu

Kwani huyo Masanja alikuwa na haraka gani, si angesubiri mpaka mradi ukamilike kisha alete picha? Hayo si ndio mambo ya kumpelekea mzazi wako picha ya mrembo kusema ndio utamuoa, kisha ukioa mwingine useme shida iko wapi wakati ni mwanamke kama mwanamke aliyeko kwenye picha?

Huyo Masanja ana uhakika gani kama huo mradi utakamilika? Na unapata wapi uhakika kuwa bei itakuwa chini baada ya kukamilika? Huo umeme wa gas si tuliambiwa bomba la gas likifika Dar umeme utashuka bei, je umeshuka? Huo ni mradi wa mkopo, una uhakika gani na bei kuwa chini?
Masanja anajua haraka yake na sababu zilizomfanya aposti aliyoposti kwenye page yake. Hajamwambia mtu aiangalie au amfuatilie. Yaani ametumia uhuru wake wa kujiexpress kufanya ile kitu roho yake inapenda. Kwanini muumie wengine?
 
Masanja anajua haraka yake na sababu zilizomfanya aposti aliyoposti kwenye page yake. Hajamwambia mtu aiangalie au amfuatilie. Yaani ametumia uhuru wake wa kujiexpress kufanya ile kitu roho yake inapenda. Kwanini muumie wengine?

Hakuna anayeumia bali anaambiwa aache upotoshaji wa kipuuzi. Kama hakutaka watu waangalie, angeiweka kwenye hiyo single room yake anayoishi.
 
Masanja ni mchungaji comedian fulani hivi mjini pia ni mkulima wa mpunga mwanachama wa ccm mtata fulani hivi. Mhamiaji kutoka Ludewa kwenda Rujewa kabila Mpangwa mmoja hivi wengi wanafikiri ni mnyakyusa si kweli asili yao ni Ludewa Njombe. Jina halisi Emmanuel Mgaya.
Oh nimesahau kidogo sifa kuu ni mcccm fulani hivi pia anafanya matangazo ya barabarani kupitia DW
Natumai nimejibu vyema
Ahsante nashukuru kwa taarifa
 
Huyu dada ni mkurupukaji tu kama viongozi wengi tu upinzani. Anajidadavua kama mwenyekiti wa BAVICHA TEMEKE.

Hapo Masanja kadanganya nini na wapi?
Hajasema imefikia hivyo lakini ukiangalia ile michoro yao, hivyo ndivyo bwawa litakavyoonekana.

Ukimuuliza huo umeme ukikamilika atapinga kuutumia? Siasa nyingine za kishenzi shezi tu.

Si aeleze mipango yao mbadala ya kutuletea umeme utakaokuwa na bei nafuu zaidi ya huo wa Rufiji?
Ila kwakuwa hakuna sera mbadala, kaamua amshambulie mtu binafsi.
Ww ndio mkurupukaji, soma vizuri uelewe
 
Sasa huyo si comedian jamani?.
Alichopost ni comedy ya swali la uhalisia wa kitu, watu wakamdandia kana kwamba kilichopostiwa ni halisi 😂😂😂 kumbe ni picha ya yatarajiwayo.
Ni sawa sawa na yeye kumuuliza aliyeko Dodoma "mji mkuu wa Tanzania ni Chamwino? na yeye kujibu ndio kwa kuwa ndiko Ikulu inapojengwa ""
Sema kosa la Masanja ni kupost kipindi hiki, angelisubili April Mosi Mwakani.
 
Back
Top Bottom