Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,565
Wanabodi,
Hili ni bandiko la ma GT, hivyo hatutataji majina na naomba usitaje jina lolote!.

Hatua ya kwanza ni sikiliza kauli hii


Hivi hata baada ya kauli kama hii, kama wewe ni mtu mzima na akili zako timamu, bado unasubiri nini to do the right thing, the needful?.

Swali ni jee tumshauri mtu wetu, a do the needful, au akomae nao, till they do him away?.

Mimi nimemsikiliza Mama, kiukweli hajamtendea haki mtu wetu!, zile kauli kuhusu tozo, mikopo na deni la Taifa ni kauli za kizalendo na wala sio homa 2025, kwasababu kiukweli kabisa mtu wetu, hajawahi hata kuwazia 2025 kwasababu ndani ya CCM kuna a silent code ya kupokezana fulani kati ya Wakatoliki na wale jamaa zetu!.

Kwa vile alianza Mkatoliki, Juliasi akaja Jamaa zetu, Hasani, akaja Mkatoliki Benyamini Wiliamu, akaja jamaa zetu Mrisho, akafuta Yohane Yosefu, hivyo 2025 ilikuwa ni zamu ya wale jamaa zetu na Mungu ndio akawatangulizia, hivyo kusema kauli ile ya kizalendo ni homa ya 2025, huku ni kumsingizia bure tuu huyu mtu wetu!.

Kwa vile the boss is always right, ikitokea ume differ na boss wako, to the point ya bosi wako to question your intellect "mtu mzima mwenye akili timamu", the best way is to Quitt, the sooner, the better.

Namalizia kwa swali hili la msingi, baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama mtu wetu ni timamu, he shoud do the right thing, "the needful", jee tumshauri to do the right thing, "The Neeful?", before its too late, au akomae nao, mpaka kieleweje, if it is to do him away, akomae till they do him away?. The game is on again, it is not over yet until it's over.

I might end up being right again!

Paskali
Rejea

 
Mama inawezekana hana taarifa za kina kuwa hana support ya kutosha ndani ya CCM na atakuja kushtuka kina Ndugai wako wengi tu wakiwemo wanaojidai kumuunga mkono leo hii kumbe wanamlia timing tu.

Kuna wataomuunga mkono kutafuta uteuzi tu na sio kwamba wako loyal kwake.
 
Tukilipa LUKU tunakatwa hela ya kusambaza umeme.

Hiyo hela inaenda wapi?

Mama anakosea sana kuachana na kundi la wanyonge ambao ndiyo wengi na kuanza kukumbatia kundi la walichonacho ambao hawazidi hata millioni 3 nchi nzima
 
Mama amehemukwa, nafikiri hii nafasi alikuwa anaisubiria kwa hamu sana na ameitendea haki....

Sasa hivi kila atakaeinua mdomo juu ya mama itaonekana ni joto la 2025, nilichofurahi Mama anawajua maadui zake.

Jamaa yetu jana ilibidi akanushe sio kuomba radhi, Sasa ameomba radhi na kichambo kapewa juu....

Mama kaita CCM nchi nzima imsaidie kumchamba Jamaa yetu
 
Mtu wetu hatakiwi kufanya hicho unachotazamia kuifanya......kwa kilichoonekana ni kwamba taasisi ya u rais imelewa madaraka....na haikubali kupokea mawazo au maoni yanayokinzana na utashi wao..

Taasisi ya u rais imejaa ubabe na utemi unaojengewa kiburi na KATIBA mbovu.

Hii inaonyesha ni jinsi gani tuna mhimili dhaifu kwa kuwa serikali imetawaliwa na ubabe badala ya hoja.

Tuna watawala wanafiki wasiokubaliana na kile walicho tuhakikishia kuwa wanakiamini.
 
Nakumbuka fulani aliwahi kutoa kauli ya kupumzika siasa 2025, alichofanya "mwenye nchi" leo ni kuonesha yeye binafsi anavyoiwaza 2025 na ameshanogewa na cheo, ndio maana alikuwa wa kwanza kuwaambia wanawake wenzake 2025 ni zamu yao.

Mengi ya maneno aliyotoa kumjibu mwenzake leo ni mihemko tu na kuchamba kama zilivyo tabia za wanawake wengi, lakini hana hoja yoyote ya msingi.

Kwa hii kauli yake ya leo inawezekana akaamsha vita ya chini chini ambayo hatajua ukubwa wake na miongoni mwa adui zake watakuwa hao wanaompigia vigelegele leo.
 
Hii conflict Kati ya executive na Bunge itufungue macho kwa hitaji la katiba mpya. Speaker kuzodolewa namna ile ni kuonesha ya kwamba Bunge letu halina nguvu. Katiba mpya inahitajika kuweka checks and balances. Tatizo ukisema katiba mpya watu wanafikiria CHADEMA basi, lakini madhara Kama haya hawayaoni.
 
Tukilipa LUKU tunakatwa hela ya kusambaza umeme.

Hiyo hela inaenda wapi?

Mama anakosea sana kuachana na kundi la wanyonge ambao ndiyo wengi na kuanza kukumbatia kundi la walichonacho ambao hawazidi hata millioni 3 nchi nzima
Luku tozo, benki tozo,miamala ya simu tozo, tumebanwa kila kona. Mfumuko wa bei upo juu, yaani kama haukujenga kipindi cha JK usahau
 
Back
Top Bottom