Baada ya malalamiko ya muda mrefu, hatimaye Serikali imeanza kutoa motisha kwa Walimu wa Sayansi

Siwezi kuwawekea waalimu,hii salary unayoona ni ndogo jua iko juu Sana kuliko wafanyakazi wengi wa serikali kuu na kumbuka walimu wanasiku chache kazini jwa mwaka na wanawahi kutoka kazini tofauti na wafanyakazi wengine
Taratibu za utumishi wa umma ni sawa haijalishi ni mwalimu, afisa kilimo au mkuu wa majeshi.
Muda wa masaa ya kazi ni sawa hakuna anaekaa masaa mengi kazini na ukikaa masaa mengi kazini unatakiwa ulipwe kwa kila saa linalozidi.
Wako walimu pia wa shule za bweni hadi saa nne usiku wanasimamia watoto prepo.
 
Nadhani yeye anamaanisha likizo za muhula wa masomo.

mwezi wa 3---likizo wiki 2

mwezi wa 6---likizo mwezi 1

mwezi wa 9----likizo wiki 2

mwezi wa 12---likizo mwezi 1

pamoja na kwamba mwl anakuwa na likizo mara moja kwa mwaka ila hata hizo likizo za masomo anakuwa anapompumzika
 
Angalau serikali imeanza kurudi kwenye chati.

Kulikuwa na madai na maoni mbali mbali kuhusu changamoto wanazopitia walimu wa sayansi, miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na mzigo mkubwa wa vipindi, kutekeleza majukumu ya watu wa maabara kama vile kuandaa na kusimamia practicals, kubaniwa baadhi ya promosheni kutokana na uchache wao na mambo mengine mengi

Kutokana na hali hiyo, wadau mbali mbali wa elimu walitoa maoni yao na kubwa zaidi wakitaka serikali kuwapa motisha walimu wa sayansi ili kuwatia moyo na hamasa ya kujituma zaidi katika kazi. Baadhi ya maoni yaliyotolewa na wadau hapa hapa JF ni haya hapa chini.

1. Maoni: Walimu wa masomo ya Sayansi wapewe malipo ya ziada

2.
Sasa, baada ya maoni hayo ni rasmi serikali imeyasikia hayo malalamiko na imeamua kuyafanyia kazi kwa vitendo.

Kwa hatua ya sasa, serikali imeanza kwa kuongeza kiasi kidogo( japo si haba!) kwenye mishahara ya walimu wa sayansi.

Sambamba na hilo, walimu wapya wa masomo ya sayansi wameanzia kidato cha tatu cha mshahara( tgts d3). Wa sanaa wameendelea na utaratibu ule ule wa mwanzo wa kuanzia kidato cha kwanza(tgts d1).
Mambo mengi tupo nyuma sana sana, ila twaanza kujitambuwa..hongera kwa hilo..
 
Nadhani yeye anamaanisha likizo za muhula wa masomo.

mwezi wa 3---likizo wiki 2

mwezi wa 6---likizo mwezi 1

mwezi wa 9----likizo wiki 2

mwezi wa 12---likizo mwezi 1

pamoja na kwamba mwl anakuwa na likizo mara moja kwa mwaka ila hata hizo likizo za masomo anakuwa anapompumzika
Hiyo naona inategemea na sehemu ya kazi. Wengine wakati wanafunzi wako likizo walimu wanasahihisha mitihani na kupanga matokeo.
Lakini pia kuna taasisi nyingi kuna loophole. Mfano:
1. Hamashauri kuna idara ya michezo na utamaduni fikiria huwa wanafanya nini kila siku?
2. Kuna hawa afisa TRA wanaokadiria kodi akisaini ofisini anatoka kuingia field je kila siku anakuwa huko field nani anamuona?
Ziko taasisi nyingi watumishi wanakula bata tu. Mambo ni mengi muda ni mchache
 
Angalau serikali imeanza kurudi kwenye chati.

Kulikuwa na madai na maoni mbali mbali kuhusu changamoto wanazopitia walimu wa sayansi, miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na mzigo mkubwa wa vipindi, kutekeleza majukumu ya watu wa maabara kama vile kuandaa na kusimamia practicals, kubaniwa baadhi ya promosheni kutokana na uchache wao na mambo mengine mengi

Kutokana na hali hiyo, wadau mbali mbali wa elimu walitoa maoni yao na kubwa zaidi wakitaka serikali kuwapa motisha walimu wa sayansi ili kuwatia moyo na hamasa ya kujituma zaidi katika kazi. Baadhi ya maoni yaliyotolewa na wadau hapa hapa JF ni haya hapa chini.

1. Maoni: Walimu wa masomo ya Sayansi wapewe malipo ya ziada

2.
Sasa, baada ya maoni hayo ni rasmi serikali imeyasikia hayo malalamiko na imeamua kuyafanyia kazi kwa vitendo.

Kwa hatua ya sasa, serikali imeanza kwa kuongeza kiasi kidogo( japo si haba!) kwenye mishahara ya walimu wa sayansi.

Sambamba na hilo, walimu wapya wa masomo ya sayansi wameanzia kidato cha tatu cha mshahara( tgts d3). Wa sanaa wameendelea na utaratibu ule ule wa mwanzo wa kuanzia kidato cha kwanza(tgts d1).
Salary imeingia leo 25/1/2021 hakuna mabadiliko yeyote. Hizi habari ulisikia wapi?
 
Duh! Kama mwalimu wa sayansi analipwa 716,000/= na ameongezewa 40,000 kuwa 756,000/= huyu anayefundisha sanaa(Kiingereza, kiswahili, histori,Jiografia n.k) analipwa bei gani?Yumkini ndo maana shule za Serikali performance iko very poor! Mishahara haitoshi kabsaaaa!!!
Leo mwanasiasa Mbunge tena class 7 anakula zaidi ya 5m/= per month na seating allowance 300,000/= per dm!!!What a disgrace to teachers???
Hiyo yenyewe 716000 sijui 756000 ni basic,wakitoa kodi na makato mengine mtu net pay yake ni laki nne. Usishangae.
 
Walimu ni kundi ambalo limejaa vilaza wengi sn
Mimi ninachojua mdogo wangu alimaliza mwaka juzi kidato cha nne tulipotaka kumpeleka diploma ya ualimu alikosa vigezo hadi awe na cheti cha form six chenye E na S.
Ila cha ajabu chuo cha afya alipata diploma kwa D nne za form four tu.
Kumbe vigezo vya diploma ualimu ni vikubwa kuliko afya.
 
Back
Top Bottom