Baada ya Makumira, Uhasibu Aarusha nao kufungua tawi la CDM

Ndugu wana JF, baada ya jana Kamanda Mbowe kufungua Tawi la CDM pale Makumira university, habari nilizozipata sasa hivi ni kwamba Chuo cha uhasibu Arusha nao wako kwenye mazungumzo na uongozi wa CDM Mkoa juu ya uwezekano wa kufungua Tawi lao haraka iwezekanavyo.
Chanda chema huvishwa pete.

Wanaohoji uhusiano kati ya CHADEMA wanafunzi vyuoni shauri yenu maana wameona CCM mambo hamuyawezi ndipo wakaja kwetu.

Msambano sema nao wanaohoji CHADEMA kupendwa na wapiga kura chipukizi nchi.
 
Big up CDM shika wanavyuo wote baadaye wape nyenzo waende vijijini, CDM msisahau kuja huku SAUT moto wa huku ni mkubwa kuliko muulizeni Masha atawasimulia.
Haya sasa mnaona nako tena SAUT nao ndio wenyewe wameamua kuwaita CHADEMA taifa kwenda kufungua tawi huko.

Sasa wale walio na kasumba ya kuhoji uhusiano kati ya CHADEMA na wanafunzi nchini ndio mjue kwamba chama hiki hakijipereki huko bali ni kwamba wao hukaribishwa tu na uongozi wa wanafunzi hawa wanaoumwa roho CCM inavyoibaka uchumi wa nchi.

Dr Slaa na timu yako zima hapo makao makuu, kanyaga twende!
 
Kazini kidogo inakua issue kujikita kwenye siasa moja kwa moja ni bora hao wabaki wanachama tu vinginevyo kweli vibarua vitaota nyasi. Chadema wafanye hima kufungua matawi kwenye vyuo vyote kuna jamaa yangu yuko pale Morogoro University of Muslim (MUM) anasema nao wanasubiri kwa hamu hatua hiyo..
 
Pamoja na jinsi watu walivyowachukia wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma, ukweli utabaki kwamba ni hawa hawa wana-UDOM ndio waliokua wa (i) kwanza kufungua tawi la CDM chuoni, (ii) wa kwanza kuitisha maandamano kutetea maslahi ya umma, (iii) wa kwanza kuchangia marehemu mashujaa wetu wa Arusha japo kwa uwezo wao kiduchu.

Shime sana UDOM na vyuo vingine vingi nchini mlioona haja ya kujitokeza na kuhesabiwa mchana kweupe kama wapambanaji halisi mnaochukia ufisadi na mashaibu yake yote nchini.

BG UP saaannnnaaaaaaaaaaa!!!!
 
Kazini kidogo inakua issue kujikita kwenye siasa moja kwa moja ni bora hao wabaki wanachama tu vinginevyo kweli vibarua vitaota nyasi. Chadema wafanye hima kufungua matawi kwenye vyuo vyote kuna jamaa yangu yuko pale Morogoro University of Muslim (MUM) anasema nao wanasubiri kwa hamu hatua hiyo..

Aaaaa wakitaka wachalazwe viboko na mashehe wajaribu!
 
Aaaaa wakitaka wachalazwe viboko na mashehe wajaribu!

kilembwe, nakuheshimu sana, u r a seniour jf member, na mimi nimejiunga mda sio mrefu sana,,, lakini ndugu yangu, huoni kwa maneno yako unaweza kuwachochea mashehe na kweli wakawaletea chadema kwere na ikawa chanzo cha udini???...na je, tungekaa kimya na mambo yakaenda sawa huoni ingekua aheri kwetu na kwa nchi yetu kwa ujumla??
 
Taratibu moto wa ukombozi unasambaa nchi nzima.....hara hara CDM msisahau na SUA tu!...ah na mzumbe na hata pale Muslim Univsity kabla ya kwenda kuvunja lile tawi la kijani UDOM
 
Vijana tunawategemea sana, msikubali kununuliwa mkauza uhuru wenu; ukombozi utaletwa na nyie, na sisi tutawapa every possible support. Angalieni baada ya hawa mijamaa kuondoka mtapata nini humu nchini kama tutkiruhusu waendelee tu kuneemeka na kuchukua vyao mapema? Don't be side tracked by the few who ate crumbs from their tables and they think that is life; duh, sitaweza kamwe kuuza uhuru wangu kwa kupokea crumbs; wanafikiri hapo wana share the real thing na hao mafisadi kumbe wao wako mbali sana sana; they are simplying using you to continue to eat those few crumbs so that wakutumie kuwapigia debe....ndivyowanavyofanya hao wachache, wapiga debe, hivi hamwaoni huko vituoni wanavyofanana? Je, tunaweza kweli kuwalinganisha na owners wa hao transport vehicles? No way can they be compared...
 
Ndugu wana JF, baada ya jana Kamanda Mbowe kufungua Tawi la CDM pale Makumira university, habari nilizozipata sasa hivi ni kwamba Chuo cha uhasibu Arusha nao wako kwenye mazungumzo na uongozi wa CDM Mkoa juu ya uwezekano wa kufungua Tawi lao haraka iwezekanavyo.
Tunapongeza hilo.Hata hapa St Joseph Songea tungependa kufanya hivo lakini wahindi hawataki kabisa siasa hapa.
 
Back
Top Bottom