Baada ya makampuni ya Tanzania kuchafuliwa,kuna mkakati kama taifa kuyasafisha?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Makampuni ya Tanzania yametupiwa lawama za kuagiza sukari iliyokwisha muda wake,wanaipaki na kuiuza,makampuni haya yanafanya biashara kimataifa na nchi kama rwanda,uganda,burundi congo,sudan,ethiopia nk,kauli za hapa nchini zinafuatiliwa kimataifa na zinaharibu sifa za makampuni haya,wengine wameitwa mashetani, pia hata pale bandarini makapuni ya uwakala yalifungiwa lakini baadae yakafunguliwa kimyakimya,nahoji je kuna mkakati wa kuyasafisha makampuni haya au yaende mahakamani yakajisafishe?
 
Si jambo jema sana katika ukimwengu wa kileo. Wafanyabiashara na matajiri ni makundi mengine yenye wajibu sawia kuchangia maendeleo na kunufaika na keki ya nchi yao. Ikitokea yana matatizo ni vizuri kutatua matatizo hayo bila kuathiri taswira yao.
 
Msameheni bure yule msukuma ana ugonjwa wa kupenda sifa. Labda baada ya muda atazoea ingawa damage imeishatokea. Ingawa amefanya vizuri katika kurudisha nidhamu ya utendaji, anaelekea kuifanya Tanzania sio mahala salama kiuwekezaji na hii itakosesha vijana wengi ajira
 
Hayo makampuni yajisafishe yenyewe kwa kuacha michezo hiyo michafu.
 
Tatizo Mzee wetu huyu akishakamata mike yan anajisahau kabisa kwamba ni rais. Tumvumilie tu.
 
Kweli kweli kabisa,kuna haja ya kukutana kati ya serikali na wawekezaji wote ili kujenga mahusiano,kila mahali wanaandamwa,ni kama kuna crusade
 
Back
Top Bottom