Baada ya Magufuli kupita Kigoma, Zitto afanya kazi ya safisha safisha!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Baada ya Dkt. Magufuli kupita mkoani Kigoma na kumwaga sera zake.

Kisha kesho yake akafuatia Lissu aliyekwenda kung'oa magugu na kupanda ngano yake

Siku iliyofuata, Ikawa ni zamu ya Zitto kupita Kigoma na kung'oang'oa magugu zaidi na kwa kufanya hivyo indirectly akapalilia ngano iliyopandwa na Lissu

Kama sote tujuavyo, uwezo wa Zitto wa kuzungumza kwa Takwimu na mifano, Zitto akaivunjavunja hoja ya Magufuli kuwa anawapenda wana Kigoma ndiyo maana akateua wabunge watatu wa mkoa huo akiwemo waziri Mpango

Zitto akatoa mifano iliyohai jinsi waziri Mpango "mtoto wa nyumbani" "alivyoshindwa kuwa msaada kwa mkoa wake hata kwa vitu vilivyo obvious kabisa visivyohitaji upendeleo wowote.

Zitto akaeleza kuhusu miradi na fedha za msaada zilizokusudiwa makhsusi kwa mkoa wa Kigoma na jinsi waziri huyo alivyoitosa Kigoma kwa kutokutoa ushirikiano.

Kwa nondo hizi za Zitto, ni dhahiri Zitto anafanya kazi ya safisafisha inayoenda kumnyang'anya Magufuli mkoa huo ambao ni kete muhimu sana kwenye uchaguzi huu na pia inaonekana ni dhahiri Magufuli ameonyesha makusudio ya kuutwaa kwenye uchaguzi huu ndiyo maana kaweka nguvu kubwa sana ya kampeni katika mkoa huo.

Kwa hii kazi ambayo Zitto kapiga huko Kigoma, ni dhahiri Juhudi ya Magufuli katika mkoa huo imepotea bure, Zitto anamdelete Magufuli kutoka katika mkoa huo kwa nondo kali bila huruma!

Kwa video cheki hapa chini

 
Safi sana. Magufuli kila anakopita ni aibu kubwa. Huko Kagera ni afadhali asingeenda. Ikamlazimu kumfukuza Mwenyekiti wake wa CCM Mkoa. Akakimbilia Kigoma. Baada ya kutamka uongo wake huko, Lissu na Zito wamepangua uongo kwa takwimu na uhalisia.

Magu kabaki kufanya fiesta ya wasanii wasio na maadili jukwaani. Kura Kagera na Kigoma zimeshamponyoka. Tusuburi aibu nyingine mikoa anayokwenda.
 
The same Location nani kafagia hapo mkuu hahahahahahaa
1600701516972.png
 
Safi sana. Magufuli kila anakopita ni aibu kubwa. Huko Kagera ni afadhali asingeenda. Ikamlazimu kumfukuza Mwenyekiti wake wa CCM Mkoa. Akakimbilia Kigoma. Baada ya kutamka uongo wake huko, Lissu na Zito wamepangua uongo kwa takwimu na uhalisia.

Magu kabaki kufanya fiesta ya wasanii wasio na maadili jukwaani. Kura Kagera na Kigoma zimeshamponyoka. Tusuburi aibu nyingine mikoa anayokwenda.
Kumbe amemfukuza mwenyekiti Kagera?
 
The same Location nani kafagia hapo mkuu hahahahahahaa
View attachment 1576363
Hata kuficha uongo mafisi---em mnashindwa ee hata kuiba kura mtashindwa hivyo hivyo. Siku zote mwizi/muongo huacha alama zinazosaidia kumumbua/kumkamata. Picha ya kijani imepigwa wakati mgombea wenu yuko pale na ile ya pili imepigwa mapema wananchi wakiwa wanawasili kumsubiria mgombea. Tuonyeshe mgombea wa CHADEMA alipo kwenye hiyo picha.
 
Kwa kweli zitto kaongea kwa uchungu kuhusu kigoma na takwimu alizonazo
Hizi ndizo siasa hai zenye mlengo wa kumshinda mpinzani wako. Mwenzako akirukaruka tu kusema nilifanya hivi ama vile mpinzani lazima aje na facts kuonesha uongo wako. Hapo Kigoma Lissu na Zitto wamefanya kitu very credible.
 
Back
Top Bottom