Baada ya Magufuli kufa mafisadi wanaweza kurejea. Je, CHADEMA watairudia sera yao ya kupambana na mafisadi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
45,014
2,000
Nauliza tu kwa nyie makamanda mliomo humu jamvini, baada ya komandoo wa kupambana na ufisadi hayati Magufuli kumaliza safari yake hapa duniani, CHADEMA itairudia ile sera yake ya kupambana na mafisadi?

2015 CHADEMA waliachana na sera ya mafisadi baada ya kuwapokea makada maarufu wa CCM wakiongozwa na mzee Lowassa, Mzee Sumaye na rip Ngombale mwiru.

RIP Magufuli!
 

Shift

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
1,056
2,000
Tutaanza na mwendazake, tutakuja ukabila na nakuhapia kutakua na Ufisadi wa kutisha kupata kutokea kwa histories ya nchi
 

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
3,589
2,000
Kuna kakundi, ndani ya CCM, kalikokuwa karibu sana ya JPM, kalikokuwa kananeemeka huku kakiwapumbaza wanyonge kuwa kanawatetea, kana hofu ya kupoteza nafasi yake kwenye utawala mpya na kanaanza kuandaa mazingira ya kuhakikisha utawala mpya haulali kwa KINYAGO KITAKACHOANDALIWA CHA WAPAMBANAJI DHIDI YA UFISADI!

... TUWAZIKE VIZURI KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA, WENYE UWAZI, UTAKAOWEKA KILA KITU HADHALANI!
 

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
1,730
2,000
Waliokua wanatafuna pesa za ruzuku za CHADEMA kuanzia 2015 hadi 2020 tuwaiteje mafisadi au wazalendo.

Maana wamesababisha CHADEMA ipoteze viti vyote vya ubunge
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
795
1,000
Fisadi namba moja pale ufipa ni mwenyekiti wa chama aliekula hela za wabunge waliochanga kwa muda wa miaka 5, bila kusahau ruzuku ya chama.

Ndio maana kwa sasa hawawezi kuirudisha hiyo sera ya ufisadi maana wasipoangalia inaweza kumnasa mwenyekiti na genge lake la wanywa gongo aliowasambaza humu mitandaoni wamkingie kifua
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,026
2,000
Kwenye kampeni za uchaguzi kuelekea October 2020, Tundu Lissu alimtaja JPM kama fisadi na alitoa mifano kadhaa, cha ajabu hakuna MATAGA hata mmoja aliyemjibu kwa hoja isipokuwa tuliona na kusikia zaidi matusi na vitisho vya kumchoma sindano ya sumu.

Ufisadi miaka 5 iliyopita ulikuwepo kwa na sura tofauti - ulikuwa laundered within an institution!
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
41,847
2,000
Waliokua wanatafuna pesa za ruzuku za CHADEMA kuanzia 2015 hadi 2020 tuwaiteje mafisadi au wazalendo

Maana wamesababisha CHADEMA ipoteze viti vyote vya ubunge

CHADEMA wamepoteza viti vyote vya ubunge, kwani hiyo 2020 kulikuwa na uchaguzi, ama maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom