Baada ya Magufuli kuapishwa, Mbowe, Sumaye, Kingunge na wafuasi wa CHADEMA, mje mtuambie

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1. Mbowe uje utuambie kama kweli ulikuwa unamaanisha kuwa Lowassa ni msafi na angefaa kuwatumikia watanzania wengi walio wanyonge au lengo lilikuwa ni mtaji wa kupata wabunge wengi kuliko wale ambao mliwapata kupitia Mtaji wa Dr. Slaa au NI UKWELI ULICHOTA MPUNGA KUTOKA KWA LOWASSA?

2. SUMAYE na wewe uje utuambie, hivi ni kweli uliyokuwa ukiyasema majukwaani kuwa LOWASSA ndiye atakayewaletea watanzania mabadiliko yalikuwa yanatoka moyoni? Au kwa vile wote nI watuhumiwa wa wahujumu uchumi wa nchi hii, yakiwemo MASHAMBA MAKUBWAwezi, mali ya Watanzania WANYONGE wa nchi hii?, basi ukaona mfichiane SIRI huko? Au ni yale yale ya PIERE NKURUNZINZA, kumaliza muda wake akiwa bado kijana na hiyo kunogewa kuendelea kushika madaraka? Si ni wewe uliyesema CCM wakimpitisha Lowassa ungehama CCM? Si ni wewe uliyekuwa ukishangaa kuwa kuna mgombea mmoja amejitangaza kuwania urais katika nchi maskini hii huku akisema rais wa nchi lazima awe tajiri? Uje utuambie.

3. Mzee Kingunge baada ya oktoba 25, kijana wako John Pombe Magufuli akishaapishwa, chonde chonde, uje utuambie, nini kilikuondoa CCM? kukiukwa kwa utaratibu wa kumpata mgombea wa CCM, utaratibu uliomnyima nafasi hiyo Lowassa? Lakini mbona hata mwaka 1995 alikatwa, mbona haukujiondoa CCM, au ulimuogopa Mwalimu? Au umeondoka kwa sababu CCM ya leo siyo ile ya Nyerere, lakini mboa inakosa mwelekeo baada ya Lowassa kukatwa au LOWASSA ndiye alikuwa CCM na CCM ilikuwa ni LOWASSA? Au tuamini maneno yanayosemwa huku uraiani kuwa UNATAFUTA AJIRA KWA LOWASSA baada ya umri wako sasa kuruhusu upumzike kwenye ajira za serikali na chama? Mzee KINGUNGE, la muhimu: UJE UTUAMBIE KATIKA UTUMISHI WAKO SERIKALI NA KWENYE CHAMA TUKUKUMBUKE KWA LIPI? Hili la kuhama CCM ukiwa na umri wa zaidi ya miaka 80, hapana shaka TUTAKUKUMBUKA nalo daima.

4. MWAPACHU, njoo utueleze kuhusu hayo tulionayo KIU kwa Mzee Kingunge.5. Wafuasi wa CHADEMA na hasa vijana, mmewaita majina mengi sana, vijana wa CCM na hata wasiyo wa CCM lakini hawako upande wenu. Mmewaita wasaliti, wasiojitambua, hawana akili, wako CCM kwa sababu wazazi wao wako ni mabalozi wa nyumba 10 n.k. na kwa sababu nami nayaandika haya, nawaruhusu mniite msaliti, nisiyejitambua, mjinga, mzazi wangu ni balozi wa nyumba 10 n.k. Nasema yote ni sawa ni haki yenu na hiyo ndiyo siasa yenyewe. Ila sikubaliani nanyi kuwa ujanja ni kuwa CHADEMA, kijana anayejitambua ni yule alioko CHADEMA, kijana mwenye akili ni yule anayeimba wimbo wa mabadiliko. " NI UJINGA KUAMINI KUWA MJINGA NI YULE ALIYEKO CCM NA MJANJA NI YULE ANAYEIMBA WIMBO WA MABADILIKO YA KUFUATA UPEPO". Lakini vijana na wote mnaopanda basi moja la Mabadiliko na LOWASSA, baada ya rais wenu, John Pombe Magufuli kuapishwa mje mtuambie haya:
1. Ni kweli mlikuwa mnamaanisha Lowassa na historia yake angetufaa au mlikuwa mnafuata tu mkumbo baada ya kuyasikia maneno matamu matamu kutoka kwenye vinywa vya wanasiasa na hivyo KUVURUGWA mpaka msijue hili wala lile? Si ni nyie mlikuwa mnapanda basi moja na Dr. Slaa , basi la kupinga mafisadi?
2. Mlijiridhisha kabisa, kauli za awali za viongozi wa CHADEMA dhidi Lowassa zilifutika kabisa akilini mwao na kumuona msafi? Kauli ya Mbowe-LOWASSA ni Dhaifu, Tundu Lissu- CCM wamempa fomu Fisadi kugombea urais ni hatari, John Mnyika- nina ushahidi wa Ufisadi na wizi wa Lowassa, Peter Msigwa- anayemshabikia Lowassa akapimwe akili, Godbless Lema- Ni hesima kubwa kwa Mungu kumzomea Mwizi na Muongo, Mabere Marando- Tunajua mengi kuhusu Lowassa ila CCM wameyasema mengine, SUMAYE- CCM wakimpitisha Fisadi nahama chama n.k.Mko waengi wa kuja kutueleza mlikuwa mnamaanisha kweli au mlikuwa mnatania?
Majibu sahihi yanahitajika kutoka siyo kwenu tu, bali na wale ambao sikuwataja kwani mko wengi,muda usingetosha niwataje wote, Makapi yote kutoka CCM ni miongoni mwenu.
Bila ya majibu sahihi, ni hatari sana kwa msatakabali wa Taifa hili kiuchumi, kijamii na kiusalama , Taifa likiendelea kuwa na watu WANAFIKI WENYE USHAWISHI MKUBWA KWA WATU WAKE, HAKIKA HATUWEZI KUSONGA MBELE HATA KIDOGO.
 
hayo maboya hatuna muda wa kuyasikiliza baada ya October 25 ni kazi tu! maneno kidogo kazi kwa kwenda mbele
 
Kiapo mahakamani wakati wakitoa ushahidi wa ukiukaji wa taratibu wakati wa uchaguzi labda. Ikulu ina wenyewe nao ni UKAWA na LOWASA.
 
Ujinga mtupu,haya sisi wananchi tunaopenda CDM/UKAWA tuje tukwambie nini?
 
Pombe Hafai Kuwa Hata Katibu Kata Kwani ni Muhasherati Kupindukia
 
hiyo lugha umetumia ndio ustaarabu. hayo ndiyo mabadiliko tunapeleka ikulu? si mlisema CCM ndio watukana. Mzee Mkapa alikuwa sahihi kumbe kweli ni wapumbavu. mnalipiza visasi.ikulu haiwafai kabisa.
 
Back
Top Bottom