Baada ya mafuta, sasa ni nyanya zinafuata kupanda bei. Kuna jambo la kujifunza hapa?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
Kuna mambo yanaendelea kimya kimya sana na kuathiri jamii.

Baada ya mafuta kupanda ngano kupanda sasa ni nyanya zinafuata

Je, wajua sababu ni nini? Sababu ya kupanda kwa bidhaa za vyakula kutoka bidhaa hii kwenda ile ni kwa sababu ya jambo moja ambalo wengi hamjalifahamu.

Ni kwasababu kwasasa sisi kama nchi ni kama tumeipuuza sekta ya kilimo kumbuka enzi za sera ya kilimo kwanza halafu sasa tulisema ni viwanda.

Tumetilia mkazo kwenye viwanda lakini bado hatujafanikiwa kufikia hata asilimia 5% kati ya 100% ya kuwa na angalau viwanda vidogo.

Tume-invest kwenye mambo mengine tumeacha kilimo serikali yetu sasa haijakipa priority kilimo kabisa ingekua tumekipa priority kilimo amini nakwambia Tanzania ingekua ndo nchi inazalisha zaidi kwa sekta ya kilimo Africa na tungeexport mno nje na hapa bongo mfumuko wa bei ungebaki stori.

Mimi sikatai sera ya viwanda i agree 100% ila wakati tunaimba viwanda tungeimba na kilimo yaani vyote viende sambamba aminia nakwambia tungekua mbali.

Imagine tuna-invest kupeleka maji singida na dodoma kutoka ziwa Victoria au mabwawa makubwa tukajenga kwa kilimo tukaanzisha mkazo kwenye kilimo cha kufa na kupona huku tukitilia mkazo kwenye kutafuta masoko na viwanda hizi shida za kupanda bei kwa bidhaa na mfumoko zingebaki stori tu.
 
jiwe alisema hana chakula cha kugawa bure kwenye ubongo wake anajua hamna lolote la kumfanya.

Yuko bize sasa hvi nakuzindua viwanda lkn anasahau kilimo na kiwanda ni pacha ukiachana na viwanda vingne visivyohusu kilimo
 
Hivi Bakhresa kama aliweza kutuletea nazi za paketi anashindwaje nyanya.
 
Wakulima wa nafaka kama vile mahindi na mchele wanalia. Soko la uhakika tumeriharibu kwa kukosa maarifa ya uchumi,diplomasia na siasa za kimataifa.
 
Ndio
jiwe alisema hana chakula cha kugawa bure kwenye ubongo wake anajua hamna lolote la kumfanya.

Yuko bize sasa hvi nakuzindua viwanda lkn anasahau kilimo na kiwanda ni pacha ukiachana na viwanda vingne visivyohusu kilimo
 
Back
Top Bottom