Baada ya madereva wenye vyeti fake kutimuliwa Ajali za STK, STJ, SU na DFP zimeshamiri

Namshangaa sana mleta mada. Ajali huwa zina sababu zake za kweli. Kusema ni kwasababu ya laana ni uvivu wa kufikiri. Kabla ya serikali kukazia kuwa mabasi yasizidishe speed ya Km80/saa tumeshuhudia kupungua kwa ajali kwa kiwango cha kuridhisha. Zilikuwepo nadharia kwanini kuna ajali nyingi za mabasi ikiwemo nadharia ya watu kutolewa kafara. Ni wakati sasa pawepo sababu za kweli za chanzo cha ajali hizi kwa magari ya serikali (haiwezekani ikawa laana).

View attachment VID-20181024-WA0002.mp4
 
True udereva sio vyeti, watarudishwa Membe akiingia 2020 na wote watalipwa mafao yao na waliobomolewa kimara watalipwa fidia.
 
Nacholiona hapa kila baada ya wiki 3 lazima gari ya.serikali ipate ajali na kuua

My take haya ni masononeko na laana ya familia zilizopoteza kibarua na wanapolala njaa hamuwezi kuwa salama na hii itaendelea hadi katika bila kujali cheo cha mtu watu wanalia kazi za udereva nikazi za kuitaji ujuzi na maarifa na sikuhitaji kwenda chuo kikuu maana akiwa ameenda NIT anaouwezo.wakulijua gari hawa wazee mlio wafukuza laana yaje haitwaacha salama nasema hapa Serikali yangu iliteleza.
Ikubali ilipitiwa.
Kwani walikuwa hawana makosa walipofukuzwa?
 
Kwa utafiti mdogo niliofanya ndani ya miezi hii mi 2 ajali zaidi ya 5 zimetokea zikihusisha magari ya SU, STK, STJ na DFP mengi kati ya magari haya yamepata ajali usiku na yanaendeshwa na madereva wapya baada ya wale wazoefu kutimuliwa kwa vyeti fake.
Tatizo linaweza kuwa nini? Nilitegemea perfomance yao ingekuwa juu sana maana wana vyeti original.
Ndiyo kusema jinamizi linatutesa?
 
Back
Top Bottom