Baada ya machozi, sasa eti kura ya maoni...Are we really serious ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya machozi, sasa eti kura ya maoni...Are we really serious ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Mar 7, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda jana alizindua kampeni ya kupiga kura kuwabaini wanaojihusisha na mauaji ya Albino na Vikongwe kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Zoezi hilo la kampeni ya upigaji kura litaigharimu kila kanda inayojumuisha mikoa mitatu Sh206 milioni ambazo zitatumika kwa ya ajili ya usafiri na uhamasishaji. Hapa naona kwa mbali watu wanaanza kujipanga mkao wa kula.

  Inaniwia taabu kuamini kuwa serikali na vyombo vyake vya dola imeshindwa kupambana na wauaji hawa na sasa itajikita katika kupiga ramli. Bila shaka hiyo orodha itakapopatikana, kama kawaida atakabidhiwa mkuu wa kaya !! Mauaji ya Albino sasa yaelekea yataingizwa kwenye siasa maanake haiingii akili vyombo vya upelelezi vinavyolipwa na hela za walipa kodi vinashughulikia nini !!
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Duh! hii kali! Kumbe shughuli ni nzito, maana wanatumia milioni 206 tshs kufanya kitu ambacho hakina maana! Sasa kura za maoni ni opinion polls? Inatusaidia vipi? Pesa hizo zinafujwa kwa lengo gani? Tatizo ni kwamba we don't hold our leaders accountable!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Ni aina nyingine ya usanii ambao zitatumika pesa chungu nzima bila ya kuona manufaa yoyote.
   
 4. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Sasa "KURA YA MAONI KWA WAUAJI WA ALBINO" imezinduliwa, na wananchi wameambiwa watapiga kura zao kwa siri. Je wananchi watapata wapi progressive report ya mpango huu? Mbona SIRIKALI haiweki mchakato mzima wa huu mpango?
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Taifa lipo njia panda.
  Ntetema amefanya utafiti mpaka akagundua kuwa kuna maofisa wa polisi wanaohusika na mauaji hayo. Inawezekana kabisa kuwa alitumia lugha ya kidplomasia kutosema kuwa kuna mawaziri wanaohusika na uharamia huo.

  Huko nyuma yaliwahi kutokea mauaji Shinyanga. Waziri wa mambo ya ndani na yule wa usalama wa taifa walijiuzulu. Lakini wale waliokuwa na wajibu wa kusimamia usalama mikoani kwao (RPC na RSO) walihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miaka miwili. Hicho ni kipindi tulichokuwa na serikali. Leo hii baada ya waingereza kutufanyia uchunguzi wote na kugundua kuwa Chenge katuibia kwenye ununuzi wa rada, bado unaambiwa kuwa Chenge si tu ni mbunge, lakini pia ni mjumbe wa kamati ya maadili ya chama chake. Hili linaweza kuelezwa kwa kifupi kuwa serikali ama haijui ifanye nini au inahusika moja kwa moja na haya yote.
   
 6. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kwa nini hizo Sh. Mil 206 zisitumike kuongeza idadi ya polisi na wapepelezi katika hizo sehemu husika badala ya kutumika katika upigaji wa kura, kweli nchi yetu tuna viongozi vichwa maji, woote akili mufilisi pumba tupu yaani mabwege mtozeni. Upigaji wa kura hautosaidia chochote katika kumaliza mauaji ya ndugu zetu albino. Halafu unakuta wananchi wenyewe wametulia kimya kazi kupiga makofi na kukenua tu, hakuna kulalamika, hakuna kupinga.
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hizo Sh. 206 ni kwa kanda ya mashariki tu - sijui kanda ziko ngapi - 5 au 6 ? Kwa hesabu za haraka ni kuwa zitatumika zaidi ya shillingi bilioni moja eti kwa ajili ya usafiri na uhamasishaji. Je ni watu gani hao watakaosafiri na kuhamasisha na ni watu gani hao watakaohamasishwa ?

  Tunakumbuka Pinda alivyomwaga machozi bungeni akijutia kauli yake ya kuwataka vijana wa CCM kuwa msitari wa mbele kwa agizo lake la kuwaua wale wanaowaua Albino. Leo anazindua zoezi la kura za maoni za kubaini wanaojihusisha na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

  Hapo hapo hela za walipa kodi zaidi ya bilioni zinatengwa kwa wanaosemekana kuwa wahamasishaji - kweli hii yaingia akilini ? Wakati anatamka haya giza totoro linaikabili taifa kutokana na tishio la Dr. Idris Rashidi baada ya janja ya dili lake na Dowans kushtukiwa na kupigwa X.

  Hii tabia ya kuogopa kuyakabili matatizo uso kwa uso na kuanza kutafuta njia za panya kuyashughulikia inaleta kichefuchefu kwa jamii. Ni heri serikali ikakiri kuwa imezidiwa na haina tena uwezo wa kuongoza kuliko kuendekeza mambo yanawafanya wengine watuone kama majuha - hii ni aibu kubwa kwa taifa.

  Kama asemavyo Mwanakijiji, tumepiga kambi kwenye bonde la kashfa na sasa inaelekea tumeamua kulifanya bonde hilo makao yetu ya kudumu.
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu miradi ya kuisaidia CCM ishinde uchaguzi itapatikana na kuanzishwa kwa hali na mali.

  Jiandaeni na mradi wa kuwasaidia wasichana wanaopata mimba waanze maisha upya utakaosimamiwa na wizara ya afya, wizara ya kina mama na UWT!
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tunaomba Upinzani uitishe mgogoro wa Katiba la kama si hivyo wafuasi wa Sultani CCM wataikwamisha Nchi na kuifanya kuwa ngumu kuongozeka kutokana wafuasi hawa kuifilisi nchi vibaya tena bila ya huruma.
  Madaraka ya nchi yanatumiwa vibaya tena bila muelekeo kila mmoja anajiamulia kivyake vyake naona usalama wa Taifa uvunjwe na kwani umeshindwa kazi ,ikiwa wahusika ni vigogo na wameshindwa kuwataja ,hii ni wazi nchi imekwisha tekwa.
   
Loading...