Baada ya Maalim Seif na Wabunge kushindwa vijibweni, mvutano mwingine waibuka CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Maalim Seif na Wabunge kushindwa vijibweni, mvutano mwingine waibuka CUF

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Habarindiyohiyo, Apr 2, 2012.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mvutano mwingine umeibuka CUF baada ya Maalim Seif na wabunge kuweka nguvu kubwa katika uchaguzi wa kata ya Vijibweni na kuambulia nafasi ya tatu.

  Baadhi ya viongozi wa chama hicho wamesema kwamba madai ya Hamad Rashid kuhusu Katibu Mkuu Maalim Seif kushindwa kukiwezesha chama kujijenga kupata ushindi yamethibitika kufuatia chama hicho ambacho ndicho kilichokuwa kinashikilia kiti hicho cha udiwani kupoteza kiti hicho na kushindwa hata kushika nafasi ya pili.

  Katia uchaguzi huo chama kikongwe CCM kilifanikiwa kutetea kura zake kikifuatiwa kwa karibu na CHADEMA huku CUF ikishika nafasi ya tatu.

  Viongozi hao wanalalamikia nguvu kubwa ya fedha na wabunge pamoja na katibu mkuu Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa pili wa Rais yeye mwenyewe kuongoza kampeni katika kata hiyo na kushindwa.

  Viongozi hao wanadai kwamba Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtariro alitoa taarifa zisizokuwa za kweli kuhusu nguvu ya chama hicho katika kata hiyo hali ambayo ilifanya chama hicho kitumie fedha nyingi bila mafanikio.

  ....ndiyohiyo
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Rip cuf
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Watu msivyopenda kushiriki furaha za wenzenu. Hemu furahia ushindi Arumeru wewe.
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani Hawajui Mtatiro anamalizia Kasri lake Mbezi? Ha ha ha ha RIP KAFU
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pamoja na mambo mengine, kitu kingine kilichowaponza CUF ni kufanya kampeni za chuki dhidi ya chadema badala ya kupambana na ccm. Sisi tulijielekeza nguvu zetu kuwashawishi wananchi pamoja na kukabiliana na hujuma za ccm.

  CUF wakaingia mkenge wa kuishambulia chadema kwenye mikutano yao wakasahau kunadi sera, wakashindwa kujua kwamba wananchi waliwachagua 2010 kwa sababu ya kuchoshwa na mambo ya ccm, hasa vuguvugu la kuhamishwa kupisha mradi wa mji wa kigamboni bila malipo stahili.

  Jana wakati sisi tunafanya kila jitihada za kukabiliana na mamluki walioletwa na ccm kuisaidia, cuf wao wakaleta mabaunza wa kuja kuwapiga mawakala wetu, mmeshambulia mawakala wetu wa nje katika vituo vya ofisi ya WEO na Vijibweni s/m, na hivyo kuwasaidia ccm kutumia mwanya huo kupenyeza mamluki na kuwapigia kura, hasa vituo vya Nunge, Ofisi ya WEO na Vijibweni s/m.

  Kwa ufupi hakuna sababu ya kugombana kwakuwa inaonekana mlikuwa mmekubaliana na ccm kwamba lazima ashinde mmoja wenu, cuf ama ccm na hivyo mkashirikiana kuihujumu chadema.
   
 6. l

  lugano5 JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 4,342
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 5
  ccm B,2015 nayo itakufa
   
 7. N

  Nabihu JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  kuwen wa kwel kuwa kiwango cha wapiga kura kimeshuka toka wapiga kura elfu 4 n ushee mwaka 2010 mpk elfu 2 na ushee ushaguz wa jana wakat jumla ya wapiga kura wote ni elfu 10 na ushee.kwahiyo ukiwa unatumia akili zako za kuzaliwa utaona kuna ununuzi mkubwa wa shahada za kura.
   
 8. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapa umenena kweli kabisa wasilalamike kwa geresha zao tu Waliona ni Kata iende ilikoenda kuliko kuwa CDM kwa sasa CDM ndiyo tawala cha upinzani pekee cha ukweli
   
Loading...