baada ya lema kuvuliwa ubunge mikutano ya kimataifa yarejea arusha

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
kuna minong'ono inaendelea huku mjini arusha kuwa baada ya Godbless Lema kuvuliwa ubunge wa arusha mjini,mji huu umeanza kupata mikutano ya kimataifa ambayo ilikuwa adimu wakati wa ubunge wa Lema.
 
Kurudishwa kwa mikutano ya kimataifa Arusha ni mikakati ya Jk kulisuka upya baraza lake la mawaziri kutokana na ripoti ya CAG.

Mikutano ya kimataifa ilihamishwa Arusha tangu Kikwete alipoukwaa urais mwaka 2005, wakati mbunge wa Arusha akiwa Felix Mrema.
Nakumbuka Kikwete aliposhinda urais 2005 Mikutano yote ya kimataifa na kitaifa zote zilihamishiwa Ngurdoto, mpaka tukaanza kujiuliza kama Jk ana hisa Ngurdoto.

Wenye data wanaweza kufuatilia.
 
Mikutano ya kimataifa haito kama uyoga, inapangwa well in advance. Lema kaenguliwa ubunge hivi karibu na kwa vyovyote vile hii mikutano ilikuwa imepangwa regardless. Na kwa maoni yangu vurugu za Arusha zimeletwa na Jeshi la polisi na sio raia wala mbunge wa CHADEMA.
 
Mkuu kwani Arusha kuna vurugu!?
 
Hapo tunahitaji before-After study design kisha tumwage maoni yetu!

Ila naamini kabisa hiyo minong'ono ni ya kweli.
 
Acha kuwarubuni watu wa harusha ili wadhanie magamba wanawajali kumbe magamba ndio kansa ya maendeleo yao. We inaelekea uko radhi boss wako achukue mkeo/ mumeo ili mradi kibarua kiwe salama.
 
Aijalishi kwani ndo wamemzuia kwa harakati iyo mikutano hatujui tunanufaika nayo vipi.Kwanza likizo ya Kamanda lema Ina maana sana katika mageuzi ya kidemokrasia tumuombee afya njema na maisha marefu.Kwani bado tunamuitaji awe kiongozi wetu na Kama lema alisababisha mikutano isifanyike basi lema ana nguvu na mamlaka kuliko serekali iliyopo madarakani apa ni peoplsssssssssssssssssss.............mpka kieleweke Kamanda lema kaza buti tupo pamoja.
 
Acha kuwarubuni watu wa harusha ili wadhanie magamba wanawajali kumbe magamba ndio kansa ya maendeleo yao. We inaelekea uko radhi boss wako achukue mkeo/ mumeo ili mradi kibarua kiwe salama.
unajua mimi ni mrengo gani?au umepost kwa jazba tu?
 
Kuna uhusiano gani? Msipende kuongea ongea tu ili kuiridhisha mioyo yenu ilojaa propaganda tu!!!!!
 
Kwani Lema ndio alikuwa anatoa vibali vya mikutano na kuamua kama ifanyike au isifanyike?
 
Mleta mada anataka kutuaminisha umbea, hayo ni majungu hebu tuambie kwa takwimu ni mikutano mingapi ambayo ilipangwa kufanyika arusha lakini ukahairishwa kwa sababu tu Lema alikuwa mbunge. Na je hao jamaa wenye hiyo mikutano walikuwa hawana ratiba isipokuwa ratiba yao ilikuwa inasubiri lema atoke ndipo wafanye mikutano, hiyo itakuwa siyo mikutano yenye tija ila kitchen party. Na kama kweli CCM waliwahambia hao wazungu wasubiri Lema atoke ndipo waje basi tukubali hukumu ya lema ni ya kupanga. kwa mwenye akili timamu hawezi kuamini maneno yako labda utuambie kwa takwimu ni akina nani walikancell mikutano na sababu wakatoa kuwa shida ni uwepo wa Lema, vinginevyo huna kazi ila kupiga majungu mahali ambapo tunatakiwa kubadilishana mawazo ya kusaidia kujenga nchi hii.
 
kuna minong'ono inaendelea huku mjini arusha kuwa baada ya Godbless Lema kuvuliwa ubunge wa arusha mjini,mji huu umeanza kupata mikutano ya kimataifa ambayo ilikuwa adimu wakati wa ubunge wa Lema.

ni kweli kabisa utakuwa mpuuzi kuleta mkutano wenye wageni ambao baadaye wataingia mtaani katika mji ambao kila kukicha watu wanajali maandamano na fujo siyo hilo tu hata watalii ambao walikuwa wanalala arusha sasa hawana mpango huo,sasa ni nairobi ama watokako wanaingia katika ndege bomba katika hifadhi za taifa lakini hapa nani muathirika kila mkazi wa arusha kuanzia yule anayeuza nyanya mpaka matunda kwani bei imeanguka na soko hakuna
 
Kuna watu na viatu! Hivi watu wengine umbea unawasaidia nini!? Hamtulii bila ya kuchombeza, acha uchokozi wewe.
 
Back
Top Bottom