Baada ya kuwakashifu viongozi wa dini, Jk apongezwa na Mkapa family................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kuwakashifu viongozi wa dini, Jk apongezwa na Mkapa family.................

Discussion in 'Jamii Photos' started by Rutashubanyuma, Jun 7, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  President Jakaya Kikwete greets retired president Benjamin Mkapa during the consecration ceremony of Bishop John Ndimbo of the Roman Catholic Diocese at Mbinga in Ruvuma Region on Sunday. Right is former first lady Mama Anna Mkapa. (Photo by Freddy Maro
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,608
  Trophy Points: 280
  Kauli ya JK yawashangaza viongozi wa dini, wanasiasa
  Na Dunstan Bahai

  BAADHI ya viongozi wa dini na wanasiasa nchini wameishangaa kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba viongozi hao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya bala
  ya kuwakamata.

  Viongozi hao kwa nyakati tofauti walisema kama kweli kauli hiyo ina ukweli, ni kwamba serikali inawajua wahusika hivyo kuhoji kwa nini isiwakamate na badala yake Rais anaishia kulalamika kwenye majukwaa.

  Juzi wakati akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga kwenye ibada maalum ya kupewa daraja la Uaskofu na kusimikwa kwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, Rais Kikwete aliwataka viongozi wa dini kuacha kushiriki kwenye biashara ya kuuza dawa za kulevya na badala yake washirikiane na serikali katika kuidhibiti.

  Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Bw. Ponda Issa Ponda alisema kauli ya Rais inaashiria kuwa yeye (Rais) na watendaji wake (serikali) wanawajui wafanyabiashara hiyo haramu.

  "Mimi nashindwa kuelewa, kitendo hicho ni kosa, na sheria inapovunjwa haiangalii huyu ni kiongozi wa dini au la, inachukua mkondo wake dhidi ya watu hao," alisema.

  Alisema kabla ya Rais kutoa kauli hiyo aliyoiita ni ya kulalamika kwa wananchi, alitakiwa kuwakamata kwanza hao viongozi wa dini kisha kuuambia umma wa Watanzania kuwa nao wanajihusisha na biashara hiyo.

  Bw. Ponda alisema kuwa viongozi wa dini ni sehemu ya serikali, hivyo haipaswi kiongozi wa serikali kuwalaumu, bali kama wanafanya makosa, sheria ichukue mkondo wake.

  Mmoja wa maaskofu wa Kanisa Anglikana Tanzania ambaye alikataa kutajwa jina lake gazeti kwa vile si msemaji wa kanisa hilo, alizungumza kwa masikitiko kwamba Rais amewadhalilisha na kuwakosea adabu.

  "Kwa kweli Rais ametudhalilisha, hakututendea haki kabisa, ametukosea heshima kwani alichotakiwa ni kumtaja huyo anayedhani anajihusisha na biashara hiyo, lakini si kutaja kwa ujumla wetu," alisema.

  Askofu huyo alisema wao ni watu wa heshima na wanaoheshimiwa na jamii na hasa ikizingatiwa pia kuwa wanaisadia serikali katika kuwaongoza wananchi katika njia iliyo nyofu, hivyo hawajui hatma yao mbele ya jamii hiyo inayowaamini.

  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema kama rais anapata ujasiri wa kusema hayo, iweje asiwachukulie hatua za kisheria kwani hayo ni makosa ya jinai ambayo adhabu zake hazichagui kiongozi wa dini, serikali au mwananchi wa kawaida.

  Alisema serikali haiko makini katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwani aliyekuwa mbunge wa viti maalumu Marehemu Amina Chifupa, alijitoa mhanga katika kuisaidia serikali kuwafichua wafanyabiashara hao haramu, lakini serikali haikumtumia hadi akafariki dunia.

  Bw. James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema mfumo wa uendeshaji serikali ni wa kifisadi, kwani hata viongozi wamejawa na ubinafsi na ndiyo maana hata sheria hazisimamiwi ipasavyo.

  "Rais ameendelea kuimba ngonjera kila siku, leo kawataja viongozi wa dini, kesho ni wewe mwandishi, siku nyingine waganga wa kienyeji. Kama anawajui anasita nini kuwachukulia hatua," alihoji Bw. Mbatia.

  Alimshauri Rais kutumia madaraka yake kuwachukulia hatua badala ya kulalamika kama wananchi wa kawaida.
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Wacheni unafik, JMK hakumkashifu kiongozi wa dini yoyote, amesema bila kutafuna maneno kuwa wapo waliokamatwa wakijihusisha na dawa za kulevya.

  Ukweli ubaki kuwa ukweli, hivi ni kashfa ngapi zimeshawakumba viongozi wa dini? Si Tanzania tu bali duniani? kwani hawa viongozi wa dini ni malaika? Kikwete katoa wito kwa viongozi wa dini watoe ushirikiano katika kujenga Taifa lenye maadili.

  Ni nani leo ataekataa kuwa kuna baadhi ya wanaojiita viongozi wa dini lakini ndio wa kwanza kuvunja kanuni na maadili ya dini zao kwa makusudi kabisa?

  Wacheni siasa za chai maharage.
   
 4. M

  MPG JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Limbukeni huyo tumeshamzoea
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  unapenda sana kushabikia mambo ya udini,kama vipi waombe waislam wenzio uwe sheigh,inaonekana ukipata madaraka utasumbua sana jamii yetu
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  SOMA POST #1 HALAFU UONE NI NANI ALIYE ANZISHA MAMBO YA DINI?

  Sasa nakuuliza, irudie post yangu halafu unieleze ni wapi niliposema kitu ambacho kibaya na kinaashiria mambo ya udini? halafu soma hii yako, unataja dini mpaka kwa jina na kunitaka niwe nani sijui (sheigh) kitu ambacho hakuna katika uIslaam, halafu upime ni nani mdini hapo.
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kikwete grew up witnessing the exercise of leadership by his grandfather Mrisho Kikwete as a local chief and father as a District Commissioner in colonial Tanganyika and Regional Administrative Secretary and an Ombudsman in post-colonial Tanganyika and the United Republic of Tanzania.

  He spent part of his childhood moving from one area of country to another as his father was transferred to different outposts. He also spent a better part of his childhood in the village under the guidance of his grandfather. Kikwete became a natural choice for leadership in school and later in the party (TANU and CCM) youth movements.

  His leadership talents emerged at early stages in life. He was a student leader both in middle and secondary schools and at the University of Dar es Salaam. He was elected Chairman of the Students Council at Kibaha Secondary School and Deputy Head Prefect at Tanga Secondary School.

  He became very active in student politics at University. He was eventually elected Vice President of the Dar es Salaam University Students Organisation and de-facto President of the student government at the Main Campus in 1973/74. As a student leader, he spearheaded efforts to fight for student's rights and welfare. He was in the forefront in bringing about awareness and activism in liberation and anti-apartheid politics in the campus and the University community at large. He represented the Dar es Salaam University students and the students and youths of the African continent in several international conferences. Among such meetings were the International Youth Population Conference in 1974 in Bucharest, Romania.

  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/65343-jakaya-kikwetes-biography-2.html
   
 8. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ulimi hauna mfupa; tukubaliane mheshimiwa kateleza!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  'Hakuteleza', alikuwa 'anatania tu':confused2::shut-mouth:
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  wewe ndo umesababisha major afungiwe kwa KUKUULIZA KAMA UNAKULA SAHANI MOJA NA MAMA SALMA??
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kwa nini kateleza? kwani hujawahi kusikia madudu ya viongozi wa dini? Hajateleza na ukweli unabaki kuwa ukweli haufutiki.
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Haya, sema usemayo ukipigwa ban ni wewe, mimi naweka ukweli kama unaweza jibu kwa hoja. Unanini wewe? Kama huna hoja kazi kwako.
   
 13. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani kazi ya hili jamaa ni kulalamika au kuwabana wateule wake ambao wanashirikiana na hawa jamaa mpaka wanafanikiwa kuingiza madawa ya kulevya hapa nchini!

  Kwani yeye ni Mjumbe wa nyumba kumi kumi!

  Tunajua kwamba alilalamikiwa na baadhi ya Mashehe waliotaka kupewa pasi za kidiplomasia ili wafanane na akina Pengo. Eti kwa kupitia pasi hizo akina Pengo wanaingiza madawa ya kulevya!!

  Akili ya kusoma huna, Hata ya Kuzaliwa pia!!!
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kazi yake ni Rais wa Tanzania, sasa kama unajuwa majukumu yake tuwekee hapa, wacha pumba zisizo na mantik.
   
 15. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  napita tuuuuu ndugu zangu
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  inamaana hajui majukumu yake unamtaka mchangiaji ambie huyu jamaa sijui tulimtoa wapi ndiyo maana huwa anasema hauji kwanini tanzania ni masikini....
   
 17. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  faiza foksi hayupo hapa ku analyse points zozote bali kupinga/defend tu. na avatar yake ilivo anawadhalilisha sana wenye kuvaa hivo kwa imani za dini yao maana wataonekana nao ni hivo hivo. taabu sana
   
Loading...