Baada ya kuwaachia kwa mwaka mzima sasa kumekucha ! Ratiba ya mikutano ya Mh Lema Arusha hii hapa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,563
217,871
- MKAAZI WA ARUSHA USIKOSE.jpg


Ewe Mkazi wa Arusha hii si ya kukosa

Note : Tutaendelea kuboresha ratiba hii kwa kadri tunavyoletewa taarifa mpya .

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE
 
Mkuu mleta uzi si vibaya uwe unatuletea alichozungumza maana hicho ndio cha msingi. Lakini kutuletea picha za mkutano bila ujumbe wake unatunyima jambo la msingi.
 
Mkuu mleta uzi si vibaya uwe unatuletea alichozungumza maana hicho ndio cha msingi. Lakini kutuletea picha za mkutano bila ujumbe wake unatunyima jambo la msingi.
Natumaini wamejipanga vilivyo, na natumaini wanajitambua na kuitambua vyema hali halisi inayowakabili wao, na hasa taifa kwa ujumla.
Natumaini wana mikakati na ajenda ya kuwafikishia wananchi wanayoweza kuieleza kwa lugha rahisi na ikaeleweka barabara na wananchi hao.
Natumaini watakuwa na ushawishi kwa wananchi katika maswala mbali mbali (mapya) yanayotokea katika taifa letu sasa ambayo hayajawahi kutokea kabisa, au sasa yanatokea na kuyafanya yaonekane kuwa ya kwaida; kama watu kupotezwa, watu kutekwa, n.k.

Bila shaka wananchi hao wakielezwa kinagaubaga wataelewa, kwamba kutafuta na kuleta maendeleo, ambayo kila mmoja wetu anayataka katika taifa letu, hakuna lazima ya kutokee mifarakano katika jamii ndipo hayo maendeleo yapatikane. Hakuna sababu ya watu kuvunjiwa haki zao na kutotii sheria na katiba za nchi ndipo maendeleo hayo yawepo. Watu waelezwe, wataelewa.

Wananchi wataelewa sana wakielezwa kwa lugha rahisi na ya ufasaha kabisa, umhimu mkubwa uliopo katika kulinda raslimali za nchi yetu ili zitunufaishe wananchi wote. Wakati haya yanafanyika ni lazima pawepo na utaratibu wa kuyafanya kwa utulivu na akili. Sio swala la kutumia mabavu na kutangazia dunia kuwa tupo vitani.

Waelezeni wananchi nyinyi mngefanya/mtafanya nini ili pasiwepo vurugu zinazoweza kuleta athari ziszokuwa za lazima katika uchumi wetu.

Wananchi waelezeni, tokea mwanzo wa kuwepo uhuru wetu, elimu na kilimo vilitakiwa viendelee kuwa vipaumbele vya kudumu, vya kila mwaka katika mipango ya maendeleo yetu. Tumepuuza elimu sana, sasa tunaona madhara yake; na tusipoirekebisha haraka tutazidi kudidimia huku wenzetu, majirani wakianza kuvuna matokeo ya kuwekeza katika elimu.

Vyuo vyetu sasa badala ya kuwa vituo mhimu vya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu katika tafiti zake, sasa vinakuwa 'majalala.' Hakuna chuo hata kimoja chenye hadhi ya kuwa chuo cha kimataifa. Hii ni aibu kubwa.

Kilimo kilianza kidogo kunyanyuka, lakini nacho ni cha kubahatisha tu... kesho mvua zikikoma njaa inatunyemelea bila wasiwasi wowote. Elezeni vizuri, wananchi wajue, nyinyi mtafanya nini katika haya.

Ndio, wananchi watafurahi kusikia mipango yenu ya "Maendeleo yetu ya Viwanda." Uchumi wa viwanda hauji kwa kutangazwa tu, ni lazima pawepo na mbinu za kuuwezesha uwepo na kuimarika. Pamba inahimizwa kulimwa, viwanda vya nguo viko hoi. Ngozi, zinavushwa mipakani kwa sababu sisi ni wasemaji sana utendaji kidogo. Sukari je, tutaanza kuvuna lini!

Lakini mhimu zaidi, muwahimize wananchi watambue umhimu wa kupiga kura zao na kuwa na uhakika wa kura hizo kuhesabika katika uchaguzi wa viongozi wao. Wao ndio wenye jukumu la mwisho kabisa kuhakikisha kwamba kura zao hazipotei kwa kuchezewa na mtu yeyote awaye, na viongozi waliowachagua ndio hasa wanaotangazwa.

Muwasihi wananchi, na wahimizeni watambue madhara ya kuwapa CCM kura na wabunge zaidi ya nusu ya Bunge zima. Mtashindwa vipi kueleza hili kwa wananchi wanaoona mnavyodhalilika mkiwa huko Bungeni kana kwamba nyinyi nchi hii sio yenu?

Msiombe huruma, nendeni mkawahimize wananchi wawape kazi ya kuliinua taifa hili linaloelekea kudidimizwa katika siasa tulizokuwa tunazisikia kwa wengine.
 
Mbunge pekee wa upinzani aliyetumia ruksa ya mbunge kufanya mikutano ktk jimbo lake ni Mchungaji Msigwa, wengine walikuwa usingizini sasa wamezinduka
 
Mkuu mleta uzi si vibaya uwe unatuletea alichozungumza maana hicho ndio cha msingi. Lakini kutuletea picha za mkutano bila ujumbe wake unatunyima jambo la msingi.
nitajitahidi kuweka video ili ujionee na kusikia mwenyewe .
 
Mkuu mleta uzi si vibaya uwe unatuletea alichozungumza maana hicho ndio cha msingi. Lakini kutuletea picha za mkutano bila ujumbe wake unatunyima jambo la msingi.
nitajitahidi kuweka video ili ujionee na kusikia mwenyewe .
 
Back
Top Bottom