Baada ya kuugundua ugonjwa unaonisumbua, sasa nishaurini juu ya lishe

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Ni miaka 15, sasa nimeugua tumbo nawashukuru wanajf kwani hamkunitupa kila nilipokuja kuwaomba ushauri.

Nilizunguka hospitali nyingi hadi Muhimbili lakini ikawa bila-bila!Namshukuru sana dakatri wa 20 kunitibu yeye aliniweka wazi kuwa wakati mwingine mgonjwa anaweza kujitibu mwenyewe hasa kwa kuufuatilia mwili wake Jamani nilipima vipimo vya Bariam meal na Barium enema havikuleta majibu.

Daktari akaanza kunipa dawa za vidonda vya tumbo ambazo hazikusaidia baada ya kupima CT-SCAN,mishipa ya tumbo iligundulika kuwa imetanuka.

Specialist wa matumbo akanijuza kuwa huenda ni minyoo nikaanza kuitafuta na hatimaye nimegundulika nina amiba wengi ambao wamekuwa sugu nimepewa tinidazole kwa siku 10.

Sasa ninawaomba ushauri wa chakula dawa ili niweze kuwamaliza ,amiba hawa kani wamenifanya vibaya ,naomba mnijuze tafadhali .

Karibu kwa mawasiliano
 
dah pole inabidi nami nikaliscan tumbo uzembe uzembe sio mzuri kabisa kwa afya
 
Kha! Nakumbuka wakati niko form two niligundulika kuwa na Amoebiasis... Daktari aliniandikia vidonge vya fragili zaidi ya mia arobaini na tano pamoja na vidonge visivyopungua hamsini vya rangi mbili...

Nakumbuka muujiza wangu wa kwanza hapa maana nilimuomba Mwenyezi Mungu anisaidie katika kumeza vidonge vya fragil maana vilikuwa vichungu kama chloroquin.

Amini usiamin nilimeza vidonge mia arobaini na tano bila hata kusikia uchungu wa kidonge kimoja. Kwa kweli huu ulikuwa ni muujiza wa pekeee.
 
Kha! Nakumbuka wakati niko form two niligundulika kuwa na Amoebiasis... Daktari aliniandikia vidonge vya fragili zaidi ya mia arobaini na tano pamoja na vidonge visivyopungua hamsini vya rangi mbili... Nakumbuka muujiza wangu wa kwanza hapa maana nilimuomba Mwenyezi Mungu anisaidie katika kumeza vidonge vya fragil maana vilikuwa vichungu kama chloroquin. Amini usiamin nilimeza vidonge mia arobaini na tano bila hata kusikia uchungu wa kidonge kimoja. Kwa kweli huu ulikuwa ni muujiza wa pekeee.
Ulipona?
 
Mimi nilitumia vidonge 400!Unafuu hakuna.Napona kwa wiki mbili tu, wiki ya tatu ugonjwa unarejea upya!
 
Back
Top Bottom