Baada ya kuua mashirika ya umma, sasa tunaelekea kuua mifuko ya hifadhi za jamii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kuua mashirika ya umma, sasa tunaelekea kuua mifuko ya hifadhi za jamii.

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by MBUFYA, Sep 18, 2012.

 1. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mifuko ya jamii nchini ambayo inachangiwa na wafanyakazi imegeuzwa kuwa chanzo cha kulipia miradi ya serikali badala ya kuhifadhi jamii yaani wanachama wake. inasikitisha kuona kuwa, wanachama hawana maamuzi juu ya mifuko hiyo na kulazimishwa kuchukua fedha hizo baada ya kuzeeka. hii ni dalili tosha mifuko hii imefulia na haina pesa za kutosha:
   
 2. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimepata bahati ya kusoma vitabu vingi vy Mwandishi mahiri wa Vitabu Bwana Robert Kiyosaki,huyu Bwana ametoa vitabu vingi ambavyo ukivisoma kwa umakini unaweza kupata maarifa mengi sana yanayohusu mambo ya Mifuko hii ya Jamii.Anachotufahamisha ni kuwa Wafanyakazi tukiendelea kuitegemea Mifuko hii ili tunapofikia wakati wa uzee itusaidie tutakuwa tunajidanganya sana! Kwa mifano aliyoitoa hapo Marekani ni kama vile Wafanyakazi wanatapeliwa kwa kuwekewa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo wao kama Wafanyakazi hawana maamuzi nayo na kwa hapa kwetu Tanzania hali ndiyo inazidi kuwa mbaya zaidi,kwa mfano Ujenzi wa Jengo la Bunge fedha zake kwa kiwango kikubwa zimekopwa NSSF na mpaka hivi sasa ulrejeshwaji wa mkopo huo una utata. Jengo la Machinga Complex nalo halijaanza kurejesha fedha kutoka kwenye Mfuko wa Jamii iliyokopa na inaonekana ulipaji wake utakuwa mgumu baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kukiri kuwa Jengo hilo halitumiki kama ilivyokusudiwa hali ambayo inaweka rehani fedha za Wafanyakazi. Pia juzi juzi tu tumeona Raisi akizindua ujenzi wa Daraja la Kigamboni daraja ambalo linajengwa kwa fedha za mkopo kutoka PPF. Kwa kweli hali ya Mifuko hii ya Jamii Kifedha siyo nzuri na ndiyo maana kipindi cha Bunge lililopita Serikali ilileta Mabadiriko ya Sheria ambayo yangewalazimisha Wafanyakazi kusubiri mafao yao bila kulipwa kwa muda mrefu mpaka watakapo timiza kigezo cha umri wa miaka 55 hivyo kusababisha mtafaruku mkubwa. Tujifunze kutoka kwa wenzetu waliokuwa kwenye Mifuko hii kwa muda mrefu na matatizo waliyokutana nayo.
   
 3. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #3

 4. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  mtu anayekaa kusubiri pensheni toka mifuko ya jamii anaota ndoto ya mchana, mfanyakazi jifunze kufanya biashara ndogo ndogo ukiwa kazini bado with time expand biashara yako na nakuhakikishia ukiwa na nidhamu kwenye hiyo biashara hutakaa ufikirie "mifuko ya jamii"
   
 5. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,925
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesahau na makabachori wanaochota kias kikubwa kwa kupiga shell deals

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 6. Mtingaji

  Mtingaji JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 1,217
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mifuko ya Hifadhi ya Jamii hasa NSSF na PPF hapa nchini ni wizi mtupu wa fedha za wanachama. Sisi huku mitaani tuna SACCOS na zinatukopesha kwa mtindo tuliojiwekea, inakuwaje NSSF nao waanzisha SACCOS wakati huo huo wanasema wao siyo Benk ya kuwekea faida (interest) kwa pesa ya mfanyakazi?

  Tanzania hatujafikia viwango vya kutunza wazee waliotumikia nchi hii zaidi ya vigogo wa kisiasa pekee, hivyo tunapo acha kazi mtu aamue mwenyewe kwa hiari yake, ama achukue pesa zake ama aingie kwenye mfumo wa pension. Siyo kulazimisha kama walivyo tunga sheria ya unyang'anyi!
   
Loading...