Baada ya kutumia ARV jamaa anaota matiti

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
breast.jpg

BAADHI ya wanaume wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa za kurefusha maisha wamejikuta wakivimba matiti yao na kuwa makubwa kama ya wanawake.

Vilevile, wanawake wanaotumia dawa hizo wanalalamika kukutwa na matatizo kadhaa ikiwa ni pamoja na ulemavu.

Joseph Mkanda (43) amekumbana na tatizo la dawa hizo ikiwa ni pamoja na kuvimba matiti. Mwanzoni alihisi ni kutopata chakula bora, lakini akagundua kwamba ni aina za dawa anazotumia.

“Naona aibu sana kutoka nje ya nyumba yangu, kwani nimepata matiti kama mwanamke…. Naona watu wakiniona watanicheka,” anasema mwananchi huyo ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Mtwara.

“Nilipokwenda zahanati ya kijijini nikaambiwa hilo ni jambo la kawaida kwa watu walioathirika na Ukimwi, hivyo sijui la kufanya wala pa kwenda,” anasema Mkanda.

Mwanamke Salima Omar (36) mwenye watoto saba kutoka Mtwara anasema mwili wake umekumbwa na matatizo kibao tangu aanze kutumia dawa hizo. Mmoja wa watoto wake wa kike alifariki mwaka 2006 muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwake.

Hata hivyo, Salima ambaye ni mke wa Hassan, na ambaye mwili wake umejaa vipele, na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, anaamini hali hiyo inatokana na kutopata lishe bora.

“Madawa haya ni makali mno, usipokula vizuri ni lazima yataivuruga afya yako,” anasema na kuongeza kwamba kuna siku analazimika kuyatumia madawa hayo bila kula chochote hususan anapokuwa mgonjwa sana.

Mwanamke huyo anasema kuna wakati hayatumii madawa hayo kutokana na ukosefu wa fedha ya chakula, kwani mumewe ni fundi wa baiskeli na yeye (Salima) hupoteza fedha anazopata kwa kunywea pombe. Hali hiyo imemsababishia kuuza mbuzi wote wa familia yake ili kumudu maisha.

Kama zilivyo familia nyingi katika Wilaya ya Mtwara ambazo zinakabiliwa na upungufu wa chakula tangu mwaka 2007, Salima naye yuko katika mkumbo huo.

Vilevile, licha ya kuwa mwathirika, mwanamke huyo bado anaendelea kuzaa. Miezi mitatu iliyopita alizaa mapacha ambapo mmoja wao alifariki na mwingine hali yake ni mbaya.

Hata hivyo, wataalam wa tiba wamewashauri wanandoa hao kuacha kuzaa, jambo ambalo huenda wakakubaliana nalo.

Chanzo: Bongo Picha Blog
 
halafu ngoma dizain saa sita......ayaaay....sasa itakuwaje....?......
Kapendeza lakini....
asante mpwa kwa hii useful pikcha.......

Hahahahaha mwenzenu anaugulia lol
Kuna wadada watayapenda haya maembe yawe kama yao.
 
Hahahahaha mwenzenu anaugulia lol
Kuna wadada watayapenda haya maembe yawe kama yao.

mbona hiyo love garden imepiga break somewhere....ilitakiwa iterereke kwa mtiririko maalumu....ili kuongeza burdani kwa wifi yetu....
Dah...kila nikiimagine sipati picha wallah........
 
halafu ngoma dizain saa sita......ayaaay....sasa itakuwaje....?......
Kapendeza lakini....
asante mpwa kwa hii useful pikcha.......

saa 6........hahahahahahah Preta wewe!!umeyapenda eeh???
wataalam walituambia ARV inarefusha maisha tuuu, duuuuuuuuh kumbe inarefusha hadi matiti!!!
kwa hiyo hapa ni kuchagua matiti au kifo???
 
mbona hiyo love garden imepiga break somewhere....ilitakiwa iterereke kwa mtiririko maalumu....ili kuongeza burdani kwa wifi yetu....
Dah...kila nikiimagine sipati picha wallah........

Kweli wanawake kuna vitu vinawavutia wewe tayari umesha zimika na garden love
 
ashukuru mungu kavimba mathiwa!! angevimba hipsi na makalio ingekuaje!
 
saa 6........hahahahahahah Preta wewe!!umeyapenda eeh???
wataalam walituambia ARV inarefusha maisha tuuu, duuuuuuuuh kumbe inarefusha hadi matiti!!!
kwa hiyo hapa ni kuchagua matiti au kifo???

mbeee......bora matiti....
 
halafu ngoma dizain saa sita......ayaaay....sasa itakuwaje....?......
Kapendeza lakini....
asante mpwa kwa hii useful pikcha.......
Sasa Bibie huu uyuzifuli hapa ni wa nini? kuangalia tu ama kuna kingine?
BTW mm misi yu sana!
Mwanga twauona lini?
 
Sasa Bibie huu uyuzifuli hapa ni wa nini? kuangalia tu ama kuna kingine?
BTW mm misi yu sana!
Mwanga twauona lini?

ha ha.....uyuzifuli ni kwa macho tu ndugu yangu.....
Long time ujue.......habari za Gambia?
Sasa ufanye haraka.....kabla mwanga haujafifia.......
 
Back
Top Bottom