Uchaguzi 2020 Baada ya Kutumbuliwa, Gambo asaka Ubunge kwa nguvu.. agawa fedha kama njugu

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Licha ya Mrisho Gambo kuenguliwa nafasi ya Ukuu wa Mkoa wa Arusha,jambo hilo limeonyesha kutomtikisa hata kidogo kwani kwa sasa ndio kwanza ameendelea kujidhatiti kwa kuendesha vikao vya kujijenga anavyofanya katika nyumba ya serikali anayoishi .

Vikao hivyo vinafanyika Majira ya Usiku na mchana huku vigogo kadhaa wa ccm Mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Arusha,Joseph Masawe na mwenyekiti wa ccm Mkoa ,Zelothe Steven wakiwa miongoni mwa washiriki wandamizi wa vikao hivyo.

Inadaiwa kwamba Gambo kupitia Mwenyekiti Joseph Masawe amekuwa na jukumu la kukutana na wajumbe kadhaa wa kata Mbalimbali jiji la Arusha na kuwarubuni kwa kuwapatia fedha ili waweze kumpitisha siku ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho.

"Ukifika katika nyumba hiyo ya serikali karibu na mahakama kuu utaona gari za aina tofauti tofauti zikiingia na kutoka wakiletwa wajumbe mbalimbali kutoka kwenye kata ili kumsaidia gambo kumpitisha nafasi ya ubunge"

Gari zinazotaja kutumika ni Pamoja na gari ya mkurugenzi wa shule ya Green Valley, Yahaya Njarita ambaye amekuwa rafiki mkubwa wa Gambo na kila wakati gari zake zinatumika katika kusomba wajumbe kupeleka aidha katika nyumba ya Gambo iliyopo Muriet ama katika makazi ya serikali hapa mahakamani kuu.

Inadaiwa kwamba kwa sasa Gambo anafanyia mipango yake ikiwemo kugawa pesa kwa wajumbe katika nyumba ya serikali ambayo bado hajakabidhi ili takukuru na vyombo vingine vya usalama visiweze kumhoji.

Baadhi ya wanachama wa ccm na wananchi wameiomba taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa Takukuru Taifa kumchunguza Gambo kwani kuna fedha nyingi amejikusanyia kupitia miradi mbalimbali aliyoianzisha ikiwemo ukarabati wa jengo la Corona katika hospitali ya Mkoa Mount Meru,Ujenzi wa Nyumba za Polisi Njiro na nk.

Miradi mingi iliyoibuliwa na Gambo haikuwa na kamati yoyote yeye ndo kila kitu hata cheki zilizokuwa zikitolewa na wadau wa maendeleo ziliandikwa kwa jina lake kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kuchota fedha hizo muda wowote na kutumia anavyotaka.

IMG-20200619-WA0016.jpg
 
Ana kazi sana kwa sababu hata akipitishwa Arusha atapitaje huko CC ya CCM ? Kwanza wakubwa zake akiwa kazini walishampania sana kuwa asingepitishwa hata angepita kwenye mchujo ngazi ya mkoa.

Siasa za Gambo zingekuwa siasa chafu sana za kulipiza hata nikiangalia clip aliyosema anataka wanaCCM wafanye fujo sana

Akatafute kazi ya kufanya tu kwa kuwa siasa hataweza tena this time.
 
Ccm kwa fitna mko vizuri. Takukuru wange kuwa wajinga kama wapiga fitna wa Ccm watu wote wangekuwa mahabusu..
 
Wakati akianza Kufanya huo Upuuzi wake ( kama ni Kweli lakini ) namtaka ajiandae Kisaikolojia kwani Kesho Mtumbuaji atamkaanga mno tu Ikulu.
 
Back
Top Bottom