Baada ya Kutoswa Uwaziri: Shamsi aungana na wazanzibari wanaotaka Mamlaka Kamili ya nchi yao...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]Friday, December 27, 2013[/h][h=3][/h]



Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha alipokuwa akizungumza na WanaCCM kwenye jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani jana.


Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya jamhuri ya muungano Tanzania.

Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa mjini kichama amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.


Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.

Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduziu Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.

Amesema licha ya mfumbo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ziko huru badala ya kun'gan'gania muungano wa mkataba au serikali tatu akidai haiku salama na Zanzibar


Chanzo: Zanzibar Islamic news blog
 
index.jpeg


Shamsi Vuai Nahodha


Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya Jamhuri ya muungano Tanzania.

Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa Mjini (kichama) amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.

Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.

Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.

Amesema licha ya mfumo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ni Zanzibar huru badala ya kung'ang'ania muungano wa mkataba au serikali tatu.




ZNZ Islamic Blog
 
motive behind kwanini ayaseme haya salsa!yawezekana ni kuupoteza uwaziri wake?just trying to be curious.
 
Huyu ni ZITTO KABWE wa CCM? Sababu Yule Mmoja wa CCM toka ZNZ aliposema hivyo Walimvua UBUNGE na U-CCM

Sasa VUAI watasema nini kwake? OH he has tittle watampa CHEO anyamaze...
 
kumekucha sasa. hayo ni maumiu ya kutemwa nini maana kwanini aseme sasa?
 
Huyu Shamsha Vua simwelewi hata kidogo.
Miezi michache iliyopita alizungumzia faida za muungano kwa wazanzibar, alihoji wznz kung'ang'ania mafuta a gesi wakati wenzao wameshaanza kuvuna gesi na kusema wznz hawaoni watakuwa wanajinyima?

Pili, suala la mafuta na gesi mbona limeshaondolewa katika mambo ya muungano kitambo?
Mansour Himid kabla hajafukuzwa CCM alipeleka mswada BLW na kupitisha haraka haraka hata kama lilikuwa jambo lililogusa muungano.
Hakuna mtu wa bara aliyelalamika, sasa sijui anataka mafuta na gesi ipi iondolewe tena.

Tatu, wakati akisema mafuta na gesi yaondolewe amekiri kuwa kuendesha wizara ya ulinzi inahitaji gharama kubwa.

Kwa uzoefu wake katika wizara hiyo amelitambua hilo vema.
Sijui anadhani gharama hizo atazibeba nani maana kama unaondoa mafuta na gesi kwanini asiondoe ulinzi na usalama? Nani atalinda mafuta na gesi yao ambayo haimhusu Mtanganyika ?

Vuai anadai kiti katika UN na sarafu vinahitaji gharama kubwa.
Kwani kwa sasa nani analipia gharama hizo?
Mbona anakwenda kinyume na madai ya wznz kuhusu kugawana nafasi za ubalozi sawa?!!

Kwanini wznz waombe nafasi sawa za ubalozi wakati hawajui nani analipa gharama za nafasi hizo?
Hata mama Fatma Karume kalalamika sana kuhusu mabalozi kuwa 3 kati ya 30!!
Shamsi angeenda kwa mama Fatma amuulize gharama za ubalozi zinalipwa na nani?

Jasusi JokaKuu Mchambuzi FJM
 
Nilishasema siku nyimngi, hawa jamaa wanasumbuliwa na ubinafsi, wao chao ni chao ila chetu pia chao. Kelele ni pale wanapondolewa kwenye uongozi, hususani kwenye serikali Muungano ambako kama watu binafsi hunufaika zaidi.

Hata huyo Seif, siku akiukwaa Urais Zanzibar hamtasikia tena kelele za mamlaka kamili kwani atakuwa kaukwaa utukufu anaouota siku zote, hata leo hii Maalim Seif wa kabla ya serikali ya umoja ni tofauti sana na huyu wa leo.

Sasa huyo dogo wa Mwera, Nahodha, atabwabwaja saaana!!!
 
Huwezi kuwa na mamlaka kamili halafu usiwe nayo wakati huo huo kuhusiana na kitu hicho hicho! Ni sawasawa na kutaka kuwa uko kwenye ndoa na uwe single at the same time... u can't.

Sawa kabisa eti uwe na mamlaka kamili halafu bado utegemee mbeleko?
 
Huwezi kuwa na mamlaka kamili halafu usiwe nayo wakati huo huo kuhusiana na kitu hicho hicho! Ni sawasawa na kutaka kuwa uko kwenye ndoa na uwe single at the same time... u can't.
Hah ha ha huu mfano makini sana. Mtu anadai ana ndoa wakati fulani na wakati mwingine ni single pengine na home alone.

MM hawa jamaa muungano ni mzuri pale unapokidhi haja zao. Nahodha kasema gharama za ulinzi ni kubwa, sarafu yao ni ghali na kiti UN kinahitaji gharama. Hapa muungano ni muhimu sana kwa znz.

Well, mafuta na gesi hivyo havihitaji nguvu ya Tanganyika, vipo baharini na Muungano ni mbaya , kandamizi, unyonyaji na ukoloni mkubwa. Muungano haufai kabisa! znz yenye mamlaka kamili inahitajika.

Ni utamaduni ule ule wa wazanzibar kudai madaraka, ukiuliza gharama watakwambi hizo za Tanganyika yahe! Kudai vyeo ukiuliza mshahara wa wenye vyeo unatoka wapi utaambiwa Dar es Salaam.

Kudai bila kutoa ni utamaduni ati!
 
Mnafiki sana tena bora kaondolewa angeweza kulishawishi jeshi vibaya, na bado tutasikia mengi subirini
 
Back
Top Bottom