Huwezi kuwa na mamlaka kamili halafu usiwe nayo wakati huo huo kuhusiana na kitu hicho hicho! Ni sawasawa na kutaka kuwa uko kwenye ndoa na uwe single at the same time... u can't.
Mnafiki sana tena bora kaondolewa angeweza kulishawishi jeshi vibaya, na bado tutasikia mengi subirini
Hapana hawajalazimisshwa. Wanakuja katika bunge Dodoma wenyewe tena wanachukua na pesa 'haramu' za mkoloni Tanganyika.
Wanachagua makamu wa rais kwasababu ya uzanzibar na walishawahi kutupatia rais mzanzibar. Hakuna aliyewashikia kiboko hata siku moja.
Wana baraza lao la wawakilishi, wanapitisha miswada kama wa kuondoa mafuta na gesi, kuweka mipaka ya nchi yao, kuwa na wimbo wa taifa na bendera yao. Walichoshindwa kufanya ni mswada wa kuvunja muungano, huo hawajawahi kuandika hata siku moja.
Wameleta wajumbe wa tume ya Warioba tena wakidai nusu kwa nusu. Tume ya Warioba inaandaa rasimu ya katiba ya Tanzania. Kama hawataki muungano wasingeleta wajumbe.
Hawajawahi kuapeleka mswada wa kura ya maoni BLW au kwa rais wao. Kama wangetaka wangeshafanya hivyo.
Bunge la katiba linaandaliwa. Wanachotakiwa ni kutokuja hapo watakuwa na nchi yao. Hakuna atakayefungwa jela kwa kutokuja. Wao wanadai waongezewe wajumbe zaidi! Alah, hawataki muungano halafu wanataka wajumbe zaidi wa kitu gani?
Hawajalazimishwa kwasababu katika muungano uliopo wao ndio wafadika. Labda uniambie Mtanganyika anafaidika nini hasa kiasi cha wewe kudhani wanang'ang'aniwa?
Sawa kabisa eti uwe na mamlaka kamili halafu bado utegemee mbeleko?
Friday, December 27, 2013
Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha alipokuwa akizungumza na WanaCCM kwenye jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani jana.
Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya jamhuri ya muungano Tanzania.
Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa mjini kichama amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.
Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.
Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduziu Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.
Amesema licha ya mfumbo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ziko huru badala ya kun'gan'gania muungano wa mkataba au serikali tatu akidai haiku salama na Zanzibar
Chanzo: Zanzibar Islamic news blog