Baada ya Kutoswa Uwaziri: Shamsi aungana na wazanzibari wanaotaka Mamlaka Kamili ya nchi yao...

Alikuwa na nafasi yakufanya hivyo kipindi anawadhifa saivi hamna atakae msikiliza anatapatapa kurudisha umaarufu
 
Huyu Shamsha Vua simwelewi hata kidogo.
Miezi michache iliyopita alizungumzia faida za muungano kwa wazanzibar, alihoji wznz kung'ang'ania mafuta a gesi wakati wenzao wameshaanza kuvuna gesi na kusema wznz hawaoni watakuwa wanajinyima?

Pili, suala la mafuta na gesi mbona limeshaondolewa katika mambo ya muungano kitambo? Mansour Himid kabla hajafukuzwa CCM alipeleka mswada BLW na kupitisha haraka haraka hata kama lilikuwa jambo lililogusa muungano.
Hakuna mtu wa bara aliyelalamika, sasa sijui anataka mafuta na gesi ipi iondolewe tena.

Tatu, wakati akisema mafuta na gesi yaondolewe amekiri kuwa kuendesha wizara ya ulinzi inahitaji gharama kubwa.

Kwa uzoefu wake katika wizara hiyo analitambua hilo vema. Sijui anadhani gharama hizo atazibeba nani maana kama unaondoa mafuta na gesi kwanini usiondoe ulinzi na usalama? Nani atalinda mafuta na gesi yako ambayo haimhusu Mtanganyika ?

Vua anadai kuwa kiti katika UN na sarafu vinahitaji gharama kubwa. Kwani kwa sasa nani analipia gharama hizo? Mbona anakwenda kinyume na madai ya wznz kuhusu kugawana nafasi za ubalozi sawa?!!Kwanini wznz waombe nafasi sawa za ubalozi wakati hawajui nani analipa gharama za nafasi hizo? Hata mama Fatma Karume kalalamika sana kuhusu mabalozi kuwa 3 kati ya 30!!
Shamsi angeenda kwa mama Fatma amuulize gharama za ubalozi zinalipwa na nani?

Jasusi JokaKuu Mchambuzi FJM

kwa akili yako kwani hizo harama zinalipwa na nani? Kama sio serekali ya muungano fahamu tanganyika haiwezi kutoa gharama yeyote kwani haipo
 
Last edited by a moderator:
Ukiaangalia kwa makini kabisa utaona miaka yote waznz wamekuwa waking'anga'nia kujitenga wakati sisi tunawalazimisha kuwa nao, swali; kuna nini hasa watanganyika wanachong'ang'ania znz?
 
kwa akili yako kwani hizo harama zinalipwa na nani? Kama sio serekali ya muungano fahamu tanganyika haiwezi kutoa gharama yeyote kwani haipo
Sasa kama Tanganyika haipo, wazanzibar wanalalalmika kunyonywa na nani? Wazanzibar wanasema mkoloni wa bara, ni yupi huyo?
 
Ukiaangalia kwa makini kabisa utaona miaka yote waznz wamekuwa waking'anga'nia kujitenga wakati sisi tunawalazimisha kuwa nao, swali; kuna nini hasa watanganyika wanachong'ang'ania znz?
Hapana hawajalazimisshwa. Wanakuja katika bunge Dodoma wenyewe tena wanachukua na pesa 'haramu' za mkoloni Tanganyika.

Wanachagua makamu wa rais kwasababu ya uzanzibar na walishawahi kutupatia rais mzanzibar. Hakuna aliyewashikia kiboko hata siku moja.

Wana baraza lao la wawakilishi, wanapitisha miswada kama wa kuondoa mafuta na gesi, kuweka mipaka ya nchi yao, kuwa na wimbo wa taifa na bendera yao. Walichoshindwa kufanya ni mswada wa kuvunja muungano, huo hawajawahi kuandika hata siku moja.

Wameleta wajumbe wa tume ya Warioba tena wakidai nusu kwa nusu. Tume ya Warioba inaandaa rasimu ya katiba ya Tanzania. Kama hawataki muungano wasingeleta wajumbe.

Hawajawahi kuapeleka mswada wa kura ya maoni BLW au kwa rais wao. Kama wangetaka wangeshafanya hivyo.

Bunge la katiba linaandaliwa. Wanachotakiwa ni kutokuja hapo watakuwa na nchi yao. Hakuna atakayefungwa jela kwa kutokuja. Wao wanadai waongezewe wajumbe zaidi! Alah, hawataki muungano halafu wanataka wajumbe zaidi wa kitu gani?

Hawajalazimishwa kwasababu katika muungano uliopo wao ndio wafadika. Labda uniambie Mtanganyika anafaidika nini hasa kiasi cha wewe kudhani wanang'ang'aniwa?
 
Huyu Shamsha Vua simwelewi hata kidogo.
Miezi michache iliyopita alizungumzia faida za muungano kwa wazanzibar, alihoji wznz kung'ang'ania mafuta a gesi wakati wenzao wameshaanza kuvuna gesi na kusema wznz hawaoni watakuwa wanajinyima?

Pili, suala la mafuta na gesi mbona limeshaondolewa katika mambo ya muungano kitambo? Mansour Himid kabla hajafukuzwa CCM alipeleka mswada BLW na kupitisha haraka haraka hata kama lilikuwa jambo lililogusa muungano.
Hakuna mtu wa bara aliyelalamika, sasa sijui anataka mafuta na gesi ipi iondolewe tena.

Tatu, wakati akisema mafuta na gesi yaondolewe amekiri kuwa kuendesha wizara ya ulinzi inahitaji gharama kubwa.

Kwa uzoefu wake katika wizara hiyo analitambua hilo vema. Sijui anadhani gharama hizo atazibeba nani maana kama unaondoa mafuta na gesi kwanini usiondoe ulinzi na usalama? Nani atalinda mafuta na gesi yako ambayo haimhusu Mtanganyika ?

Vua anadai kuwa kiti katika UN na sarafu vinahitaji gharama kubwa. Kwani kwa sasa nani analipia gharama hizo? Mbona anakwenda kinyume na madai ya wznz kuhusu kugawana nafasi za ubalozi sawa?!!Kwanini wznz waombe nafasi sawa za ubalozi wakati hawajui nani analipa gharama za nafasi hizo? Hata mama Fatma Karume kalalamika sana kuhusu mabalozi kuwa 3 kati ya 30!!
Shamsi angeenda kwa mama Fatma amuulize gharama za ubalozi zinalipwa na nani?

Jasusi JokaKuu Mchambuzi FJM

Ukiongelea gharama uongelee na mapato. Unajuwa lolote kuhusu 10.02%?
 
Huwezi kuwa na mamlaka kamili halafu usiwe nayo wakati huo huo kuhusiana na kitu hicho hicho! Ni sawasawa na kutaka kuwa uko kwenye ndoa na uwe single at the same time... u can't.

Hili ni dongo la wazi kwa Mbowe wa chadema. Lilian vs Joisi.
 
[h=2]Friday, December 27, 2013[/h][h=3][/h]

Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha

Alistaafu lini, unafahamu maana ya kustaafu? huyu waziri aliachishwa kazi (kufukuzwa uwaziri)
 
Hili ni dongo la wazi kwa Mbowe wa chadema. Lilian vs Joisi.
Ukisikia umburula, uzezeta ndo huu, kuwaza vyama, watu wanaongelea ishu za kitaifa wewe unakurupuka na CHADEMA na Mbowe, think big!
 
Nilishasema siku nyimngi, hawa jamaa wanasumbuliwa na ubinafsi, wao chao ni chao ila chetu pia chao. Kelele ni pale wanapondolewa kwenye uongozi, hususani kwenye serikali Muungano ambako kama watu binafsi hunufaika zaidi.

Hata huyo Seif, siku akiukwaa Urais Zanzibar hamtasikia tena kelele za mamlaka kamili kwani atakuwa kaukwaa utukufu anaouota siku zote, hata leo hii Maalim Seif wa kabla ya serikali ya umoja ni tofauti sana na huyu wa leo.

Sasa huyo dogo wa Mwera, Nahodha, atabwabwaja saaana!!!

Tunakushangaa sana unapiga makelele kwa jambo usilolijuwa., bora kama hukuwa na chakuongea ungekaa kimya tu
 
Friday, December 27, 2013

Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha alipokuwa akizungumza na WanaCCM kwenye jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani jana.

Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya jamhuri ya muungano Tanzania.

Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa mjini kichama amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.

Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.

Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduziu Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.

Amesema licha ya mfumbo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ziko huru badala ya kun'gan'gania muungano wa mkataba au serikali tatu akidai haiku salama na Zanzibar

Chanzo: Zanzibar Islamic news blog

watu wana madukuduku moyoni,wanashindwa kusema kwa kuwa ni viongozi na hii ipo ktk vyama vyote,kuwa watu wanamanung'uniko ila hawasemi kwa kuwa tu wapo ktk nafasi za juu na pindi wakitoka watasema tu
 
Uyu Shamsi amepotoka mara kama simke ndume., si ndo yeye huyu alisema mamlaka kamili ya Zanzibar yalishapatikana tokea Mapinduzi? sasa mamlaka gani tena anayoyataka yeye??

Mara zote wazanzibar wakidai mamlaka yao yeye ni No.1 alikuwa anabeza kwasababu alikuwa na fupa anabenya kule Tanganyika., saivi amepigwa na chini ndio anaanza kubana pua ama anaungana wazanzibar wanaodai mamlaka kamili., hawa watu wakoje???

CCM kwali kumbe ni shameless., na usishangae naye seif ali iddi akikosa pakushika akaja kusema naye anaungana na wazanzibari., si kwamba hawaelewi Tanganyika wanavyotukandamiza ila basi tu ujinga.,

Kama ni mwanamme kwanini maneno haya hakusema wakati ni Waziri kule Tanganyika?? haaaya welcome nahodha mtoto akinyea kiganja hakikatwi huoshwa lakin ww si mtoto tn sijuw tukufanyeje dumila kuwili.,
 
Wanajamii,

kwenye uchambuzi wa kina faida na hasara muungano kwa Tanganyika na kwa upande wa Zanzibar,labda tuanzie hapo tunaweza pata mjadala mpana zaidi,
 
Shamsi mbona leo ndio unakuja kuongelea haya ulikuwepo wapi?waznz sio watu wajinga wamekwenda shule wanajua kama nyinyi waroho wa madaraka mkifukuzwa kwenye serekali mnajiunga na upizani
 
Friday, December 27, 2013

Waziri Mstaafu wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Mhe Shamsi Vuai Nahodha alipokuwa akizungumza na WanaCCM kwenye jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Amani jana.

Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ndani ya katiba ijayo ya jamhuri ya muungano Tanzania.

Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa mjini kichama amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na gesi liondolewe kwenye muungano.

Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.

Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduziu Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa maendeleo ya ulinzi na usalama wake.

Amesema licha ya mfumbo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo, lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ziko huru badala ya kun'gan'gania muungano wa mkataba au serikali tatu akidai haiku salama na Zanzibar

Chanzo: Zanzibar Islamic news blog

Yale yale! Kwa hiyo kwenye gharama ( sarafu, ulinzi n.k.) kubaki kwenye Muungano (Tanganyika ibebe) lakini kwenye ulaji (mafuta, gesi n.k.) kubaki kwa Zanziba huru! Siasa za chako chetu na changu changu ziawasumbua. Hawawezi kufuta Muungano kwa sababu wanapenda dezo.

Amandla.......
 
Back
Top Bottom