Tetesi: Baada ya kutosaini EPA, lafuata la VISA ya utalii.

ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
2,965
2,000
Tanzania imejitoa dk za lala salama kusaini makubaliano ya visa ya pamoja ya nchi za Áfrika Mashariki kuhusu watalii kutembelea nchi yeyote ya AM kwa kutumia visa moja (common visa charged at $100 instead of $150 that each country charged before)

Ikumbukwe pia mwezi July mwaka huu Tanzania ilitosa kusaini makubaliano ya Economic Partnership Agreement (EPA) kati ya EAC na EU.

Nyuma kidogo ingawa hii ni kwa kenya pekee, Tanzania ilifanikiwa kumtongoza Uganda apitishe bomba lake la gesi TZ tofauti na mwanzo ambapo lilikua lipitie Kenya.

Kwa haya yote naona ni kama yanawagusa zaidi wakenya kuliko nchi zingine za AM. ni kwa sababu wana uchumi mkubwa zaidi kuliko nchi zingine za AM.
 
morenja

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
4,508

Tz ni mkia eac ukiondolea mbali wageni burundi na rwanda .Uganda ilipata kuongoza kwa uchumi eac kabla ya IDD amin na vita kuiporomosha hadi Leo.kwa sasa Kenya ndio inaongoza .Tanzania aijawahi ata Mara moja kuongoza .Sijui labda sasa kamaitaweza .na hii hali ya kuwa mkia ndio inayoihofisha na mbaya zaidi inapoona mbona ni kubwa na rasilimali nyingi inajihisi kama mshamba kaingia mjini na pesa zake kuona kila anaemsogelea ni mwizi anataka kumwibia .shida ndio iko hapo .salama ni mpaka wazee waishe kwenye mangazi ya uamuzi kije kizazi cha dotcom
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,520
2,000
Asante sana rais wetu mtukufu JPM. Barikiwa sana kwa hili na ni lazima wasome namba tu hawa wakenya wanatudharau sana.
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
6,005
2,000
Wanavyo vileta mezani kila mara havina tija kwa Tanzania. Vimeka kusaidia wao na sisi tunakuwa wasindikizaji. Na wanafanya hivyo makusudi kwa uhai wa nchi zao. Sisi tukiweka chochote mezani wanakirusha mbali. MF. single currency, mchepuko wa reli Mombasa to Arusha, hata mafuta ya Uganda tulikuwa tunapigwa teke la kisigino.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,108
2,000
Tanzania can market its own tourist attractions without the EAC.
La msingi tufanye juhudi zote watalii waje Tanzania moja kwa moja bila kupitia nchi jirani hasa Kenya!
Maamuzi ya lazima. Vinginevyo tutabakia kuambulia posho wakati vivutio vipo kwetu.
Wanaokuja kupanda Mlima Kilimanjaro wafikie Tanzania. Sio kula, kulala, kununua souvenir Kenya harafu kuja Tanzania kulipia tozo ya kupanda mlima tu.
 
kisikiji

JF-Expert Member
Feb 2, 2015
2,533

We umeona mbali mkuu. Kula like.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom