Baada ya kutoa mabandiko kuhusu hali ya Corona nchini, Kaimu Balozi wa Marekani aitwa Serikali kutoa ufafanuzi

Hawajamuweka ndani? Wamuweke ndani mara moja kwa kosa la kuchapisha maudhui potofu. BTW wanafikiri Marekani wanakaa kizembe zembe na hawana details za kila kitu kinachoendelea Tanzania? Ni nini kazi ya CIA? Wanajua mpaka idadi ya vifo halisi vya korona japo walizika usiku kwa kujificha.

Kabisa
 
Muwekeni ndani muone cha mtema kuni
Kutomweka ndani sio kwasababu ni Mmarekani. Ni kwasababu ni Balozi. Hata angekuwa Balozi wa Comoro, huwezi kumuweka ndani katika nchi anayowakilisha. Hata Balozi wetu Masilingi (Kiboko ya Lissu) Wamarekani hawawezi kumuweka nani kwa KOSA LOLOTE atakalofanya huko. Umenielewa dogo? Haya njoo unywe K Vant. Ahahahahahahahaj
 
Unafikiri sijui? Mbona nime-kejeli tu? Athibitishe nini wakati yeye anawapa raia wake hali halisi? Hujui nchi kama USA zinathamini sana sana usalama na uhai na raia wake na siyo kama hapa Bongo wanakoona uhai wa raia ni kama wa nzi tu?
In fact, tungekuwa ni watu wa ufahamu, picha hii waliyotuonyesha hawa watawala, kwa kuthamini uchumi zaidi ya maisha yetu, wakati huu wangekuwa katika hali ngumu zaidi.
Badala yake, eti ndio wanapiga kampeni kuonyesha jinsi walivyotuepusha na janga, wakati hakuna lolote walilofanya, na licha ya kuficha taarifa za ugonjwa huo.

Tanzania tunalo tatizo kubwa, kwa sababu tunakubali kufugwa kama mifugo na watu wasioelewa chochote.
 
Mtu mwenyewe hajaangaika na mitanzania yeye ameamua kuwa alert watu wa nchi yake ambapo kimsingi ni jukumu lake la kwanza. Hapa serikali imefanya utopolo mtupu. Mimi namuunga mkono balozi maana kwa hilo tangazo lake na mimi naponea humo humo kwa kuendelea kuchukua tahadhari. Acha wanaoficha maradhi waendelee hivyo hivyo.

Mnaomba misaada ya kupambana na Corona huku mnasema mumeifuta! 👋👋👋👋👋👋
 
Sisi tutaishia kutoa “masikitiko yetu” tu na ubalozi wataendelea kutoa travel advisory kwa raia wao ambazo kama Nchi hatuna mamlaka ya kuwazuia. Ukitaka kuepusha speculations, weka data hadharani
 
Mtu mwenyewe hajaangaika na mitanzania yeye ameamua kuwa alert watu wa nchi yake ambapo kimsingi ni jukumu lake la kwanza. Hapa serikali imefanya utopolo mtupu. Mimi namuunga mkono balozi maana kwa hilo tangazo lake na mimi naponea humo humo kwa kuendelea kuchukua tahadhari. Acha wanaoficha maradhi waendelee hivyo hivyo.

Mnaomba misaada ya kupambana na Corona huku mnasema mumeifuta! 👋👋👋👋👋👋
Duh

P
 
Hawa wakinyamazia uongo unaoenezwa na kundi hili lenye madaraka watakuwa wanashiriki uhalifu.

Wanachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kufichua uongo wote, kwa sababu uwezo wa kufanya hivyo wanao.

Watakuwa wanawasaidia waTanzania waliowekwa mateka kwa kufichua maovu yote wanayofanyiwa.

Tunataka watalii waje, halafu tunaficha taarifa mhimu za ugonjwa. Hizo serikali wanakotoka hao watalii watakuwa hawana akili timamu kutowaeleza raia zao hali halisi ya hatari iliyopo huko wanakotaka kwenda kutalii.

Ni wajibu wa serikali zao kufanya kazi hiyo.
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imemwita Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Imni Patterson ili kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.

Kaimu Balozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za ushauri wa kiusafiri (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19.

Ubalozi wa Marekani wasisitiza maambukizi ya Corona jijini Dar yameshika kasi. Wadai Hospitali zimeelemewa! - JamiiForums


Kama ubavu upo fungeni ubalozi wao. Hizi zingine ni mbwembwe tu na hazitobadili chochote.
 
Back
Top Bottom