Baada ya kutaka EAC kuwa Nairobi, sasa lake Victoria kuwa bila mipaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kutaka EAC kuwa Nairobi, sasa lake Victoria kuwa bila mipaka

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Ubungoubungo, Apr 13, 2009.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Taarifa ya habari jana, nimeona wanasema ati mawaziri wa Kenya na Uganda wametoa proposal kuwa ati mipaka iliyoko ziwa victoria ifutwe ili nchi hizi tatu zitumie hilo ziwa bila mipaka yoyote. yaani, wakenya wawe na ruhusa ya kuvua toka kisumu hadi bukoba hadi uganda jinja bila matatizo, hivyohivyo na kwa watz na waganda wavue popote pale ndani ya ziwa bila mipaka yoyote ile. nilishangaa, na ninaomba mtu mwenye data kamili hapa atuambie kwasababu naona kama ni ndoto.

  Baada ya wakenya kuvua visamaki vyao kule karibia na migingo kwenye kisehemu kidogo sana cha ziwa victoria wanachomiliki, wamemaliza kwa uvuvi haramu na wanataka sasa waje wavue na huku kwetu. patakalika kweli? au mnaonaje jamani tuwamegee kaeneo kengine ka ziwa ili sehemu yao ya ziwa at least iwe kubwa kidogo, kwasababu wanamiliki only 6% of the entire lake, kitu ambacho ni kidogo sana, ni sawa tu na hawamiliki. nawakilisha wajameni.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sijaipata hoja vyema, yaani wakija kuvua nchi jirani (mathalan waKenya aje kuvua upande wa Tz), nchi jirani inafaidikaje? hapo ndipo mjadala inabidi uanzie hapo.

  Kwa sababu kama nchi haifaidiki ni wazi huu utakuwa ni ujinga wa kupindukia.
   
 3. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Silioni tatizo sisi sote ni wafrika isitoshe jirani ,ndugu kwanini tuishirikiane ?
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ziwa victoria linamilikiwa na nchi tatu, kenya tz na uganda. wakenya wanayo nafasi yao na wanatakiwa kuvua samaki hadi mwisho wa mipaka yao ndani ya ziwa ndio maana wanagombana na uganda hadi sasa hivi kwasababu ya kisiwa kidogo sana cha migingo, pia kuna wavuvu wa kikenya wamekamatwa na waganda hadi leo hii kule migingo kwa mambo mbalimbali. tz wanavua hadi kwenye mipaka yao, vivyohivyo na kwa uganda. ndio maana watz na waganda wamekuwa wakiwakamata wavuvu wa kikenya mara nyingi pale wanapovuka mipaka ndani ya ziwa na kuja kuvua.

  hivi wewe, unasema kama wakenya wakija kuvua huku kwetu wanafaidika na nini? kwani si unaona wanavua maliasili/rasilimali zetu ambazo zinatakiwa kutuzwa kwa faida ya watz? halafu, huyo anayesema tusiweke mipaka kwasababu sisi sote ni ndugu, basi na mipaka yote ya ardhini iondoke, inawezekana? au ninyi nyote mlioongea hapa ni wakenya?
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wewe utakuwa Dar es Salam, hivi unasikia raha gani kuingia na ID nyinginyingi?
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Punguza jazba,

  Unajua unapokuwa na jazba wataalamu wanasema you can't even listen to yourself, yaani unakuwa kama possessed hivi.

  Nilichosema hapo juu ni kuwa kama mathalan Wakenya wanakuja kuvua Musoma, halafu sisi waTz tunakuwa hatufaidiki, makubaliano ya aina hii yatakuwa hayana tofauti na mikataba ya akina Sultan Mangungu wa Msovero.

  Nadhani umenipata.
   
 7. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sijakuelewa nakuomba ulirejee swali lako
   
 8. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nimekupata mkuu, sawasawa. cha ajabu ni kwamba, hivyo ndivyo wanavyotaka iwe. unajua wakenya ni kama wanatapatapa fulani hivi, ardhi yao ni ndogo, ziwa hawamiliki, maliasili ni kidogo sana. sasa mambo mengi wanapenda kufosi waje tz ambako kuna opportunity kubwa, ardhi ya kumwaga, ziwa la kutosha etc. tukiwa tunabana wanachukia na kutuona sisi kama hatufai. wanataka tukubali kama vile sisi ni mabwege fulani hivi. hii proposal wameitoa uganda walivyoenda kusuluhisha mgogoro wa wavuvi wa kikenya waliokamatwa na polisi wa uganda kisa wameiba mali za waganda kule migingo. the problem ni kwamba, wakenya wanawatetea wavuvi wao bila hata kuangalia kama ni kweli wameiba au la, hadi wametishia kuwa kama uganda haitawaachia wavuvi wake kenya yaweza kuchukua uamuzi wowote ule. hivi ndivyo walivyofanya kutulaumu hata sisi watz tulipowaua majambazi wao kule arusha na moshi, jambo ambalo limetukosti hadi leo hii polisi wa kiselikali kulinda mabenki badala ya vikundi vya ulinzi vya private. zaidi ya hayo, vikundi vingi vya private securities hapa ni makampuni ya wakenya.
   
 9. K

  Kalunguyeye Member

  #9
  Apr 13, 2009
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  U gatta be kidding me BJ ....!
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  So you can imagine how important we are to kenyans, we are a gold, diamond and life to them. mate yanawadondoka na hasa wanapoona sisi nasi tumeanza kunawiri, democrasia imeanza kuwa juu, wananchi wamechangamka kukamata mafisadi kitu kitakachoinua accountability kwenye uongozi then maendeleo kuwa juu haraka. wanaogopa watakuwa koloni letu si muda. mali hawana, ardhi kidogo. wanamendea eac wamiliki mali zetu, hasa ardhi, ziwa victoria, kila kitu.

  we need to merge with these people, lakini sio iwe federation, tuwe na mipaka sana na tushirikiane kibiashara tu, na sio kufuta mipaka ya nchi na ziwa letu. tunaweza kufuta baadhi ya tarrifs na vitu vya kodi kama hivyo, na hata hivyo, tuwe ne rules za kutosha za immigration ili nchi hii isiuzwe tukajikuta tunapoteza chetu kama walivyotupora kinguvu hisa za East africa airways ambayo imeiwezesha kenya airways kuwa juu hadi leo. sisi tumelala fofofooooo na air tz.walituwahi, sasa hivi tunavyoingia tuingie kwa akili, sisi sio mabwege tena. tutaingia kwa akili, tutashirikiana nao kwa akili na ikiwezekana tutaachana nao kwa akili.
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  God bless Tanzania. Mungu tusaidie tukamate mafisadi wote, na tuwafunge segerea miaka mingi. Mungu saidia wala rushwa mahospitalini,mahakamani,barabarani ne sehemu zingine za mikataba wote waaibike na wakamatwe. Tanzania tutashinda.kaza mwendo.
   
 12. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama kuna maeneo hatuyafanyii kazi na yapo tu kwanini tusitowe fursa kwa ndugu zetu wa east afrika ?ni kwa maslahi ya nchi zetu, na kama TANZANIA tunamaeneo ya zianda na ndugu zetu hawana kwa nin tusisaidiane.na kunda umoja wenye Nguvu.
   
 13. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  basi na mimi kama nyumbani kwako unayo magari matatu na huendeshi yote, naomba moja niwe naenda nalo kazini mzee. au vipi? hauelewi kuwa, kama hatuyatumii sasahivi, watoto wako wewe watakuja kutumia?watoto wako wewe watakuja kuvua samaki? au hata wewe ukipata mtaji utaweka kiwanda cha samaki? wakenya wameshafunga viwanda kadhaa kule kisumu vya samaki kwasababu samaki wachache kwenye kaziwa kao.
   
 14. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbuka tuna watu wengi kwa sasa hawana kazi naimnai zitatokea fursa nyingi kwa ndugu zetu kupata maisha bora pale miradi itakapo anza
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  1. Tz tusipokuwa makini na EA tutajajuta! Hili ni la Lake Victoria fikiria Kenya yenye 6% ya Lake ndo ina makao makuu ya kuratibu mambo ya samaki EA

  2. Ardhi Kenya ipo Mkuu!! sema wamepewa/gawana watu wachache kama familia za Kibaki, Kenyatta n.k. Yaani mtu mmoja kenya anamiliki kama Mkoa wote wa Singida yeye peke yake! Sasa kwanza wafanye Land reforms wawape watu wa kawaida pia ardhi Na sii kuja Tz kukimbilia ardhi yetu! Raha ya Tz angalau kila mtu ana ardhi ya kulima chakula chake! Kenya ni tofauti!
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wacha jirani, ndugu wanagombania mipaka sembuse jirani wa hivi. Mi nadhani tusifike huko. Mipaka ya ziwa iendelee kaama ilivyo. Cha msingi ni kuwa kama Wakenya ama Waganda wanataka kuvua upande wa Tanzania basi wa-apply kibali cha kuvua na sheria ifutwe. Wataanza hivi mara watasema mipaka kati ya Maasai Mara na Serengeti haina haja, mwisho watarudi kudai Kilimanjaro nayo iwe hivyo hivyo. Wajameni nasema hapanaaaaaaaaa! tuachwe na umbumbumbu wetu ambao tumekuwa nao, lakini mipaka ni muhimu.
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  mimi nlivyofundishwa ni kuwa umoja ni nguvu na muungano ni kitu bora. Tunataka tuungane kwani ulimwenguni sasa watu wanaungana na hivyo tuwaachie tunufaike sote na hilo ziwa.
   
 18. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  ni vizuri ungefikiria kabla ya kutoa kauli hii!!Tanzania tusipokuwa makini tutaanza kutawaliwa na waafrika wenzetu, rasilimali zetu tukizigawa hovyo maumivu yake yatakuwa ni ya milele.Wakenya, Waganda nk wakipewa fursa ya kuvua bila mipaka watz hamtapata nafasi hata ya kurusha nyavu,na mishangae kuja kusikia kila siku wavuvi wa TZ wameuawa ziwani.TANZANIA TAKE CARE!!!!!!!!!!
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sifikiri kuwa litakuwa jambo la ujinga kwa vile tunachotowa umuhimu hapa ni Muungano na Muumgano maana yake aliekuwa hana kitu akipate kwa mwenzake.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ALA!!!
  Mbona hii kauli yako haijakaa vizuri?
   
Loading...