Kyatile
JF-Expert Member
- Feb 5, 2017
- 1,727
- 1,565
Kwanza nianze kabisa kwa kusema kuwa sikuwa na sababu za msingi kuishabikia Simba.
Mara ya kwanza kuwa mshabiki wa Simba ni pale nilipojiunga na shule ya msingi darasa la kwanza. Muda wa mapumziko tukaenda kucheza mpira. Zikaundwa timu 2,moja simba na nyingine yanga. Nilipoangalia upande wa simba nikawaona watu wenye nguvu na wanajua mpira pale darasani, basi nikawa nikachagua kuchezea Simba na tangu hapo nikaanza kuishabikia Simba.
Baada ya kuwa mtu mzima nimeona sikuwa na sababu za msingi kuishabikia Simba na pia timu hii imeninyima raha kwa muda mrefu.
Tangu leo ninatangaza kujiunga na timu ya Kagera sugar nikiwa na akili timamu.
Sababu za kuishabikia Kagera:
1. Ni timu inayotoka katika mkoa wangu.
2. Ni timu inayofanya vizuri
3. Ninaipenda na kwa hiyo nitaweza kuivumilia.
Hata kama hawatachukua vikombe naamini itanipa raha pale itapokuwa ikishinda mechi. Nitaisapoti kwa nguvu zangu zote bila kukata tamaa. Sitakosa mechi ya Kagera itakayopigwa uwanja wa Kaitaba.
[HASHTAG]#NaipendaKagera[/HASHTAG]
[HASHTAG]#KageraNiTimuYangu[/HASHTAG]