Baada ya kushindwa, Mchungaji lazima ataanika kilichotokea hata ikibidi kwa kutotumia lugha ya moja kwa moja mradi tu ajisafishe mbele ya waumini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kwa jinsi alivyo-handle issue ya kijana yule wa Koromije kipindi kile, inaonyesha ni mtu asiekubali kushindwa au kusema akae kimya jambo lipite hasa iwapo ana taarifa au ushahidi wa kutosha kuhusu jambo husika.

Kwa msingi huo, kama kuna figisu zilifanyika kumbeba mtoto wa dada,basi nina uhakika wa asilimia 80 Mchungaji kufunguka walau kimafumbo mbele ya waumini wake Jumapili ijayo kueleza kilichotokea lengo ni kujaribu kulinda heshima yake mbele ya waumini wake.

Nasema haya kwasababu mtu huyu namuona hana uvumilivu wa kukaa kimya, na zaidi anaamini yeye si mtu wa kushindwa; hivyo, ni lazima atasema tu unless ameshindwa kihalali, ingawa hata akishindwa kihalali, bado anaweza kutumia maandiko kuhalalisha kushindwa kwake.

Tusubiri mahubiri yake ya Jumapili huenda itakuwa fursa nzuri ya kuju nini kilijiri katika mchujo wa leo.

Kama siyo Mchungaji kuanika kilichotokea, basi hata huyu mwenzetu wa hapa JF ambae nae kaangukia pua, anaweza kuja kutujuza kilichotokea japo kwa lugha ya mafumbo.
 
huyu Wa kwetu humu kashindwa kueleza, ila sababu kuu ya kushindwa ni kutoenda jimbo husika hata Mara moja angalau kwa kificho, hebu fikiria huyo MTU anaenda siku ya kuomba uteuzi, kinachofuata ni kura mbili au ziro, maana watu hawamjui
Huyu wetu siamini sana kama alishiriki ili ashinde, bali nadhani alishiriki ili wenye mamlaka ya uteuzi wamuone na pengine waje wampe uteuzi hapo baadae.The same to Mashinji.
 

Attachments

  • IMG-20200721-WA0113.jpg
    IMG-20200721-WA0113.jpg
    39.9 KB · Views: 1
  • IMG-20200721-WA0088.jpg
    IMG-20200721-WA0088.jpg
    47.4 KB · Views: 1
Mchungaji aseme nn ,wkt kuna ushahidi katoa rushwa kata ya Mikocheni, Msasani ,Kawe kwa baadhi ya wajumbe wapiga kura
 
Halafu anatangaza bifu na chadema, hao wajumbe tu mia mbili wamemtoa roho ndio ataiweza chadema,, arudi kwa kondoo wake, ila next time atapima kina cha maji kwanza, kabla kuyaoga.
 
kwa jinsi alivyo-handle issue ya kijana yule wa Koromije kipindi kile,inaonyesha ni mtu asiekubali kushindwa au kusema akae kimya jambo lipite hasa iwapo ana taarifa au ushahidi wa kutosha kuhusu jambo husika.
Nakumbuka wewe ulikua ripota wake humu na 'stay tuned'zako
 
Back
Top Bottom