Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Tayari baadhi ya taasisi zimeanza kuwaandikia barua wafanyakazi wao kuwajulisha juu ya kuchelewa kwa mishahara ya mwezi wa tano. Katika barua hizo inaelezwa kwamba hazina ipo kimya kabisa kuhusiana na suala la mishahara. Hata pale walipofuatiliwa, waligoma kuzungumzia suala la mishahara ya mwezi huu. Haijulikani, kama itachelewa tu au haitakuwepo kabisa kama ambavyo inatokea kwenye mikopo ya wanafunzi.