Baada ya kushindwa Gaza Wabunge wa Israel wahoji aibu iliyopata Israel hadi wanajeshi kutiwa mateka na Hamas

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,996
2,000
Baada ya kushindwa Ghaza, sasa Wazayuni walana wao kwa wao

Baada ya kushindwa katika vita vya siku 11 baina yao na wanamapambano wa Palestina, sasa wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamenza kupapurana wao kwa wao.

Wabunge wa utawala wa Kizayuni wamelaani udhalili iliotumbukia Israel kwa kukubalishwa kusimamisha vita na wanamapambano wa Palestina na wamesema kuwa, hiyo ni fedheha kwa utawala huo.

Mbunge Ayelet Shaked wa utawala wa Kizayuni amesema kuwa, kulazimishwa utawala wa Kizayuni kusimamisha vita bila ya masharti yoyote ni aibu na fedheha kwa Israel.

Mbunge huyo Mzayuni amemlaumu vikali sana waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu kwa kushindwa hata kuwakomboa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na wanamapambano wa Palestina huko Ghaza.

Mbunge mwingine wa Israel, Gideon Sa'ar kutoka chama cha "Matumaini Mapya" amesema, kulazimika utawala wa Kizayuni kusimamisha vita bila ya kupata mafanikio yoyote, ni kashfa na aibu kwa Israel. Mbunge mwingine Mzayuni amelalamika kuwa, kitendo cha Israel cha kukubali kusimamisha vita kwa sura hii ya aibu na udhalili ni hatari sana kwa utawala wa Kizayuni na kitauweka utawala huo katika wakati mgumu sana.

Muqawama wa wanamapambano wa Palestina

Wananchi wa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina walimiminika mitaani na barabarani kushangiria ushindi, sekunde chache baada ya kutangazwa kuanza utekelezaji wa kusimamishwa vita baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na wanamuqawama wa Palestina, saa nane kamili usiku kwa majira ya eneo hilo.

Baada ya siku 11 za hujuma na mashambulio ya kijeshi ya utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel, hatimaye jana saa nane usiku utawala huo ulianza kutekeleza usimamishaji vita kwa kuhofia vipigo zaidi vya makombora na maroketi ya wanamapambano wa Palestina.

4by18901a327211vgkg_800C450.jpeg
4bsm734eb72e531ir9w_800C450.jpeg
 

othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
2,636
2,000
Kama hali ile ndiyo Israel imeshindwa vita sijui ikishinda inakuaje

Lkn nyie akina mudy ndio mlikuwa mnalialia kwa kusema watu wenu wanaangamia sasa myahudi kawaacha mpumue bado mnasema mmeshinda vita

Ngojeni awamu ya pili sasa
 

Zero zone

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
1,388
2,000
Kama hali ile ndiyo Israel imeshindwa vita sijui ikishinda inakuaje

Lkn nyie akina mudy ndio mlikuwa mnalialia kwa kusema watu wenu wanaangamia sasa myahudi kawaacha mpumue bado mnasema mmeshinda vita

Ngojeni awamu ya pili sasa
Rejea kauli ya wazili mkuu Wa Israel utagundua kua walishindwa kufia malengo ktk hii vita
 

Bin Chuma75

JF-Expert Member
Dec 15, 2012
970
1,000
Kwa hiyo unataka kusema miungu ya kigeni imemaliza Vita vyao?

Allah amemshindaje Jehovah? Hebu fafanua maana tulikuwa tunaona Allah akipigwa kwelikweli.

Hebu tupe takwimu za vifo na majeruhi wa pande zote mbili
Kwa ninavyofahamu waisraeli sio wakristu,tena nao ni wapingaji katika kristu
 

Echolima

JF-Expert Member
Oct 28, 2007
3,783
2,000
Kwa hiyo unataka kusema miungu ya kigeni imemaliza Vita vyao?

Allah amemshindaje Jehovah? Hebu fafanua maana tulikuwa tunaona Allah akipigwa kwelikweli.

Hebu tupe takwimu za vifo na majeruhi wa pande zote mbili
Bora wewe umeuliza swali la msingi na sisi wengine tuweze kupata data za pande zote mbili!!!!
 

paschal Martin

JF-Expert Member
Jul 30, 2020
401
500
Yaani juzi dunia yote ilisimama kuiombea Gaza inateketea hadi waislamu wa huku Tanzania mlipanga siku ya dua leo mnawasifia hammas wameshinda wakati magorofa yamebaki vifusi Hamas wengi wamekufa mlitaka Israel iendele kuwaangamiza hammas
 

mud-oil-chafu

JF-Expert Member
Dec 27, 2020
309
500
Kama hali ile ndiyo Israel imeshindwa vita sijui ikishinda inakuaje

Lkn nyie akina mudy ndio mlikuwa mnalialia kwa kusema watu wenu wanaangamia sasa myahudi kawaacha mpumue bado mnasema mmeshinda vita

Ngojeni awamu ya pili sasa
Ushindi wa Hamas sio kuuawa Ila nu kukomboa ardhi ilivokuwa iporwe, ushindi wa Israel sio kuua Ila nu kupata Jerusalem
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom