Baada ya kushindwa Gaza mawaziri wa Israel waanza kuparuana

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Wazayuni wazidi kupapurana, sasa mawaziri wawashambulia majenerali wa kijeshi kuhusu Ghaza

May 22, 2021 06:34 UTC

[https://media]

Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni limelilaumu jeshi la utawala huo kwa kuboronga katika vita vilivyoisha juzi usiku vya Ukanda wa Ghaza.

Leo Jumamosi, gazeti la Kizayuni la Haaretz limewanukuu mawaziri wa serikali ya nchi hiyo wakisema katika kikao kilichohudhuriwa na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuwa, mashirika na taasisi za kijasusi za utawala wa Kizayuni hazina maana, zimeshindwa kuainisha maeneo muhimu ya wanamapambano wa Palestina hivyo utawala wa Kizayuni umeshindwa kuleta mabadiliko yoyote kwenye Ukanda wa Ghaza.

Katika kikao hicho cha Baraza la Mawaziri la Israel, mawaziri Wazayuni wamelalamika kuwa, jeshi la Israel halikupata mafanikio katika mashambulizi yake huko Ghaza na kwamba jeshi la anga la utawala huo limeshindwa kuvunja mahandaki mengi ya kiuilinzi ya HAMAS.

Baraza la Mawaziri la Israel vile vile limewalaumu makamanda wa kijeshi na kisiasa wa utawala huo kwa kushindwa kuanzisha vita vya nchi kavu huko Ghaza na kutosheka tu na mashambulizi ya anga.

[https://media]Wanajeshi wako Netanyahu bado ni mateka Ghaza



Mawaziri hao wa Israel wamehoji, ni vipi wanamapambano wa Palestina wameweza kuyapiga kwa makombora na matokeo maeneo mbalimbali ya utawala wa Kizayuni hadi sekunde za mwisho za vita hivyo huku jeshi la Israel likishindwa kugundua maficho ya viongozi wa ngazi za juu wa HAMAS kama vile Yahya Sinwar na Mohammed al Deif.

Baraza la Mawaziri la Israel limelilaumu pia jeshi la nchi hiyo kwa kushindwa kuzuia mashambulio ya makombora ya makundi ya muqawama huko Ghaza.

Mara chungu nzima makundi ya muqawama ya Palestina yamekuwa yakisisitiza kwamba, yataheshimu makubaliano ya kusimamisha vita, iwapo tu utawala wa Kizayuni utayaheshimu kikamilifu.



pichani:Wanajeshi wa Israel waliotekwa na Hamas
4bsm734eb72e531ir9w_800C450.jpeg
 
Juzi tu mlikuwa mnahimiza kuwa waislam wote duniani wapaze sauti zao kulaani uonevu wa Israel. Sasa leo Izrael kaamua kustopisha vita mnaona kama kawashindwa.
 
Back
Top Bottom