Baada ya kushinda uchaguzi mkuu kwanini waheshimiwa huzitupa timu zao za kampeni?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Ni kama kuna maushirikina ndani yake. Wengi ambao huwasaidia waheshimiwa wabunge kuingia mjengoni kwenye uchaguzi mkuu huwa wanasahaulika haraka sana.

Vijana na akina mama wengi hujitoa kimasomaso kuwapigania waheshimiwa wao washinde lakini pindi tu mtu anapoingia mjengoni hujisahaulisha sana. Huwatupa ndugu na jamaa waliosta nao kwenye kampeni.

Unakuta mtu anabadili namba ya simu na makazi yake. Vijana hubaki vijiweni kuiga miayo. Wakati usiku na mchana wamepigania na kulinda kura za mh. fulani.

Waheshimiwa husahau haraka sana wakishaingia tu mjengoni.
 
Hizo timu za kqmpeni zilikuwa zinatimiza wajibu wao ktk harakatu za kulinda na kutetea demokrasia. Siyo haki na vema kwa mbunge kuendelea kulea kikundi kilichokuwa kinamfanyia kampeni.

Akifanya hivi atalazimika kuwatenga waliokuwa wakimpigania mpinzani wake, jambo ambalo in hatari kwa ustawi wa jimbo.
 
Kama ulikuwa unapiga kampeni bila kukipwa ujira wako utakuwa ni mjinga. Baada ya uchaguzi kazi yako imeisha. Hivyo 2020 ukifanikiwa kuwa timu kampeni piga hela kwa hasira. Uchaguzi ukiisha katumie ulizochuma na ukiweza hata ww futa namba ya huyo uliyempigia kampeni asikuletee mazoea.
 
Si huwa mnanunuliwa, mnamalizana kabisa sasa utafutwe ili umsaidie kwa lipi. Ndio mjifunze 2020 msieendekeze njaa zenu kwa wagombea
[HASHTAG]#Kunywa[/HASHTAG] Maji Mwanangu
 
Kuto jitambua tu Mimi Mwenyekiti wa mtaa alikuja nimpigie debe kwakua nina ushawishi alikuwa akija mbunge tunaenda sambamba.mgao napewa ni kawa najiongeza sasa ni kawa na namba ya mbunge baada ya kushinda sikumuona na namba haipatikani ila nilimkamua. Asikwambie mtu wabunge kipindi cha kampeni wapole na mazuzu ukimwambia una vijana mia200 fungu linatoka bila kujiridhisha
 
Uchaguzi ukiisha maana yake kambi zote zinavunjwa na kuanza kufanya shughuli za maendeleo maana hao waliomsaidia ilikuwa ni kwa mapenzi yao lakini pia wanamwamini kwamba akiingia madarakani watashirikiana nae vizuri katika kuleta maendeleo
 
Wanasiasa ni watu wa kuwakamua tu. Ukifika wakati wa kampeni usiwaonee huruma.washenzi sana
 
Bado saini 278 tu kufikisha saini 1000 zinazohitajika kabla Avaaz hawajaichukua petition hii na kuiwasilisha kwa Kamishna wa Haki za Binadamu huko Umoja wa Mataifa achunguze ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania, hususan mamia ya watu "waliopotea" huko MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji).

Saini hapa Office of the United Nations High Commissioner for Human Rights: Investigate 100s of Missing People in Tanzania kisha sambaza Facebook, Twitter, Instagram na kwenye Whatsapp groups
Screenshot_20180520-115607_Instagram.jpg
 

Mungu akubariki Chahali katika hili umetimiza wajibu wako,nafahamu kazi wanafiki wengi watakutupia mzigo wa lawama lakini Mungu anauona moyo wako safi katika kufanikisha jambo hili jema kwa ustawi wa demokrasia na haki za waTanzania ambao hawakufikiri wangefikishwa katika hali hii ovu.

Ni ajabu waTanzania wengi tunakubali hali hii ya kusikitisha kuendelea kwakuwa Mama,Baba,Dada au shemeji zetu hawajagushwa moja kwa moja na madhila haya yanayoendelea kila ujio.

Kwa hakika Ndugu yangu Chahali nikimaliza kuchangia badiko lako nakwenda moja kwa moja ku sign hili jambo hili la hovyo lipate kuchunguzwa mara moja.
 
2015 mgombea X nilimkamua zaidi ya M. na akashindwa ila kaambulia usimamizi Wa uchaguzi.

nimeona watu wameanza kuwashwawashwa tena 2020 ingawa wanamuogopa jiwe, nimeshaanza kuwapampu wagombee ili niwavune hasa.

Hawa maviumbe usiyahurumie, yakamue kabisa hadi yakome.

2020 nakamua 2,500,000 namalizia na nyumba yangu.
 
Back
Top Bottom