Baada ya kushinda Igunga, Sasa tuelekee Mbagala!!

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Wakati mchakato wa kampeni ukipamba moto huko Igunga, yalitokea maafa ya nyumba kadhaa kuezuliwa eneo la mbagala na kusababisha wananchi zaidi ya 600 kukosa makazi, wengine kujeruhiwa na kukosa huduma nyinginezo za kibinadamu.

Kufuatia kinyang'anyiro hicho cha ubunge jimbo la Igunga na serikali yote kuhamia huko, hatimaye ccm imeweza kutangazwa mshindi.
Nawaomba wana ccm pamoja na viongozi wa serikali, baada ya kutoka igunga, ile huruma mliyoionyesha kwa watu wa Igunga muielekeze kwa wananchi wa mbagala. Tunafahamu jinsi mlivyokuwa wakarimu kwa kugawa vyakula kama mahindi, sukari na fedha ambayo ni posho kwa ajili ya wanaigunga kujikimu kutokana na uhaba wa chakula unaowakabili.

Wananchi wale wa mbagala nyumba zao zimeharibika vibaya/zimebomoka kwahiyo hawana mahali pa kulala, hawana chakula na hawana huduma nyingine muhimu za kibinadamu. Sasa ni muda muafaka kuwakumbuka na kuwakirimu kwa kuwa ccm ni wakarimu kwa wananchi wake.

Karibuni mbagala.
 
Hilo sahau mkuu, hadi pesa yao ya igunga irudi.

Bado matumaini yangu yako hai kwamba baada ya ushindi wa igunga, wataelekeza nguvu zao mbagala.

CCM na serikali yake ni wasikivu, na hili wanalisikia na watalifanyia kazi.
 
Sahau samaki kucheza na paka au kuwa tu marafiki mpaka warudishe ndesa zao za igunga....BYEEEEEEEE............
 
Potezea hiyo wao ni kushinda uchaguzi kwa sababu ushindi kwao lazima, hayo mengine mtajiju!
 
Sahau pesa imetumika igunga tena si kwa ajili ya maendeleo moja kwa moja ila kuweka mtu ambae hatuna hakika kama atasaidia kitu
 
Sahau pesa imetumika igunga tena si kwa ajili ya maendeleo moja kwa moja ila kuweka mtu ambae hatuna hakika kama atasaidia kitu

Kwahiyo pesa yote imeishia igunga? Nilisikia tetesi kwamba hata mishahara ya mwezi wa tisa imetoka dakika za nyongeza inaweza kuwa ni kweli?

Pamoja na hayo, kwa furaha ya ushindi wa igunga, lazima waje mbagala, hawawezi kutusahau haraka kiasi hicho.
 
Sahau, CCM ni ushindi tu, hayo mengine ni ya kwenu.

Mzee mukama, mwigulu nchemba, nape nnauye, january makamba na wengineo, bado tunawasubiri mbagala.

Nadhani jana mlikuwa mnasherekea ushindi wa igunga na leo mlikuwa mmejipumzisha kutokana na uchovu wa kampeni na safari ya kurudi dsm.

Sina shaka kwamba kesho tutakutana mbagala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom