kudamademede
Member
- Jan 1, 2020
- 62
- 241
Kwanza nikubali kwamba maisha yanabadilika kwa kasi sana siku kwa siku na hakuna namna unaweza kufanya yakusubiri mpaka uwe tayari.
Leo nimebahatika kupita barabara ya juu ya Ubungo interchange iliyofunguliwa hivi karibuni nikiwa njiani kuelekea Airport. Nikiwa juu nimepata mwanga fulani na kama ukipata muda pita hapo utabaini mambo kadhaa yafuatayo.
1. Tanzania imepiga hatua kubwa katika miundombinu kwa kipindi kifupi cha miaka mitano
2. Ukiwa juu ya barabara hii akili inakwambia hapa sio Tanzania maana barabara imejengwa kwa kiwango cha juu sana
3. Tunahitaji muendelezo katika maendeleo tusije kuangukia mikono ya mtu ambaye maendeleo kama haya kwake sio ya maana
4. Ujenzi siku zote ni kipimo cha hekima, kile unachokijenga ndio kinaonesha hekima yako. Magufuli apongezwe katika hili.
5. Tumechelewa sana kuwa na barabara za juu lakini tunaweza kukimbia tukafika mahali.
USHAURI WANGU
Magufuli anastahili kuendelea kuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi kingine. Mengi yanaweza kuongelewa lakini kwa kutia jitihada za kuelekeza mapato ya serikali vizuri.