Baada ya kupata Uhuru Z'bar kabla haijapinduliwa na Muungano (Z'bar to the United Nations in 1963) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kupata Uhuru Z'bar kabla haijapinduliwa na Muungano (Z'bar to the United Nations in 1963)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHIBUU, Jun 23, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  msikilize waziri mkuu wa zanzbar baada ya zanzibar kupata uhuru wake kamili kutoka kwa wakoloni weupe muengereza na kujiunga katika umoja wa mataifa,hii ni speech iliyoongelewa na waziri mkuu wa zanzibar,sasa wazanzibari tunatawaliwa na mkoloni mweusi,MUUNGANO.

  Mapinduzi yaliofanyika 1964 yalikuwa ni ya kupinduliwa wazanzbari kwa agenda ya waengereza kwa kumtumilia nyerere,nia hasa nikuitawala zanzbar kwa kutumia tekniki ya muungano,na kuidhibiti vikwazo vyote vya uchumi.

  Ukweli utaendelea kuwepo forever,naamini iko siku wazanzbari tutapata uhuru wetu na dola yetu muliotunyang'anya watanganyika kwa kisingizio cha muungano.
   
 3. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280  [​IMG]jee huyu pia ni muarabu ? huyu ndie alikuwa waziri mkuu kabla ya mapinduzi ya zanzibar, hapo ilikuwa mwana 1963 katika umoja wa mataifa baada ya kupata kujiunga na umoja huo na kutambulika kimataifa taifa la wazanzibari, na hapo juu ni video ya mapinduzi ya 1964,ukiangalia inanyesha zahiri walikufa ni watu weusi na wala sio waarabu,ni waislamu wa zanzibar,tena weusi wazanzibari halisi,historia yetu inapotoshwa na viongozi na wana ccm kwa kuficha maovu yao,hiyo ndio maafa ya nyerere kuitawala zanzibar na kuuwa usilamu zanzbar
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,595
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  Sultani Mwarabu. yeye alichaguliwa na Wazanzibari kuwa sultani kwa kura ngapi?. mbona waswahili wenzetu wasingeweza kuwa masultani isipokuwa Mwenye damu ya kiarabu tu? Mapinduzi daima!
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani hizi habari tulishazungumzia sana humu... Zanzibar ya mwaka 1963 haina tofauti na Rhodesia ya Ian Smith na unaweza kuandika lolote jema kuhusiana a na Smith kama wewe ni Kaburu.

  Zanzibar vile vile hakuna anayekataa Uhuru wao bandia wa kumrudisha Sultan madarakani na hakika Zanzibar iliekuwa mbele sana wakati wa Sultan kuliko leo, hii haina maana turudishe utawala wa Sultan bali tunaweza kufuata mipango ya maendeleo ya Sultan ktk kuboresha maisha ya wananchi.
   
 6. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Kwani utawala wa sultan ulikuwa na tatizo gani ? Au kwa sababu ulikuwa wa kifalme ? Mbona UK,Qatar,Sweden,Oman,SAUDIA ARABIA,Bahrain,na nchi nyengine watao watawala wa kifalme na nchi zao zimeendelea na hakuna tatizo lolote ?

  Hazi ni properganda za kisiasa tu,kuwa sultan akiwafanya watu watumwa,mohamed shamte utawala wake wa kifalme ulikuwa si wa kitumwa,na mwaka 1963 wakati tulipojinga katika umoja wa mataifa tulikuwa na mfalme wetu,na waziri wentu na wakilishi wetu,tulikuwa na serikali kamili,tulikuwa na dola kamili.

  Tunachokilia sasa hivi ni kwamba muungano ndio ulio tunyima uhuru wetu,uchumi wetu na dola yetu,tunaweza kusema ya kwamba bora wakati huo wa sultan ulikuwa wakati mzuri na maisha mazuri kuliko muda huu tulio nao,maonevu,hatuna haki,tunakosa haki zetu za msingi,kila kitu chetu kimekuwa cha muungano,wakati vya bara ni nyenu.

  Tunachotaka muda huu kuirudisha zanzibar kama vile ilivyokuwa kabla ya mapinduzi,simaanishi kuwa turejeshe utawala wa sultani,bali tunataka dola yetu huru,tunataka haya.

  Kuwa mwanachama wa umoja wa mataifa.
  Kuwa na jeshi letu la watu wa zanzbar,ulinzi uwe wetu wenyewe sio wa muungano.
  Tuwe na vyama vyetu vya siasa sio vya muungano kwani sisi tuna nchi yetu.
  Tuwe na maamuzi yetu sio kuamuliwa na bunge.
  Na mengineyo ambayo yataifanya zanzibar kiamataifa kuwa nchi.

  Ndio maana wazanzbari tunauchukia muungano,muungano tulionao wakati huu ni wa watu wachache tu,ni muungano wa TANU na ASP tu yaani ccm,lakini hakuna muungano.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna mtu kawakatalia kuichukua Zanzibar yenu? Ichukueni.

  • Vyama vya siasa si mnavyo japokuwa hakuna upinzani Zanzibar. Historia ya Zanzibar inaonyesha kupendelea muungano wa vyama: ZPPP na ZNP, ASP na CCM na sasa CCM na CUF
  • Vikosi vya SMZ - KMKM, Mafunzo
  • Baraza la Wawakilishi
  • Mahakama
  • BMZ
  • Bendera
  • Wimbo wa Taifa
   
 8. PongLenis

  PongLenis JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  wazenji kelele nyingi.. initiative hamfanyi....
   
 9. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Tumeshafanya za kutosha,na ndio maana sasa tumetulia,sasa tunaenda hatua kwa hatua,ila bado activities tutaendelea kufanya ikishindikana kutumia sheria,na vyombo vya sheria kuda dola ya zanzbar.
   
 10. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sijui tuite ni unafiki au nini! tungependa kusikia siku moja kuwa baraza la wawakilishi la zanzibar limetoa tamko/azimio kuwa zanzibar hawataki muungano ndipo tutakapojua kweli wazenj wapo serious na sio vitamko vya mtu mmoja mmoja! serikali mnayo, baraza la wawakilishi mnalo na ndo wawakilishi wa wananchi, kwa nini msitumie vyombo hivyo kutoa tamko la kutaka zanzibar kujitoa kwenye muungano? tunataka mfanye hivyo halafu tuone reaction ya serikali ya muungano then tujadili/tuone matokeo yake. Acheni kelele, chukueni hatua, hizo kelele zenu huwa nazifananisha na mtu anaetoa ushuzi wenye harufu kali inayokera lakini baada ya muda harufu hupotea halafu anatoa ushuzi tena ambao utapoa and so on, ndivyo mlivyo kila mara kelele kelele lawama lawama halafu kimya then mnaanza tena kero zenu lakini hamtaki kuchukua hatua madhubuti, acheni kulalamika utadhani nchi yenu imechukuliwa ikafichwa mahali fulani halafu alieficha hataki kuwaonesha! nchi mnayo wenyewe serikali mnayo wananchi wapo rasilmali mnasema mnazo sasa tatizo ni nini? eti tatizo Tanganyika/muungano! na tabia yenu ya kusema serikali ya muungano inawanyanyasa waislamu wa zanzibar tunaomba ikome,msitake kutuchonganisha watanganyika kwa misingi ya kidini, mtakapojitenga muondoke na kubaki na matatizo yenu, matatizo yetu tutatafuta njia ya kuyatatua. stop pestering us, we are sick and tired of your confusing complains!


  .
   
 11. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Mmoja ataka uvunjike, mwingine kura ya maoni Spika wa Bunge, Anne Makinda
  Mjadala kuhusu kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umefika pabaya, kufuatia baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar na Wawakilishi, kutaka Muungano huo uvunjwe kwa madai kwamba, unawapendelea wananchi wa Tanzania Bara na kuwaacha nyuma Wazanzibari katika maendeleo.
  Matamshi hayo yalitolewa na wabunge hao kwa nyakati tofauti walipokuwa wakichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana. Mbunge wa Micheweni (CUF), Haji Khatib Kai, alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano, ambayo iliunda mataifa mawili yakiwa na lengo la kuunda taifa litakalosimamia maendeleo ya nchi.
  Hata hivyo, alisema kinyume cha matarajio hayo, kila siku Wazanzibari wamekuwa wakinanung'unika zaidi kuhusu kubanwa na kero za Muungano, ambazo kila wakati zimekuwa zikizungumzwa bungeni, lakini hadi sasa serikali haijaeleza kama zimetatuliwa au la. "Wakati mwingi Wazanzibari wananung'unika zaidi kuliko Watanzania Bara.
  Wazanzibari imefika mahali hawana imani na Muungano huu kwa sababu wao ndio walio nyuma katika maendeleo, lakini ikiangalia Tanzania inasonga mbele," alisema Kai.
  Aliongeza: "Kwa hivyo, tunachokisema na tunachokiomba ikiwa serikali hii imeona kwamba Zanzibar imekuwa kikwazo ama imekuwa kero ama mzigo, basi ni vema watuache…narudia tena kusema ikiwa Zanzibar imekuwa mzigo na imekuwa kero, basi hebu tuachieni huo mzigo, uteremsheni kichwani ili muwe huru. La, si hivyo vinginevyo, basi afadhali Muungano huu uvunjwe, uundwe tena iwapo itawezekana."
  Kauli hiyo ilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kusubiri mchakato wa kuandika Katiba mpya ili watumie fursa hiyo kutoa maoni yao.
  Hata hivyo, kauli hiyo ya Spika Makinda haikufua dafu, kwani Mbunge wa Mgogoni (CUF), Kombo Khamis Kombo, naye aliposimama kuchangia mjadala huo, aliendeleza hoja ya Kai kuhusu kero za Muungano.
  Alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina wizara 26, ambazo kati ya hizo, sita ni za Muungano na kusema hali hiyo inamaanisha kwamba, mambo yote, ambayo si ya Muungano, yanapangiwa bajeti ndani ya serikali hiyo.
  "Mheshimiwa Spika, tuangalie kutakuwa na usawa gani katika Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar?" alihoji.
  Alisema licha ya kwamba mambo ambayo si ya Muungano yamezungumzwa kwenye Katiba, kimantiki hakuwezi kuwa na usawa katika Muungano kama wizara za Muungano ni sita na wizara zilizokuwa si za Muungano ni 20 na bajeti ni moja.
  Kombo alisema kama kweli serikali ya Jamhuri ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo ndani ya Muungano, anaamini mapendekezo ya JFC (Kamati ya Pamoja ya Fedha) yangelifuatwa kama yalivyo, lakini hayakufuatwa.
  Alisema anaamini hakuna ukweli wa dhati wa kutatuliwa kero hizo na kuitaka serikali ikae ikijua kwamba, imewafikisha Wazanzibari kuona kwamba, Serikali ya Muungano wa Tanzania inawadhalilisha.
  Kombo alisema kuna wanajeshi, polisi na wafanyakazi wengine Zanzibar, ambao wanatumia huduma visiwani humo, lakini hawalipi kodi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzinbar (SMZ), badala yake kodi zao zote zinaelekezwa Serikali ya Muungano.
  Alisema Serikali ya Muungano imekuwa ni ‘juja wa maajuja' kwa Wazanzibari kwa kuifanya Zanzibar haina haki wala uwezo wa kuweza kupewa nafasi ya kuitumikia Tanzania nje ya nchi. "Tuangalie mabalozi waliopo.
  Zanzibar ina mabalozi wanne tu. Na hawa wote hupangwa katika nchi za Kiarabu, nchi za Kiislamu. Isipokuwa Mheshimiwa Mapuri (Ramadhan Omar) labda kapelekwa China.
  Sasa niseme kwamba, Wazanzibari nao wana haki na uwezo katika Muungano huu na wana haki ya kupewa wafanyakazi kufanya katika ofisi za kibalozi," alisema Kombo.
  Alisema kuna kamati, ambazo huundwa mara kwa mara kushughulikia kero za Muungano, ikiwamo Tume ya Jaji Francis Nyalali, ambayo alisema ilikuja na mapendekezo yake, lakini mpaka leo hawajui yalikokwenda.
  Kombo alisema pia kuna kamati ya Shellukindo, lakini ripoti yake mpaka leo haijatolewa na pia kuna ya Amina Salum Ali, ambayo hadi leo haijatolewa na kuhoji: "Hivi tuamini kuna kamati gani itaweza kukaa kutatua kero za Muungano?
  Kutokana na hali hiyo, alisema haamini kwamba, Serikali ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo kwenye Muungano, hivyo, akamtaka Waziri Mkuu kusimamia jambo hilo ili lipatiwe ufumbuzi ili Wazanzibari waweze kujenga imani ya dhati.
  MWAKILISHI ATAKA KURA YA MAONI
  Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana alishauri Serikali ya Mapinduzi kuitisha kura ya maoni itakayoamua hatma ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
  Saleh Nassor Juma (Wawi-CUF) alisema kura hiyo itumike kupata maoni iwapo wananchi wa Zanzibar wanataka au hawautaki Muungano.
  Saleh alikuwa anachangia makadirio ya bajeti ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Baraza la wawakilishi jana, alisema walio wengi Zanzibar wanatofautiana kuhusu suala la Muungano uliofikiwa baina ya pande hizo mbili mwaka 1964.
  Alisema makubaliano ya Muungano yanainyima Zanzibar fursa ya kuongoza taasisi nyeti kama vile Idara za Polisi, Usalama wa Taifa, Jeshi na Bunge.
  "Mheshimiwa Spika, iitishwe kura ya maoni haraka … Zanzibar haijawahi kuongoza nafasi ya juu katika vyombo vya ulinzi na usalama," alisema.
  Saleh alisema kuwa marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yameipa Zanzibar hadhi ya kuwa nchi, hivyo pia ni lazima iruhusiwe kujiunga na Jumuiya Afrika Mashariki bila kupitia mgongo wa Serikali ya Muungano.
  Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakari Khamisi Bakari, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali kwa sababu uliridhiwa na wabunge kutoka pande zote za Muungano.
  Waziri Abubakari alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi, Omar Ali Sheha (CUF) wa Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.
  Alisema kwamba mkataba wa Muungano uliridhiwa na wabunge wote kutoka Tanzania bara na Zanzibar jambo ambalo linaonyesha uhalali wake.
  Alisema kwamba mkataba wa Muungano ulitakiwa kuridhiwa na Bunge na Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM) taratibu ambazo zimezingatiwa baada ya wabunge kutoka pande mbili za Muungano kuridhia mkataba huo.
  Hata hivyo, alisema kwamba jambo lolote linalotumika kwa muda mrefu bila kuhojiwa uhalali wake huwa ni halali kutokana na uwepo wake.
  "Muungano ni halali kwa sababu mkataba wa Muungano ulipitishwa na wabunge wakiwemo wa pande zote kwa utaratibu uliowekwa na katiba katika kupitisha mambo ya Muungano," alisema.
  Aidha, alisema kwamba mambo yaliyoorodheshwa ya Muungano hivi sasa yamefikia 22 kutoka 11 na sio zaidi ya 30 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
  Hata hivyo, alisema kwamba kwa mujibu wa katiba mambo ya Muungano hayawezi kuongezwa au kupunguzwa hadi ipatikane theluthi mbili ya wabunge kutoka Tanzania Zanzibar na Bara.
  Awali, Sheha alitaka kujua taratibu gani za kikatiba zimezingatiwa kabla ya mambo ya Muungano kuongezwa kutoka 11 tangu kufikiwa kwa Muungano huo mwaka 1964.
  Kwa upande wake, Mwakilishi wa (Viti Maalum-CCM), Raya Suleiman Hamad, alisema Muungano wa Tnganyika na Zanzibar umeleta faida kubwa ikiwemo kujenga umoja wa kitaifa kwa wananchi wake "Leo Ndugu zetu wapo Tanzania Bara ukivunjika waende wapi, jambo la msingi ni kurekebisha kasoro za Muungano kwa sababu umeleta faida kubwa kwa wananchi," alisema mwakilishi huyo.
  Akifunga Mjadala, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alisema Muungano umeleta faida kubwa na tayari kero mbalimbali zimepatiwa ufumbuzi kupitia Kamati ya pamoja ya kujadili kero za Muungano.
  Kuhusu utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar, Balozi Iddi alisema suala hilo haliwezi kutekelezwa kabla ya kufanyika marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kuwataka Wajumbe wa Baraza hilo kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kulitafutia ufumbuzi.
  CHANZO: NIPASHE
  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 12. PongLenis

  PongLenis JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  basi badala ya ku p[ost malala miko kila siku hebu siku moja weka thread ya mambo miliyofanikisha hadi sasa katika safari yenu ya kuelekea kwenye huo uhuru wenu,
   
Loading...